CUF: CCM isitumie rasilimali za nchi kuendeshea shughuli binafsi za kisiasa za chama

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,353
TAARIFA KWA UMMA

Imetolewa leo Tarehe 11/12/2016

Na, Kurugenzi ya Habari CUF-Taifa

CCM ISITUMIE RASILIMALI ZA NCHI KUENDESHEA SHUGHULI BINAFSI ZA KISIASA ZA CHAMA
TAREHE 5/12/2016 NDUGU Suleiman Y. Mwenda kwa niaba ya msemaji wa CCM alitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya kufanyika kwa vikao vya kitaifa vya Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni Kamati Kuu (CC) tarehe 12/12/2016 na Halmashauri Kuu (NEC) tarehe 13/12/2016, vikao hivyo imeripotiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam. Kwanza tunapongeza kwa CCM kufanya vikao vyake vya kikatiba jambo ambalo ndio afya ya Chama na Demokrasia kwa kuwa CCM ndio Chama kinachoongoza Serikali. Ni wajibu wa wanaCCM kutathmini mwelekeo wa hali ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa maslahi mapana ya Taifa na watu wake na kuisimamia na kuishauri Serikali namna bora ya uendeshaji wa nchi hasa katika kipindi hiki ambacho wananchi walio wengi wanalalamikia uwepo wa ugumu wa maisha ikilinganishwa na uongozi wa awamu iliyopita. Uchumi wa nchi haujayumba bali UMEYUMBISHWA na Style ya uongozi wa nchi usiozingatia ulinzi wa misingi ya KIUCHUMI. (Principles of Economic protection) Na kusababisha UCHUMI WA NCHI KUNYAUKA. Lakini pia uendeshaji wa nchi kwa kuzingatia misingi ya Haki, Usawa, Demokrasia na Utawala wa Sheria na kufuatwa kwa Katiba ya nchi. Pamoja na mambo mengine Uzingatiaji wa MISINGI YA HAKI ZA BINAADAMU BADO IMEKUWA NI TATIZO KUBWA KATIKA NCHI YETU.

Tanzania ni nchi kubwa yenye idadi ya watu takribani milioni hamsini (50) lazima kuwepo na mgawanyo wa madaraka na usimamizi wa mambo badala ya kuonekana kila jambo lazima lisimamiwe na mtu mmoja na au kwa maagizo kutoka Ikulu. Hata hivyo, Vikao hivyo vyenye wajumbe wanaokadiriwa kufikia kati ya 360-400 vinapaswa kufanyika kwa kutumia rasilimali za Chama chenye kupokea ruzuku ya serikali ambayo si chini ya shilingi milioni 800 kwa mwezi kuweza kuendesha shughuli zake.

KUNA TAARIFA KUWA VIKAO HIVYO VIMEPANGWA KUFANYIKIA IKULU YA NCHI, DAR ES SALAAM JAMBO AMBALO KAMA NI KWELI HIVYO NDIO NDIVYO ITAKUWA NI MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI ZA NCHI KWA MASLAHI YA CCM BINAFSI. Hili halikubaliki. Ikulu ni ya watanzania wote. Na watendaji wa Ikulu ni wa Serikali siyo wa Chama cha Mapinduzi. Ni vyema Katibu Mkuu wa Chama akashauriana na Mwenyekiti wake kufanya utaratibu wa kukodisha Ukumbi katika sehemu nyingine nje ya Ikulu, kwani tunaamini kuwa Ukumbi wa Ikulu haukodishwi kwa matumizi binafsi nje ya shughuli za kiserikali. Ni vyema wakatafuta njia mbadala ya kukusanya fedha za kulipia madeni mbalimbali wanayodaiwa.

Ni matarajio yetu kuwa CCM itazingatia ushauri huu na kutenganisha baina ya shughuli za Chama na za Serikali ili kulinda itifaki, maadili, nidhamu na heshima ya Chama Chao na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa maslahi binafsi ya kichama.

HAKI SAWA KWA WOTE

___________________________
MBARALA MAHARAGANDE

K/NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA

MAWASILIANO: 0784 001 408/ 0715 062 577
 
Propesa nafsi ishamsuta tena huyu na nae haeleweki kama sigara kali inawaka kotekote
 
Hivi huyu MAHARAGANDE ni CUF-Lipumba au CUF-Asili? Naona kaanza na pongezi kwa chama "pinzani" kufanya vikao vyake. Imeharibu maana nzima ya habari yenyewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom