CUF, CCM kuinyongelea mbali CHADEMA bungeni

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
147
na Ratifa Baranyikwa

MKAKATI wa kukiengua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushika nafasi za uongozi katika kamati za bunge unaandaliwa, imefahamika.

Inadaiwa kuwa baadhi ya wabunge wachache wa CUF kwa pamoja na wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamewakamia wenzao wa CHADEMA kuhakikisha hawapati nafasi hizo.Mpango huo pia unadaiwa kutekelezwa nyuma ya pazia na vyama tajwa, kilieleza chanzo chetu.

Vyanzo vyetu vya habari toka katika ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam, ndani ya Chama cha CUF na CCM, vililiambia gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao kuwa sababu ya mkakati huo kwanza ni hofu ya nguvu waliyonayo hivi sasa CHADEMA katika idadi ya wabunge.

Sababu nyingine ni mgogoro wa kiuongozi ndani ya kambi ya upinzani baina ya CUF na CHADEMA.Kambi hii katika Bunge lililopita ilikuwa ikiongozwa na Hamad Rashid ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Wawi kupitia chama cha CUF.


Inadaiwa kuwa CUF haijafurahia kambi hiyo kuongozwa na CHADEMA na hilo ndilo lililosababisha waungane na wenzao wa CCM katika kuwashughulikia wabunge wa CHADEMA kuhakikisha hawapati nafasi ya kuongoza kamati za Bunge pindi watakapowasilisha majina yao.

Sababu nyingine inadaiwa ni kutaka kuwakata makali CHADEMA ambao wabunge wake wawili Dk. Willbrod Slaa na Zitto Kabwe katika Bunge lililopita waliokuwa ni miongoni mwa viongozi wa kamati na inadaiwa kushika kwao nafasi hizo kulisaidia kuongeza umaarufu wao na wa chama.

“Wakati wakiwa viongozi wa kamati katika Bunge lililopita watu kama kina Dk. Slaa hawakuacha kutaja mabaya waliyoshuhudia katika kutekeleza majukumu yao.

“Mara ya kwanza wakati walipopewa uongozi walifikiri kuwa wasingefurukuta tena, wangekuwa bize na majukumu ya kamati na kutatua mambo yanayoisibu lakini hali ilikuwa ni tofauti walitumia yale mabaya waliyoshuhudia yakifanywa na watendaji wa serikali kuwaeleza wananchi,” kilieleza chanzo chetu.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Tanzania Daima imebaini kuwa mkakati huu wa sasa umeanza kufanywa chini kwa chini mara baada ya kuapishwa wabunge na kuundwa kwa kambi ya upinzani ambayo kwa sasa inaongozwa na Freeman Mbowe wa CHADEMA.

Chanzo chetu kililidokeza gazeti hili kuwa wanaoshinikiza mkakati huo ni baadhi ya wabunge ambao wana uchu wa kimaslahi na madaraka.

Hivi sasa wabunge wako katika utaratibu wa kuorodhesha maombi ya kamati wanazozitaka.

Baada ya hatua hiyo, hatua inayofuata ni kupanga kamati na hili litafanyika wiki mbili kabla ya Bunge kuanza Februari 8 mwakani ambapo Spika Anne Makinda ataweka majina ya kamati mbalimbali kulingana na elimu na uzoefu na mwisho wa siku hizo kamati zitachagua wenyeviti.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hili, Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah hakuwa na nafasi kwani alipotafutwa kwa njia ya simu alimtaka mwandishi wa habari afike ofisini kwake.

Lakini mwandishi alipofika ofisini kwake jana alielezwa na katibu muhtasi wake kuwa alikuwa ametoka kidogo kwa dharura za kiofisi.
 
Chuki zote hizi ni uroho wa madaraka wa CUF-Pemba(CCM B)
 
You don't need a genius brain to work out what is up in CUF-CCM minds! Shame on CUF, the pace has already been set.
 
They are now dancing to CDM's tune! Aibu kweli kweli
Wataendelea hivyo hadi lini maana CDM kwa sasa ni kama gari moshi, likishika kasi halifungi break ovyo hovyo. Kitu pekee wasichojua ni kuwa hawana uwezo wa kuziba uwezo wa wabunge makini iwe ndani ya kamati au nje. CDM haitoingia kwenye mitego iliyowanasa CUF na NCCR maana inaishi kwa nguvu ya umma!
 
Utawatambua kwa matendoooooo... utawatambuaaaaa!!

Wabunge wa CHADEMA walichaguliwa kuwatumikia wananchi wala si kugombania vyeo! Wale waliokubali kuolewa pamoja na uanaume wao na kugeuzwa kuwa mazezeta baada ya kupewa vyeo huko Zanzibar, hawawezi kuwa saizi yenu. Waache waendelee na chochote wanacho taka na malipo yao ni kupigwa bakora na CCM tu. Acha wakimbilie vyeo na kupindisha kanuni za bunge,Watanzania tunawaona na tutawahukumu kwa matendo yao!!
CHADEMA msije mkatoka nje ya mstari mkajiingiza kwenye vita vya kugombania vyeo kama wao!! Endeleeni kupigania kilicho wapeleka bungeni whether mtakuwa mnaongoza hizo kamati au la!!!
 
Back
Top Bottom