Jatropha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2009
- 1,151
- 199
jana wakat wabumge wa chadema wanatumia haki yao ya kikatiba kumsusia rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambaye wanaamini kuwa hakupatikana katika uchaguzi huru na wa haki, wabunge wa vyama vingine hususan cuf n.k vyenye viti 8 tu tanzania bara kwa pamoja (cuf 2, nccr , tlp 1 na udp 1) walionekana haraka haraka wakikimbilia kujaza viti vya wabunge wa chadema ili kuepusha aibu hiyo.
Nafurahi kitendo hiki kimetokea wakati ambapo mjadala uundwaji wa kambi ya upinzani ukiwa bado mbichi kabisa; ambapo waliokuwa wakitetea kushirikishwa kwa vyama vingine katika kambi hiyo natumai wamejionea wenyewe namna ambavyo wawakilishi hao wanavyoshiriki kuunga mkono kuendelea kuwepo katiba ya sasa katika mfumo na maudhui yake pamoja na tume ya uchaguzi isiyokuwa huru.
Kilichonifurahisha zaidi ni kitendo hicho kuweka mpaka vichwani na mawazoni mwa wananchi kuwa ni chama gani kipo kwa maslahi mapana zaidi ya taifa na watanzania na vyama gani vipo kwa ajili ya kutumiwa na ccm kujinda katiba na tume huru isiyokuwa huru; na kwa maana hiyo ufukara na umaskini na kukua kwa matabaka miongoni mwa watanzania.
Kwa kumsusia rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania aliye zao la katiba na tume ya uchaguzi mbovu, chadema imeungana na 51.2% ya watanzania waliojiandikisha kupiga kura lakini wakasusa kujitokeza kupinga mambo mbali mbali ikiwemo katiba na tume mbovu. Ukichanganya na 26% aliyopata dr slaa baada ya kuchakachuliwa utagundua kuwa wabunge wa chadema walikuwa wanawawakilisha takribani 77% ya watanzania waliojiandikisha kupiga kura ikilinganishwa na ccm na mhe jakaya kikwete amabye alikuwa akiwawakilisha 27% tu ya waliojiandikisha kupiga kura.
Big up chadema!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!