CTI Kutumika kukodisha Majenereta ya DOWANS: Fikra Pevu

Una hakika na hilo lekundu? Umeshamsikiliza Dr Slaa vizuri ndugu?

Wanaongea in general shida za nchi, lakini hata siku moja hawajasema jinsi hao watu walivyo hovyo. At least mimi sijawahi kusikia wakizungumza hilo. Kesho kutwa 2015 Mwandosya atagombea Urais (or at least atajaribu). Ishu sio shida za nchi, maana hata ccm watasema tunapambana nazo, ishu ni yeye anaweza. Na katika hilo lazima muweke track record yake wazi. Sasa kweli katika kampeni zote 2005/10 hakuna mtu aliyeonyesha jinsi kikwete alivyo nanga na kupewa wizara nyeti bila kuweza kazi? Kutoa facts kama hizi kungebadilisha minds za wangapi?
 
Mh. Zitto

Samahani sana Punguza jazba kiongozi jaribu kupokea changamoto na uzipatie majawabu sio kutoa matusi kama mtu wa kijiweni

Mimi ni supporter mkubwa wa cdm tokea ulipoanza alakati zako, lakini mpaka sasa sikuamini tena maana umekuwa ndumilakuwili mara huku mara huku.

About NEXT GENERATION
Mh Zitto sijui kama haya maneno yametoka mdomoni mwako, did you real feel TAnzania Generation? kwanini ZITTO wa sasa sio ZITTO wa ZAMANI? KIPI KIMEKUBADILISHA?

Connection with RA and LW

Mbona hukijitokeza kupinga haya, naweza kusema niliamini makala ya hili gazeti kwa 40% lakini matendo yako ndo yananipa muelekeo wako mpaka sasa





Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 15 December 2010

zitto_219.jpg



ZITTO Kabwe, naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amekuwa na mawasiliano ya karibu na na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, imefahamika.
Kufichuka kwa taarifa za mawasiliano kati ya Zitto na Rostam kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha mawasiliano kati ya Zitto na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini (TISS), Jack Zoka.
Aidha, kufichuka kwa mawasiliano kati ya Zitto na Rostam kumekuja siku mbili baada ya mama mzazi wa Zitto, Shida Salum kunukuliwa akisema, “Mwanangu ni mkorofi.”
Mama Zitto alikieleza kikao cha Kamati Kuu (CC) ya chama chake kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, “Namfahamu mwanangu. Ni mkorofi. Si msikivu.”
Kwa mujibu wa rekodi ya mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini, TISS na Rostam, watu hao wawili wamekuwa wakijadiliana mambo kadhaa.
Miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa na viongozi hao, yanahusu CHADEMA, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na taifa kwa ujumla.
Rostam ambaye CHADEMA imekuwa ikimtuhumu kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi, ni mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM.
Gazeti hili limeshindwa kujua mapenzi ya Rostam kwa CHADEMA hadi kujipa jukumu la kujadiliana na Zitto juu ya “uhai bora” wa chama hicho.
Kwa mfano, Zitto na Rostam walifanya mawasiliano ya simu mara tano hapo tarehe 11 Agosti 2010. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754555555 ambayo hutumiwa na Rostam.
Mawasiliano hayo yalifanyika saa 07:08:35, saa 22:09:02, saa 22: 28: 39, saa 22:49:54, saa 22:44:37 na saa 22:45:09.
Wakati mawasiliano hayo yanafanyika simu ya Zitto ilikuwa inasomeka kuwa yuko Uzunguni, Dodoma, huku simu ya Rostam ikisomeka kuwa ilikuwa Area D, Dodoma.
Mawasiliano mengine yalikuwa katika maeneo tofauti. Mathalani mawasiliano ya Zitto na Rostam yalyofanyika 30 Novemba 2010 yalionyesha kuwa Zitto yuko Ohio, Ilala, Dar es Salaam. Yalifanyika saa 14:58:42, saa :16:41:58, saa 15:38:00, saa 16:09:56 na 17:48: 35.
Mawasiliano mengine ya Zitto na Rostam yalifanyika siku mbili kabla ya wabunge wa CHADEMA hawajakutana Bagamoyo.
Mawasiliano hayo yalifanyika tarehe 7 Desemba 2010 saa 07: 57:27, saa 14:32:08, saa 09:44:36 na saa 14:07:07.
Haijaweza kufahamika pia kiini cha mawasiliano kati ya Zitto, Zoka, Rostam na vigogo wengine wa serikali, CCM na usalama wa taifa.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu kutoka ndani ya kikao cha CHADEMA, awali mama Zitto alieleza masikitiko yake kuhusiana na taarifa mbalimbali zinazomhusu mwanawe.
“Najua mwanangu ni mkorofi. Lakini kuna njia ya kufanya kuliko kukitia chama msukosuko…Kila mara Zitto, Zitto, Zitto. Haya mambo hayana faida kwa chama,” alieleza.
Hata hivyo, vyanzo huru vya taarifa vimeeleza MwanaHALISI kuwa mpango uliopo ni kumtumia Zitto “kusambaratisha CHADEMA.”
“Kaka, nakuhakikishia kuwa upo ushahidi wa kutosha kwamba Zitto anatumika kuvuruga CHADEMA. Kuna baadhi ya vigogo ndani ya CCM na serikali, wanaomtia ujinga kwa kumueleza, ‘kwa hali ilivyo ndani ya CCM, wapo baadhi ya watu wanatamani kuondoka. Lakini hawawezi kwenda CHADEMA kwa sababu kinaongozwa na Mbowe (Freeman Mbowe),’” ameeleza mtoa taarifa.
Anasema, “Hivyo wanampampu Zitto kugombea uenyekiti. Wanataka Mbowe ang’oke na CHADEMA kisambaratike. Ni kwa sababu, wote wanaomtumia Zitto, wanajua kuwa huyu bwana mdogo hana uwezo wa kuongoza CHADEMA na haaminiki.”
Akiongea kwa kujiamini, mtoa taarifa anasema, “Ni mbinu zilezile zilizotumiwa NCCR- Mageuzi, ambapo baadhi ya vigogo wa idara ya usalama wa taifa walitumia fedha ili kumng’oa Marando (Mabere Marando), katika uongozi wa chama.”
Anasema taarifa kwamba wapo watu wanataka kuondoka ndani ya CCM na kujiunga na CHADEMA ni mkakati unaosukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya vigogo wa serikali kwa kushirikiana na usalama wa taifa.
Inadaiwa ni katika mkakati huo, ndimo linapatikana jina la Rostam ambaye uongozi wa juu wa chama hicho umekuwa ukimtuhumu kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini.
“Unajua ndugu yangu hapa Tanganyika, Rostam angependa sana awe na uwezo wa ku-control vyama vyote vinavyokua, hasa CHADEMA kwa sasa; ingawa uwezo wake wa kupenyeza unakuwa mgumu.
“Mkakati wake ni kumweka mtu wao katika uongozi wa juu wa CHADEMA ili waweze kumuendesha. Mpango huo ukifanikiwa, kina RA (Rostam) wataacha ugomvi na CHADEMA. Kwa sasa mtu wao ni Zitto. Na kuna mambo mengi ya siri ambayo RA amekubaliana na Zitto,” anaeleza mtoa taarifa mmoja ambaye yuko karibu na Rostam na Zitto.
Mjadala juu ya mwenendo wa mashaka wa maisha ya kisiasa ya Zitto, uliibuka baada ya katibu wa wabunge wa CHADEMA, John Mnyika kuwasilisha taarifa ya shughuli za kamati hiyo mbele ya Kamati Kuu.
Kikubwa kilichojadiliwa ni hatua ya Zitto kuongoza kikundi cha baadhi ya wabunge kusaliti maamuzi halali ya kamati ya wabunge wa chama hicho.
Zitto anatuhumiwa na wabunge wenzake kutotii agizo la kutoka nje wakati Rais Jakaya Kikwete anahutubia Bunge, 18 Novemba 2010.
Katika taarifa yake kwa CC, Mnyika alisema katika kushughulikia suala hilo, hakukuwa na lolote la kuviziana kama ambavyo baadhi ya wajumbe wamedai.
“Hakuna kanuni iliyovunjwa, wala hakuna kinachoitwa kuviziana. Wabunge walikuwa na hasira sana juu ya hatua ya Zitto na wenzake kutotii agizo la kamati na kupita katika vyombo vya habari kupotosha ukweli,” alisema Mnyika kwa sauti ya upole.
Akiongea kwa sauti ya kusisitiza, Mnyika alisema, “Mheshimiwa mwenyekiti, kwa kweli, wabunge walitaka hata kuwapiga wabunge walioasi makubaliano yao. Uongozi wa Kambi ukafanya juhudi kulipeleka mbele suala hili, angalau kupunguza munkari wa wabunge,” alieleza.
Ni katika kikao hicho cha wabunge kilichofanyika Bagamoyo, ndipo wabunge walipiga kura ya kutokuwa na imani na Zitto.
Kile kilichoitwa, “kuviziana” kiliibuliwa ndani ya kikao cha CC na Dk. Kitila Mkumbo, ambaye amenukuliwa akisema ameshutushwa na hatua ya wabunge kumhukumu Zitto wakati ni mgonjwa.
Alikuwa ni Benson Kigaila, mjumbe wa CC aliyeeleza viongozi wenzake umuhimu wa kujenga chama imara badala ya kuangalia mtu.
“Mtu aliyekosea, lazima aadhibiwe. Tusiangaliea kama ataanguka, au atanufaika. Kwa muda mrefu, chama hiki kimenufaika kwa makosa ya CCM, ambapo kutokana na makundi yanayokinzana, wameendelea kukumbatia maovu. Ni lazima chama kichukue hatua za kukabiliana na magenge haya,” alieleza.
Mjumbe mwingine wa CC aliyeongea kwa sharti la kutotajwa gazetini, ameliambia gazeti hili, “Yale mambo yalikuja kama taarifa, si vingenevyo. Jukumu sasa, liko kwa Zitto mwenyewe kujipima kama anaweza kuongoza watu ambao hawana imani naye.”
Baada ya kupeleka taarifa hiyo CC, wabunge wameeleza, “…Tunapeleka maamuzi yetu haya kwa Zitto. Anatakiwa kuamua ama kuachia ngazi au kusubiri hatua nyingine zinazofaa kuchukuliwa kwa mtu kama yeye katika kikao chetu kingine.”
Mara baada ya mjadala wa Zitto kwa CC kutoingilia maamuzi ya Kamati ya wabunge wake, ndipo uamuzi wa kuunda kamati ndogo ya “kumpa ushauri” Zitto ilipoundwa.
Kamati hiyo inaongozwa na Profesa Mwesiga Baregu.Wajumbe wake ni Nyangali Shilungushela, SylivesterMasinde na Mama Zitto.
Kazi ya kamati ya Baregu ni kufuatilia nyendo za Zitto, kumshauri jinsi ya kujibadilisha ili hatimaye arejee katika njia iliyonyooka



Usiamini kila unachosoma. This was an article crafted and delivered by Freeman Mbowe. And wote mnajua bifu la Mbowe na Zitto. This article shows how disappointing our politics have become. It tells you a lot about a puppet that is Mwanahalisi na Saeed Kubenea.

Nyie wanaChadema hamjaseto, mnataka Zitto aende huko Ma-Shinyanga kuandamana wakati ni Mwenyekiti wa kamati ya Bunge and his jobs entails FINDING SOLUTIONS for our problems. And that is what he is doing? Kama NSSF sio mwekezaji sahihi, then who else? changia in a constructive way. Dowans was a mwekezaji and u think our treatment of Dowans didn't muddy the waters for other investors?

Mnataka umeme au mnataka politiki?
 
On my agenda - moja mchuchuma na Liganga miradi ianze. Mbili, Ngaka coal fields mradi uanze. Tatu, Kiwira ifufuliwe. Nitahakikisha kwa kupitia kamati yangu tunawezesha NDC na NSSF wanatekeleza miradi hii na kuliondoa taifa kwenye tatizo la umeme katika muda wa kati.

I dont care about the next election. I do about the next generation.

Sibabaiki. I do the right thing and inshaallaah i will succeed for the benefit of my country!

The rest I have nothing to comment but on the next generation case I wish you could by thinking on hyro-power generation like the Stiglers Gourge and wind mills kule Singida na Pare mountains other than these plans you have on fossils energy which highly contribute kwenye global warming!
 
Kwani CTI hii nayoijua si imesajiliwa kama shirikisho na sio kampuni sasa wana nguvu kisheria ya kufanya biashara zaidi ya ile iliyoainishwa kwenye Memo of Association yao,au na kuzalisha umeme ipo humo? Naomba nipate ufafanuzi tafadhari!

"Artcles of Association" sio msahafu ambao hauwezi kubadilishwa au kurekebishwa wakati wowote ule. Ikiwa katiba zinabadilishwa, zinafutwa, zinatengenezwa mpya itakuwa ka "articles of association". Hoja dhaifu.
 
Sasa wanataka kubadilisha sheria na kununua mitambo hiyo nayo sawa.. kuna ulazima wa kufunga watu wote walifanya madudu haya na kuona leo Watanzania wanakaa gizani kabisa
 
Kwanza unaelewa nini kuhusu IPP in Tanzania au Independent Power Producer ? Kisheria NSSF kama IPTL na Songas sheria inawaruhusi ku zalisha umeme ila TANESCO bado wana monopoly ya distribution

inanekana umeamua ku bwa bwaja bila kuleta ushahidi wowote ule waka kufanya utafiti wowote ule

wapi Capian wamesign mkataba na NSSF au Tanesco?

You cant even think!?
I agree with you, Tanzania as in govt is currently losing 14bn per day due to loadshedding,

TANESCO is losing 4bn daily due to powershedding

Kazi ya serikali ni kuinvest kwenye umeme, haijafanya hayo kwa muda sasa na kulazimisha 260mw rentals ambazo gharama zake ambazo ni heavy fuel ni 356bn

Umeme wa diesel utageneratiwa kwa 22cents na kuuzwa kwa 10cents, hiyo gas thru dowans, itageneretiwa kwa cent 4 na kuuzwa kwa cent 10

Hizo rentals zitasababisha tarrif ipande kwa asilimia 85 mpo hapo?
 
Its getting old. Seeing and reading Dowans everydays is taking a toll in me. It seems like we as a country are obsessed with smallness. We should be ashamed of ourselves for discussing Dowans since 2006. What a country! Maybe wabongo tumelaaniwa. If as a country we can't reach a consensus on Dowans, we are doomed.

Siasa, paranoia, propaganda and chuki got into reality and grown people cannot make their minds up on small issues like Dowans or Kiwira. Whatever happened to commonsense? Wabongo tuna matatizo.

Kwani, it makes sense for CTI to want Dowans. They are in business that needs UMEME. And DOWANS generate UMEME. How hard is that to comprehend? Damn!

Sheria ni muhimu kufuatwa, ni aibu kwa watanzania kuendelea na imani kuwa Dowans ndilo suluhisho la mgao wa umeme!

Hata hiyo mitambo ya Dowans ikiwashwa mgao mbona utaendelea?

Swali; ni kwanini serikali haikununua mitambo yake tokea kipindi kile Dr. Rashid alipozuiwa kununua mitambo ya Dowans?. Majibu ya swali hili ndiyo chanzo cha suluhisho la kudumu kwa haya matatizo yetu ya umeme. Kwasababu wote tunajua kuna watu ambao ni wazembe na taifa limefika hapa kwa sababu yao, bila kuwawajibisha hao ni ndoto kuwa na nishati ya uhakika!
 
Naona hoja ya msingi ya hii topic ilikua ni CTI na mitambo ya Dowans. Sasa ama kwa makusudi ama kwa bahati mbaya, watu wametoka katika mada na kuanza hoja ya Zitto. Nadhani hatuitendei haki hii hoja hata kidogo maana ina maslahi kwa Taifa, na kwa wote wanaojadili inawagusa ama +ve ama -ve, lakini sasa mjadala umehamia kumshambulia Zitto. Kwa wote nadhani ni wakati mwafaka wa kurudi kwenye hoja na mwenye hoja kuhusu mambo mengine aanzishe thread yake kama anaona ina maslahi kwa umma na kama ni kushambulia watu binafsi, nadhani JF si mahala pake hata kidogo. Mashambulizi dhidi ya watu binafsi ambayo hufanywa na wachangiaji wa kawaida wengi wakiwa wageni ama wamejigenisha kwa malengo maalumu, kwa kuwa wana JF makini (wa dhati) huwa hawashambulii watu, bali hujenga hoja na kuweka ushahidi na wanapokosea hujisahihisha na kuomba radhi ama kuondoa hoja potofu. JF si mahala pa kushambuliana ama kutumia maneno ya kuudhi, ni mahala pa watu wastaarabu na wengi tumeipenda na kuithamini kama kisima cha kuchota mambo mengi ya msingi na kupata mahusiano mema ya kujenga nchi yetu, JF ni hazina ya kujenga udugu na mapambano ya dhati dhidi ya maadui wakubwa wa nchi yetu ikiwamo umasikini, ujinga, maradhi, vyote vikiwa vinaguswa kwa kiasi kikubwa na ufisadi unaobebwa na ubinafsi wa watawala na maswahiba zao. JF imekuwa kimbilio la wanyonge waliokosa pa kusemea. Wanyonge ni pamoja na wale wenye uwezo wa mkubwa lakini wakanyimwa uhuru na nafasi ya kusema wanachotaka kusema na hata wale wanyonge wasio na kitu wanaokosa pa kusemea lakini wanaweza angalao kuingia katika intanenti kefu na kuandika wanachoweza. Wamo wafanyakazi wanaoonewa na kukosa pa kusemea kutokana na kubinywa kwa uhuru kunakofanywa na fedha za rushwa, wako wanyonge wengine wanaokosa pa kusema kutokana na nguvu za kisiasa za wanaotaka kuwasema, wote wamepewa nafasi JF, sasa jamani chonde chonde tusiipoteze nafasi hii adhimu ndani a JF kwa kuichafua na kuifanya ionekana ni jukwaa la kutupiana maneno yasiyo na ushahidi na hata tunapijibizana tutumie maneno ya staha kidogo kw akuwa na tafida. Nimeandika haya kwa uchungu na hisia kali maana kuna nia ya makusudi ya watu kuichafua JF na wana JF bila kujua hata huyo anayechafua JF naye ana haki ya kuwa JF, bila kujua hata anayejifanya anichukia JF ni sehemu ya JF na ana haki ya kuitumia yeye na watu wake bila ubaguzi wowote (mod watanisahihisha). Naamini JF si kama magazeti wala redio, ni jukwaa huru ambalo linaruhusu mijadala huru na ya wazi.

Kuhusu Mradi wa Mchuchuma, Liganga, Kiwira/Kabulo, ni miradi ambayo inahitaji umakini wa hali ya juu na uwekezaji wa sasa ambao umekua wa uwazi, hauna budi kujadiliwa kwa umakini bila jazba, maana uwekezaji wa mwanzo kupitia Tanpower (Kiwira) na MM Steels (Mchuchuma/Liganga) uligubikwa na wingu la ufisadi uliosukumwa na wanasiasa na ulikwenda kwa usiri mkubwa. Sitaki kuamini kwamba waathirika wa uwekezaji wa mwanzo hawahusiki katika hii vita ya sasa ya kuzuia uwekezaji mpya. Tujadili bila jazba na kwa hoja na hili litasaidia sana kupata uwekezaji makini na itasaidia pia kuchukua hatua ikiwa kuna ushahidi wa ufisadi ama uhujumu. Jamani tuangalie TAIFA KWANZA na ubinafsi baadae.

Pole Halisi lakini huwezi kutofautisha kujadili hoja na mtoa hoja,Zito ni Mbunge na ndiyo mtu muhimu sana kuhusu hoja hii kwahiyo na yeye anapojadili kwa vijembe,kiburi,dharau na matusi wewe hulioni msitake kuwafumba watu midomo kwa kisingizio cha kujadili hoja.Zito ni mbunge na naibu katibu mkuu wa CDM,chama kinachotaka kwenda ikulu kikiwa na zito kama mwenyekiti au hata rais 2005(kama anavyoota) nasema kama ni hivi kweli CDM bado ndiyo maana wanaitwa watoto bungeni Na kuhusu hili la kiburi cha zito kwa kumsaidia tu siyo sustainable anakaribia mwisho amuulize Mramba au marmot.Zito acha kiburi nafasi uliyonayo si kwa ajili ya kufuraisha nafsi yako ni kutumikia watanzania na CDM mnaitaji viongozi mahiri na makini
 
You still dont get it dude. Who is Rostam after all and what hole did he crawl out of ? Our war is not with Rostam but with the system, the system that lets filthy rats like Rostam roam our streets with impunity plundering everything that crosses their path. Our war is with sycophants and traitors the type of Selemani and Majimshindo, who would rather look the other way as their masters tear and destroy the fabrics that hold us together as one country.

The bottom line is that as long as Tanzania remains a haven for thieves, drug traffickers, con men and what have you, we are dead though we continue to live !


Mag3.
'' Destroy the fabrics that hold us together as one country''. Red meat! kudos

Guess what, the country is divided from the ruling party to government. Having succeeded on that, now Tycoons are dividing the nation on the line of tribal/ religions.
The Dowans tycoons have infiltrated the idea that, it is due to their faith and not wrongdoing, there is a backlash from the public. Uncovered report on assassination of some leaders has a strong connection with Dowans to prove the point.

The Dowans tycoons have taken the control of central government and now operating by remote. They own media and use every resource to ensure the Pandemonium in the state. These monsters have reaped the nation hefty amount with impunity, unfortunate there some myopic citizens who would like to see this uncouth behavior continue unchecked. Enough is enough!

 
It is even more stupid to link every initiative in Tanzania with Rostam Aziz! Who is Rostam Aziz anyway to be linked to everything. This is cheap propaganda. Yeye amekuwa Pweza anajitandaza kila mahala?

yes...he is untouchable.

Tuogope kufanya maamuzi kwa kuwa atahusishwa Rostam Aziz? Acha upuuzi.

Kwa nini tusiogope? ikiwa hili janga la giza yeye ndiye anahusika.

I dont care nani atachimba makaa pale. What i care ni kuona Kiwira inafufuka, makaa yanachimbwa na umeme unazalishwa. Hizi mbinu za kuhusisha makampuni yanayomilikiwa na watu wenye mawaa ya ufisadi na miradi ili ikwame ni mbinu za kitoto, za kijinga na za kipuuzi.

What do you mean,when you said you don't care nani atachimba huoni kuwa sasa jazba yako inaweza ikaathiri making decision?

Tumeshaumwa na nyoka kwa hiyo watu wanaogopa kila kitu wanaona nyoka kwa hiyo ukileta jazba ndio unavunja moyo kabisa...hizo ndio siasa watu hutukanwa na hata mara nyingine wakatupiwa mayai mabovu
 
yes mkuu .... umerudi kwenye point .... kamati za bunge ni kutoa ushauri au tunaweza kusema ni watchdog ... sasa Lyatonga mrema anasema watu wakamatwe .... hivi huu ndio utaratibu na mwenendo wa kazi au...? mimi nakubali sasa kuwa TANESCO inaingiliwa kimaamuzi tena na watu wasio na experience ya sector hiyo just wao ni wanakamati za bunge.... bullshit

Kaka hongera,umehit points mwanzo mwisho!

Nilianza kusoma tokea mwanzo wa thread nikatafuta mtu aliyeongelea competency ya zitto kwenye energy industry mpaka leo hii awe ndio mshauri wetu watz,nimeona kwako tu!

Huyu jamaa nakumbuka alikuwa penguin pale chuo,leo hii anatuingiza chaka kama consultant wa umeme? Is this a joke??

Hapa lazima sheria za procurement &procedure zifuatwe.

Pia naamini tanesco kuna vichwa; kwani tulikuwa nao pale chuo ni cream tupu ipo pale! Waombwe ushauri,wawe wazi kutueleza wananchi ,n nini wao wanafikiri ,options a,b,c,d if possible!
Or any other approach should be used to get a technical advise directly from technical guys o consultancy firms as per procurement procedure!

I can't read zitto on this, he is too low on this. We have to respect other peoples' professions for God sake!
 
Kama kuna Mkono wa RA na EL nyuma ya pazia la NSSF tumekwisha!
Na kwa jinsi hawa jamaa wanavyopangailia karata zao sitoshangaa,lakini angalau safari hiii wameshtukiwa mapema,kuna nafasi ya kupambana kabla hawajatu do-once!
Tupambane watanzania,GOD LESS US and REJECT THEM mafisadi
 
Huku ni kuleta propaganda kwenye masuala ya maendeleo ya nchi. Ni upumbavu kila wakati kufikiria kwamba kila uamuzi unalenga uchaguzi wa mwaka 2015. Inaonyesha kuna watu wanaweweseka na uchaguzi wa mwaka 2015 na kudhani kwamba kila mtu akili yake ni huko huko. Ni upumbavu kwa sababu haiwezekani kila mradi wa maendeleo unaofikiriwa basi kuna watu wanataka ulaji. Kuna watu tunaendeshwa na fikra za kutenda na kupata matokeo ya kutenda. Haiwezekani tuwe watu wa kuzungumza tu kila siku.

I have no connection whatsover with RA na EL kwenye Urais au mpango wowote wa kisiasa. I say this loud and clear. I am not supporting anybody. I, myself, am ambitious. Siwezi kuingia kwenye miradi ya watu kutaka Urais kwani wote mnaowataja na kuwaunga mkono au kuwapinga naona hawana uwezo wa kuongoza Taifa hili.

Usinifanyie propaganda za kijinga. Ninafanya kazi yangu kwa mujibu wa kanuni za Bunge. Sasa kama unataka niwe mwenyekiti posho, kukaa bila kutoa masuluhisho ya maendeleo ya nchi, go and hang yourself. I am not like that. I am action oriented. Call me arrogant or whatever the names, i am different. Mark my words! Acha propaganda kwenye maendeleo ya nchi.

NSSF
Sitafuti support ya mtu yeyote yule. Hoja za NSSF kukabidhiwa Kiwira nimeziweka wazi. Wala sijajificha kama wewe unavyotumia pen name hapa kwa unafiki wako. NSSF wameikopesha sana TANESCO. NSSF wana haki ya kuwekeza kwenye jambo lolote litakaloleta faida kwa mfuko. Hoja zako za kitoto eti why not TANESCO. Mbona Ngaka na Mchuchuma watakaozalisha umeme ni NDC? Nao tuwatoe tuwape TANESCO? Hayo ni mawazo mgando. It is stupidity to stay out there and wait for people to come with solutions and start criticising the solutions. It is even more stupid to link every initiative in Tanzania with Rostam Aziz! Who is Rostam Aziz anyway to be linked to everything. This is cheap propaganda. Yeye amekuwa Pweza anajitandaza kila mahala?

Tuogope kufanya maamuzi kwa kuwa atahusishwa Rostam Aziz? Acha upuuzi.

Kwamba Caspian watapewa tender ya kuchimba makaa. Huu ni upuuzi tu ili kujenga chuki na fikra hasi za initiative ya kuhakikisha Kiwira inafufuliwa. I dont care nani atachimba makaa pale. What i care ni kuona Kiwira inafufuka, makaa yanachimbwa na umeme unazalishwa. Hizi mbinu za kuhusisha makampuni yanayomilikiwa na watu wenye mawaa ya ufisadi na miradi ili ikwame ni mbinu za kitoto, za kijinga na za kipuuzi.

Hizi ni propaganda za kishenzi kabisa!

On my agenda - moja mchuchuma na Liganga miradi ianze. Mbili, Ngaka coal fields mradi uanze. Tatu, Kiwira ifufuliwe. Nitahakikisha kwa kupitia kamati yangu tunawezesha NDC na NSSF wanatekeleza miradi hii na kuliondoa taifa kwenye tatizo la umeme katika muda wa kati.

I dont care about the next election. I do about the next generation.

Endelea kumwaga sumu zako. Sibabaiki. I do the right thing and inshaallaah i will succeed for the benefit of my country!

Mh. Zitto nashukuru kwa majibu ingawaje umejibu kwa jazba.

Let us go in Facts on this SAGA in few lines.

1) I agree with U that Kiwira should be developed quickly to add power to the National Grid and also to sell excess coal overseas.

2)The issue then comes, NSSF is neither a power company nor has any expertise in this field of power generation. Whichever way U cut it, NSSF will need a PARTNER to generate Power and also to mine coal.

Hapo sasa ndio mchezo mchafu unapotaka kuchezwa. Tanesco ni shirika la umma na lina matatizo makubwa sana ya Cash flow sasa kama wakiwezeshwa kwenye KIWIRA faida kubwa itapatikana na hiyo faida Tanesco watatumia kwenye POWER DISTRIBUTION ambako kunahitaji massive investments.

So issue here ni PARTNER WA NSSF awe TANESCO au ?????????.............

Kwa kuwa kamati yako inasimamia both Mashirika, tulitazamia uwe mbele kutaka hii win win SOLUTION, yaani NSSF wanafinance wanapata interest yao say 10% per yr ( WITH GOVT GUARANTEE) na Tanesco wanapata faida kwa kugenerate power na kutumia pesa kuimarisha miundombinu ya kusambaza umeme.

IS THERE ANYTHING WRONG WITH THE ABOVE SUGGESTION Mh. (MB)??????

May God Bless Tanzania.
 
Hatuwezi kukaa miaka 5 tunaongelea Dowans tu. Ni nchi gani sisi?

Hili ni swali ambalo wengine tuliliuliza miaka mitatu iliyopita; tumepiga kambi kwenye bonde la ufisadi. Watawala wetu ndio wangeweza kututoa hapa kwa kuwajibika lakini hawataki. Siyo kosa letu sisi kuzungumzia. Dowans ni kilele cha uzembe na wangeweza kulimaliza jambo hili kabla halijaanza hawajafanya hivyo. Kwa kupenda mambo mepesi hatutaki kugonganisha vichwa; tunataka tukubali tu "yaishe" kwa sabbau tukijadiliana sana basi inakuwa kama "inachosha hivi".

demokrasia siyo kuburuzana ni kushawishiana. Hadi hivi sasa wenye hoja ya kutaka Dowans iwashwe hawajaweza kutushawishi kwa sabbau kimsingi hoja yako inataka kupuuzia mengine yote yaliyotokea na kutokana na Dowans kwa kisingizio kuwa "Taifa lina mahitaji ya umeme, basi yawashwe".

That is a very faulty way of reasoning.
 
Wasiwasi wangu ni kuwapa hawa NSSF kila kazi ambayo Serikali au Mashirika mengine yameshindwa. Kwa nini mashirika mengine yanashindwa na lije shirika jingne la Serikali pia na liweze? kujenga UDOM, wao. Kujenga daraja la Kigamboni, wao. Umeme, wao. Sijui mwisho mtawapa hadi ATCL na hilo pia waliendeshe? nk nk.......

Hawa jamaa kujihusisha na mambo mengi, itaishia kulifilisi shirika hili. Tumeona makampuni makampuni ya magari ya USA ambayo walikimbilia kuwekeza kila sehemu duniani na mwisho wake, wamedoda hoi. Hata kampuni kubwa la meli la MAERSK, walijiingiza na wao hadi kwenye BANK na kuinunua NORDEA BANK ila mwisho wakaja shituka na kusema "wao tangu miaka ya 18-- wamekuwa wakitengeneza na kuhodhi meli, mambo ya Bank, hawayajui. Wakauza Share zao na kujitoa.

Kuipachika kila kitu NSSF kwa sababu tu wana hela za bure za wananchi ambao sijui hata kama wanalipwa inavyotakiwa, itapelekea hata haka kashirika pekee kanakozalisha faida (kiwiziwizi) nako wakafilisi maana ndiyo sehemu pekee imebaki Tanzania inaleta hela nyingi baada ya mashirika mengine yote makubwa kuuzwa. .

asante kwa hii observation...
 
Tanzania system is not clean, our society by itself is not clean. You can't find me 100 Tanzanians who have never ask or receive rushwa. There is an entire class of bureaucratic entrepreneurs out there--mid-level government officials who are stealing our monies kila siku. And those are the same guys wanalalamika kuhusu ufisadi. My point is, hauwezi kuzuia safari kwa sababu abiria mmoja hajalipa nauli. Tanzania has tons of problems, and Dowans is just a small, small ishu. Wanasiasa waache kutuchezea and fix it, so as we can move on to fix education, inflation, barabara na mambo mengine kibao.

Hatuwezi kukaa miaka 5 tunaongelea Dowans tu. Ni nchi gani sisi?


If you don't tackle corruption with ruthlessness you can not fix the other ills of the society. Corruption is not just one of the problems troubling our society; it is the glue which hold all the other problems together.
 
Huku ni kuleta propaganda kwenye masuala ya maendeleo ya nchi. Ni upumbavu kila wakati kufikiria kwamba kila uamuzi unalenga uchaguzi wa mwaka 2015. Inaonyesha kuna watu wanaweweseka na uchaguzi wa mwaka 2015 na kudhani kwamba kila mtu akili yake ni huko huko. Ni upumbavu kwa sababu haiwezekani kila mradi wa maendeleo unaofikiriwa basi kuna watu wanataka ulaji. Kuna watu tunaendeshwa na fikra za kutenda na kupata matokeo ya kutenda. Haiwezekani tuwe watu wa kuzungumza tu kila siku........

Mkuu

  • kwanza angalia siasa sizikufanye uzeeeke kimawazo wakati bado tunakuhitaji sana. Naona jabza inapanda.
  • Pili kumbuka hivi sasa hatuko enzi ya za kina mwalimu JKN ambapo ni wanasiasa ndo walikuwa wanajua solution za matatizo yote. Hili ni Kosa CCM wanaendelea kulifanya.
Sasa sijui wewe unayosema ununga mkono je umepata cosnultantcy ya kirafiki au kiofisi kutoka kwa wataalam wowote kama

  • wakufunzi wa chuo kikuu na vyuo vingine wa mmbo ya nishati
  • maengeneer wa Tanesco
  • wataalm mbali mbli
Remember hata Hii dowans chanzo chake ni wanasiasa walipodhani wao ndo wanajua A-Z

Nyie kama wanasiasa wenye majibu mbadala mkiwa mjukwaani onekaneni tofauti na CCM. support hoja zako kwa kunukuu wataalam wa sekta husika.
 
If you don't tackle corruption with ruthlessness you can not fix the other ills of the society. Corruption is not just one of the problems troubling our society; it is the glue which hold all the other problems together.

Well said.
The question is not discussing Dowans for five years rather what leaders have done to bring the issue to rest.
Leaders are dithering to make difficult decision for the benefit of the nation. Why!

The executive branch of the state and parliament are under siege because at certain point they were the participants of the corruption or at the receiving end. As results of this intrusion in the states organs, the society fabric holding us as a nation is in jeopardy. For instance, if custodians of laws are rallying behind these evils, then who can defend us! No leader who can stand for our right, no leader who can talk on our behalf.

The main strategy of these libertine people is to dissect the nation so that they can pave a way for massive looting. They are using our own tax to plot assassination and instigate fights on streets as it is unfolding now. If we will not stand firm for the rule of the law and honor our principles and values, our future is obscured.
 
Thanks Mwanakijiji for the very useful inform.
Ninachotaka kuchangia ni hili, wananchi tunaona jinsi gani ccm inavyoongozwa na Kikwete kama kipofu na kiziwi vile. Hii sio kuwadharau ndugu zetu vipofu na viziwi ila ni kutumia ukisiasa ndani ya Kikwete kuendesha watanzania kama vile hatupo ila tumepakia bajaji na yeye anaufunguo hataki kutupa tushike usukani. What the hake we want the keys!

Kesi ipo mahakamani ya kuzuiwa kulipwa na wananchi wameshaonyeshwa hawataki kusikia dowans tena na tena hata kama Makinda kuziba Wananchi wasijue kiini cha tatizo. Kikwete anakuja na kusema hata yeye hakupendelea ila Kamati yake kuu ya ccm ika-endorse hili swala. Tena akaja Pinda, Rostam na yule mu-Oman bumbu wazi. Kama ccm wanataka kujua wananchi wanataka nini tufanye petition ya kura na nchi nzima kama Kikwete afahamu jinsi gani tunataka dowans ifukuzwe na owners wao. Hizi njama za kuleta huu ufisadi tena Tanzania ni hatari sana na inaonekana Kikwete asikii na kichwa ngumu sana. Wananchi tukae kujua kwamba hii mitambo isiwafunge watanzania kwamba hatuna options za kuleta umeme Tanzania isipokuwa mitambo ya Rostam. Leo hii watanzania tukiweka bids za kutafuta makampuni ya kuongeza energy sources Tanzania tutapata nyingi sana duniani. Huu ujinga na tactics za January kutumiwa na Rostam kuleta tena Dowans Tanzania lazima tusimamie na kuweka miguu chini - it will not happen in our land again. Rostam ondoeni majenerata yenu nchini na mpeleke huko Costa Rica au Oman au Iran. Kabla sijamaliza niongezee hivi, Pongezi na Shukruni za Dhati kwa Mashujaa Wote Tanesco Wanaokataa Kurudishwa kwa Dowans Tanzania. Anaezuia upatikanaji wa umeme Tanzania ni Kikwete kwa sababu anang'ang'ania kumuingiza Rostam kama mteja wa watanzania - there options rather than ufisadi

Zaidi Nawapongeza na Kujipongeza Watanzania Wote kwa Kuweza Kuzuia Mpaka Sasa Kulipwa kwa Dowans na Kukataa Sera za Rostam Tanzania. Onyo la Mwisho kwa Serikali ya Kikwete, Mkituletea Siri na Kumlipa Rostam Tutawaonyesha Utanzania​
 
Back
Top Bottom