CUF 100% KUNG'OA VIGOGO wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF 100% KUNG'OA VIGOGO wa CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwiba, Oct 27, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  [FONT=&quot]CUF kung’oa vigogo CCM[/FONT]​
  [FONT=&quot] CUF kimeanza kujigamba wazi wazi kwa kutoa tathmini inayoitwa ya kisayansi kuonyesha kwamba, kina uhakika wa kutwaa bila jasho jingi majimbo 47 ya ubunge Tanzania Bara matokeo ambayo kinasema ni tofauti na ya Visiwani ambako kinatarajia kuzoa viti vingi vya ubunge na uwakilishi.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]​
  [FONT=&quot]Mengi ya majimbo yanayotajwa ni ya Mikoa ya Lindi na Mtwara ambako duru za CUF zinasema mawaziri wawili wa Serikali inayomaliza muda wake wanaweza kuangushwa na wagombea wa chama hicho.[/FONT]​
  [FONT=&quot]Mawaziri wanaotajwa kuwa hatarini ni wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara. Mkuchika ni mbunge anayemaliza muda wake na ambaye anawania tena nafasi hiyo kwenye Jimbo la Newala, mkoani Lindi.
  Mwingine anayewekwa njia panda na CUF ni Hawa Ghasia, ambaye ni mbunge anayemaliza muda wake katika Jimbo la Mtwara Vijijini.
  [/FONT]​
  [FONT=&quot]Meneja wa Kampeni wa CUF, Mohamed Miraji akitoa tathimini ya chama hicho katika mahojiano ya simu kutokea Shinyanga, Jimbo la Solwa, Jumatatu wiki hii, alisema tathmini ya chama chake tangu kuanza kwa kampeni hadi sasa kuelekea ukingoni inabainisha kuwa watachukua, bila jasho, majimbo 47 Bara mbali na ya Zanzibar.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]​
  [FONT=&quot]Kwa mujibu Miraj majimbo hayo wameyapanga katika kundi la A na kwamba yenye utata kidogo yamewekwa kundi B+ kwa maana kwamba huko watashinda si kwa idadi kubwa ya kura. Mbali na alama hizo za A na B+, Miraji alisema majimbo mengine 20 wameyawakea alama B.[/FONT]​
  [FONT=&quot]Akifafanua alama hiyo B ambayo ni tofauti na B+, kiongozi huyo alibainisha kuwa maana ya alama hiyo ni kwamba ushindi kwa kiasi kikubwa utategemea namna CUF na wagombea husika kwenye majimbo hayo watakavyocheza karata zao dakika za mwisho.[/FONT]​
  [FONT=&quot]“Alama A maana yake tuna uhakika wa ushindi kwa asilimia 90, B+ tuna ushindi ambao si wa wingi mkubwa wa kura na B tunaweza kushinda kwa kutegemea tutakavyocheza karata zetu, tukicheza vibaya tunaweza kushindwa,” alisema kiongozi huyo anayeongozana na mgombea urais wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]​
  [FONT=&quot]Aliyataja majimbo ambayo tathmini yao imeyapa alama A kuwa ni Mchinga lililokuwa likiongozwa na Mudhihir Mohamed Mudhihir na Newala la Mkuchika.[/FONT]​
  [FONT=&quot]Mengine ni Handeni linaloongozwa na aliyepata kuwa askari wa mwavuli Awamu ya Tatu, Dk. Abdallah Kigoda na Mtwara Vijijini linaloongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ghasia.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]​
  [FONT=&quot]Kwingine ni Tunduru Kusini ambalo limegawanywa kutoka lililokuwa Jimbo la Tunduru chini ya Mbunge wa CCM anayemaliza muda wake, Mtutura Abdallah Mtutura, jingine ni Tanga Mjini lililokuwa chini ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Raia, Harith Bakari Mwapachu na Lindi Mjini la Mohammed Abdulaziz.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]​
  [FONT=&quot] Mengine ni Geita lilillokuwa chini ya Ernest Mabina, Liwale chini ya Hassan Chande Kigwalilo, Masasi ambalo kwa vyovyote litatoa mbunge mpya baada ya aliyemaliza muda wake, Raynald Mrope kuangushwa kwenye kura za maoni.[/FONT]​
  [FONT=&quot] Kwingine ni Kondoa Kaskazini lililokuwa chini ya Zabein Mhita, Nanyumbu kwa Danstan Mkapa, Kilwa Kaskazini kwa Dk. Samson Mpanda, Rufiji lililokuwa likiongozwa na Profesa Idris Mtulya.
  [/FONT]
  [FONT=&quot] CUF pia imejinasibu kutwaa Jimbo la Tarime lililokuwa likiongozwa na Charles Mwera wa Chadema, ambaye kwa sasa ndiye mgombea wa CUF.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]​
  [FONT=&quot] Jimbo la Sumve chini ya mbunge anayemaliza muda wake, Richard Ndassa nalo limetajwa na CUF kuwa sehemu salama kwa ushindi, kama ilivyo kwa Jimbo la Solwa lililokuwa likiongozwa na mbunge anayemaliza muda wake, Ahmed Ally Salum.[/FONT]​
  [FONT=&quot]Mtwara Mjini chini ya mbunge anayemaliza muda wake, Mohamed Said Sinani nalo limetajwa kuangukia mikononi mwa CUF. [/FONT]​
  [FONT=&quot]Alisema kampeni za mwaka huu CUF imejidhihirisha kukubalika zaidi vijijini kuliko mjini na kwamba hali hiyo inatokana na ukweli kuwa awali vyama vya Upinzani havikuwekeza maeneo hayo.[/FONT]​
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama mkichunguza mtaona Chadema hapa JF wamepwaya sana ,ila utawaona wale waliosikia kuwa Tz kuna uchaguzi na viposti vyao wakipiga makelele bila ya kujua walitendalo.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nifahamishe -- wewe unashabikia CCM au CUF? Au udini unakusumbua sana maana hueleweki kabisa. Ni kama vile MS.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mimi sio kama vile wewe MS ,Kwa wakati huu nipo kama mkombozi wa wanyonge na ninawaelekeza na kuwafahamisha wengi sana na sio hapa tu hata vijijini nimewaamsha wengi sana na mwisho huwambia kura ni siri ya mtu na uelewa wake ,ila usipeleke kura yako kwa CCM,na huzidi kuwafahamisha kuwa hata kama kura yako hukuipeleka CCM bado CCM wataibuka washindi na hapo huwapa maelezo mafupi tu nao hunielewa na kusema sawa mzee. Ila nashangaa hapa kwenye wasomi kushindwa kuielewa CCM na kushindwa kuelewa kuwa CCM hawataiwachia nchi upinzani kupitia kisanduku cha kura ,hilo halipo kwenye mipango yao ,huu uchaguzi ni kama mazingahombwe , tutashinda ubunge nikimaanisa upinzani lakini kwenye uraisi hapo ni mbinde na tutashindwa kwa margin kubwa sana tusioitegemea ,hao ndio CCM.
   
 5. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umesahau majimbo ya kigamboni, ubungo na kinondoni haya yote ni ya cuf. Inavyooneka mwandishi unataka kukatisha watu tamaa eti ionekane kua upinzani hauna lao jambo mjini lkn si kweli. Bongo jino kwa jino.
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wee mwiba wewe,
  Ukweli ni kwamba hayo majimbo ni ya ndugu zenu sisi m. Msitegemee lolote pale. Labda kama kuna muafaka wa bara kati yenu.
   
 7. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umesahau majimbo ya kigamboni, ubungo na kinondoni haya yote ni ya cuf. Inavyooneka mwandishi unataka kukatisha watu tamaa eti ionekane kua upinzani hauna lao jambo mjini lkn si kweli. Bongo jino kwa jino.
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hayo nj ya miji mikubwa sana ndio pakasemwa kuna kuvutiana wapiga kura.
  Tetesi na simulizi za watu wengi inaonekana kura atapewa au watampa Lipumba maana hao wengine wameonekana kuporomoka katika kuwashawishi wananchi kwa maneno yenye kujenga matumaini.
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli kweli i am just watching anyways 31 Oct will tell
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kumbe wewe ni CUF tupo pamoja bwana! tumtose CCM kabisaaa hatakiwi awepo! nilimsikia LIPUMBA akishuka sera zake ATN si mchezo, but alichelewa kuimalisha chama (kuuunganisha) for Now DR!
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
Loading...