CUF, acheni kupotosha watu kuhusu matokeo ya Uchaguzi Wilaya ya Igunga 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF, acheni kupotosha watu kuhusu matokeo ya Uchaguzi Wilaya ya Igunga 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Aug 2, 2011.

1. Mag3

Mag3 JF-Expert Member

#1
Aug 2, 2011
Joined: May 31, 2008
Messages: 9,094
Likes Received: 6,188
Trophy Points: 280
Wapenzi wa CUF, acheni kudanganya watu kwani mwaka jana Chadema hawakuweka mgombea Ubunge katika Wilaya ya Igunga. Waliogombea Ubunge Igunga walikuwa wawili tu - ROSTAM AZIZI ABDULRASOOL wa CCM aliyepata kura 35,674 na LEOPOLD LUCAS MAHONA wa CUF aliyepata kura 11,321.

Na katika kinyang'anyiro cha Uraisi Wilayani Igunga, pamoja na uchakachuaji uliofanyika Kikwete wa CCM alishinda kwa kura 34,090 akifuatiwa na Dr. Slaa wa Chadema kura 8,874 na Prof. Lipumba akawa wa tatu kwa kura 3,181. Ukitafakari kidogo utagundua mgombea Ubunge wa CUF anamzidi mgombea Uraisi wa CUF kwa kura zaidi ya 8,000 (see ?)

Hata hivyo Chadema waliweka wagombea Udiwani kwenye kata mbali mbali Wilayani Igunga na waliweza kushinda maeneo fulani tofauti na CUF iliyoambulia sifuri. Swali - huo umaarufu wa CUF Igunga unatoka wapi ?

2. Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji Platinum Member

#2
Aug 3, 2011
Joined: Mar 10, 2006
Messages: 31,362
Likes Received: 6,393
Trophy Points: 280
Mag3, hiyo ni mbinu ya kawaida tu vitani kukatisha watu tamaa; itasikitisha kama CHADEMA watakata tamaa. Pamoja na hilo, wananchi wa Igunga watahitaji kuona kuwa mgombea atakayesimamishwa na chama chochote ni kweli anawakilisha maslahi yao. Binafsi nitaangalia sana ni nani anaonekana kuwa mrithi Rostam. Sijui kama Kafumu atakuwa tayari kwenda kujaribu jimbo ambalo kwa muda mrefu aliamini ulikuwa ni urithi wake halali.

3. RedDevil

RedDevil JF-Expert Member

#3
Aug 3, 2011
Joined: Apr 30, 2009
Messages: 2,287
Likes Received: 903
Trophy Points: 280
Pamoja na yote, tangu lini kukawa na ushirikiano kati ya vyama vya siasa tanzania! Hapa utagundua kuwa kuna janja fulani inataka kutumika ili chama kimoja kipandie kupitia mgongo wa mwingine! hivyo si shauri wala siwasemei watu hapa, " In politics, you must play smarter than your enermy".

CDM wakiweka mgombea, kuna faida nyingi zaidi ya kushinda hilo jimbo, hivyo waweke mgombea tena mgombea sahihi.

4. Arafat

Arafat JF-Expert Member

#4
Aug 3, 2011
Joined: Nov 17, 2009
Messages: 2,582
Likes Received: 41
Trophy Points: 0
Sina huhakika kama wapiga kura Igunga wanafika 35,000! haya ndio mambo yanayomsumbuwa Kikwete juu ya hawa anaotaka kuwafukuza mara nyingi CCM wamekuwa na wizi wa kura hasa vijijini kwa kuongeza idadi ya wapiga kura hata mara dufu ya idadi ya halali, sasa hao walio kuwa wanasuka mbinu za kuiba kura zake ndio leo anaambiwa awafukuze ataweza wapi?

Hii ina maana kama Igunga walikuwa na wapiga kura 20,000 basi katika huo uchaguzi Dr. Slaa alipata kura 8,874 kikwete kura 7,945 na Lipumba kura 3,181 na margin yake ushindi ni kura za wizi ambazo zinaongezwa juu ambayo kwa kesi hii tofauti ya 20,000 na 35,000 ambayo ni kura 15,000.

Cha ajabu ni kuwa wizi huu sehemu nyingine za Tanzania umekuwa ukihusisha hadi wabunge wa Chadema na Madiwani wao sasa sijui 2015 Chadema wamejipanga vipi juu ya wizi wa namna hii na pia wananchni wenyewe pia tunajipanga vipi juu ya wizi wa aina hii kila kona ya Tanzania, maana pale ambapo hakuta kuwepo wagombewa na CDM au kuwepo wagombewa ambao ni weak au wa CCM lakini wanagombea kwa ticket ya CDM lazima wataendelea na Mtindo huu.

5. Nyambala

Nyambala JF-Expert Member

#5
Aug 3, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 4,470
Likes Received: 21
Trophy Points: 135
Numbers don't lie, itashangaza pale ambapo wapiga kura wanaweza kuwa chini ya hiyo idadi ya kura alizopata JK. Just wait and see, na ukitaka kujua hawa jamaa hawana umakini pamoja na kuwategulia kitendawili hiki mapema the may easily fall into this trap!!

6. Mag3

Mag3 JF-Expert Member

#6
Aug 3, 2011
Joined: May 31, 2008
Messages: 9,094
Likes Received: 6,188
Trophy Points: 280
Kuna watu wanataka kutuaminisha kuwa Upinzani ukitaka kushinda huko Igunga inabidi waunganishe nguvu nyuma ya Prof. Lipumba wa CUF kwa sababu kwanza ni kwao na pili CUF wana nguvu sana huko kuliko Chadema. Wanadai kuwa hata kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge mwaka 2010 CUF ndiyo ilichukua nafasi ya pili ! Sasa hapo ndo napata taabu, hivi CUF walitakiwa kuchukua nafasi gani kama 1) wagombea walikuwa wawili tu na 2) CUF haikushinda !

7. Nyambala

Nyambala JF-Expert Member

#7
Aug 3, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 4,470
Likes Received: 21
Trophy Points: 135
Nimetafuta data kutoka tume ya uchaguzi za mkoa mzima wa Tabora, pamoja na hiyo mbinu ya kutaka tuamini CUF ni maarufu huko Tabora kuliko chama chochote cha upinzani lakini ukweli uko hivi kutokana na matokeo ya mwaka jana:

Dr. Slaa - 38, 341

Lipumba - 34,374

Tofauti anayozidiwa nayo Lipumba ni 3,977 karibu kura 4000 sasa sijui huo umaarufu na ukwao wa Lipumba unaelezekaje hapa. Kwa kifupi kama alivyosema Mag3, mashabiki wa CUF wanawaongopea watanzania.

8. Laurence

Laurence JF-Expert Member

#8
Aug 3, 2011
Joined: Jun 11, 2011
Messages: 3,106
Likes Received: 37
Trophy Points: 145
Hayo ni mawazo ya watu wachache kutaka kupandikiza mbegu kwa wengine ati kwamba ni bora wakasimama CUF na hao Magamba,hii si kweli kabisa CDM wasimamishe mtu makini ni dhahiri mawazo ya watz wamebadilika na mtizamo wao wengi nikwa CDM so swala la msingi ni maandalizi ya nguvu na kutizama mahitaji ya wana Igunga ni nn haswa then hapo ndipo pa kuanzia,lakn kutuaminisha tuwaachie hawa mume na mke i.e CCM na CUF itamaanisha hakuna upinzani tena maana hawa wamejitanabaisha kua si wapinzani tena na wana Igunga waelezwe hili na thari zake

9. m

mzee wa mawe Senior Member

#9
Aug 3, 2011
Joined: Aug 2, 2011
Messages: 151
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
jamani tuongee ukweli chadema kama chama hakipo igunga kwa kuwa hata heche ameliona hakuna viongozi hata kata moja kwa kuwa mmeishazoea kununua viongozi wa upinzani mfano Lwakatare hiyo ndio siasa zenu kama ccm

10. Mshume Kiyate

Mshume Kiyate JF-Expert Member

#10
Aug 3, 2011
Joined: Feb 27, 2011
Messages: 6,774
Likes Received: 22
Trophy Points: 135

11. Mag3

Mag3 JF-Expert Member

#11
Aug 3, 2011
Joined: May 31, 2008
Messages: 9,094
Likes Received: 6,188
Trophy Points: 280
Nakuomba uwe unasoma kwa makini post za watu - Mag3 alitoa za Wilaya ya Igunga na Nyambala katoa za Mkoa wa Tabora.

12. m

mtanzania1989 JF-Expert Member

#12
Aug 3, 2011
Joined: May 20, 2010
Messages: 2,142
Likes Received: 1,711
Trophy Points: 280
ebu tuwekeni sawa takwimu zipi ni sahihi[/QUOTE]

hizi ni za mkoa wa tabora
Dr. Slaa - 38, 341
Lipumba - 34,374

na hizi ni za jimbo la Igunga
Dr. Slaa - 8,874
Lipumba -3,181

13. Shinto

Shinto JF-Expert Member

#13
Aug 3, 2011
Joined: Dec 6, 2010
Messages: 1,781
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
Hili ndio tatizo la CDM, wanalewa umaarufu....
Kwa tafsiri yao, ushirikiano lazima uwe kwa manufaa ya chadema tu, na mtu akitaka kugombea lazima agombee kwa ticket ya Chadema ili kuongeza ruzuku!
Mbona Kigoma NCCR ilipata wabunge wengi lakini kwenye majimbo walioshionda Slaa alipata kura nyingi za Urais kuliko Rungwe? Kwa hiyo mtasema NCCR sio maarufu kwenye majimbo hayo?

Na hii ndio imekuwa kikwazo cha ushirikiano baina ya vyama vya upinzani........CHADEMA NI WALAFI NA WAROHO wa madaraka!

14. by default

by default JF-Expert Member

#14
Aug 3, 2011
Joined: Jul 11, 2011
Messages: 843
Likes Received: 4
Trophy Points: 0

hizi ni za mkoa wa tabora

Dr. Slaa - 38, 341

Lipumba - 34,374

na hizi ni za jimbo la Igunga

Dr. Slaa - 8,874

Lipumba -3,181[/QUOTE]

acha kuwa na akili nzito kama tope la mfinyanzi sasa hapo ujaelewa nini! Wakati kitu ipo wazi kabisa haya sasa soma kwa umakini tena hapo kuna matokeo ya igunga upande wa wagombea urais kati ya dr na prof na mkoa mzima wa tabora kwa jumla kuu imewekwa kuonyesha ao wanaosema cuf inakublika kulko chadma waone takwmu za wagombea urais mwaka jana

15. Mshume Kiyate

Mshume Kiyate JF-Expert Member

#15
Aug 3, 2011
Joined: Feb 27, 2011
Messages: 6,774
Likes Received: 22
Trophy Points: 135
Tunashukuru kwa takwimu

16. Felixonfellix

Felixonfellix JF-Expert Member

#16
Aug 3, 2011
Joined: Feb 16, 2010
Messages: 1,680
Likes Received: 4
Trophy Points: 135
Ukweli utakuwa wazi baada ya miezi 3 kama taratibu zitazingatiwa na sheria zikafuatwa.
Bora vyama vyote visimamishe wagombea na apatikane mshindi wa ukweli
Ku-rely kwenye takwimu zilizopita wakati mwingine si sahihi, kama ni sawa basi hakuna sababu ya wapinzani kusimamaisha mgombea maana jimbo litakuwa mikononi mwa CCM automatically kwa mujibu wa law of proportionality. Kama kweli CUF ngome yao kubwa ni Tabora, basi wangeshika hata jimbo moja tu. Kwa kuwa CHADEMA hawakusimamisha mgombea last year, wanatakiwa kujiuliza ilikuwaje wasifanye hivyo??? Na je kwa nini this phase wasimamishe? Kuna haja ya kufanya tathmini kabla ya kuamua kufanya jambo lolote na kufanya maamuzi.

17. Duble Chris

Duble Chris JF-Expert Member

#17
Aug 3, 2011
Joined: May 28, 2011
Messages: 3,487
Likes Received: 7
Trophy Points: 135
wananunuaje mtu ?? elewa kuwa kama mtu anapenda kuwa mpinzani ktk nchi hii basi CDM ni chama cha upinzani

18. Nyambala

Nyambala JF-Expert Member

#18
Aug 3, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 4,470
Likes Received: 21
Trophy Points: 135
Tatizo ni kwamba huwezi kupindisha facts just for hating something....... Kama una kumbukumbbu nzuri Busanda ilikuwa almost same story na hii ya Igunga. 2005 mgombea wa CUF alikuwa wa pili tena kwa kura nyingi tu, uchaguzi mdogo baada ya mbunge kufariki CDM nusura ilichukue jimbo. Mark my words this is what is going to happen!!!

Uchaguzi jimbo la busanda 2005 general elections:

Faustin Rwilomba Kabuzi, CCM - 61,868 = 72.7%

Hussein Musa Abdallah, CUF - 13,094 = 15.3%

Manyanya Chalahani Ismail, CHADEMA - 3107 = 3.65%

FOUR YEARS LATER

Uchaguzi mdogo jimbo la busanda, May 2009.

Lolensia Bukwimba, CCM - 29,242 = 54%

Oswald Ndalawa, CUF - 977 = 1.03%

Faustin Magesa, CHADEMA - 22,799 = 44%

Priory of Zion upo???????????

19. Mwita Maranya

Mwita Maranya JF-Expert Member

#19
Aug 3, 2011
Joined: Jul 1, 2008
Messages: 10,569
Likes Received: 105
Trophy Points: 145
Katika hili ni bora kuitwa walafi na waroho kuliko kushirikiana na cuf.

Kitendo cha chadema kushirikiana na cuf ni sawa na kujichoma kisu wenyewe.

Ni juzi tu mbunge wa cuf ame declare bungeni kwamba wao hawana ushirikiano na chadema, sasa watu kama hao utawaaminije hadi ushirikiane nao?
Katika hali kama hii na mazingira kama haya ni muhimu na lazima chadema wawe "walafi na waroho" kwa maslahi ya demokrasia, chama na wananchi wa igunga.

20. Mwita Maranya

Mwita Maranya JF-Expert Member

#20
Aug 3, 2011
Joined: Jul 1, 2008
Messages: 10,569
Likes Received: 105
Trophy Points: 145
wao walizoea kununua na bado wanaendelea kununua, kwahiyo si ajabu wakadhani na wenzao wanafanya hivyo.

Tofauti ni kwamba chadema ni chama cha kweli cha upinzani na kinajiuza chenyewe, watu kutoka vyama mbali mbali wamekuwa wakimiminika chadema.

Mimi ninawafahamu viongozi kadhaa wa ccm, udp na cuf ambao wamchukua kadi za chadema mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 na hakuna mtu yeyote aliyenunuliwa, wameamua wenyewe kwa hiari yao "kuhamia chadema".

Loading...