OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Sera ya Fedha(Monetary Policy) ni hatua za makusudi zinazochukuliwa na BoT ili kuthibit Uchumi. Leo katika Uzinduzi wa Jengo la BoT Mwanza, Gavana wa BoT, Prof Florens Luoga ambaye kwa taaluma ni mwanasheria nimeona ametaja matumizi ya fedha taslimu kuwa changamoto dhidi ya Sera ya Fedha.
Ukiachilia hilo, BoT ktk website yao wameweka wazi pia kuhusu Global Prices kuwa zinaathiri uwezo wa Sera ya Fedha, Global Prices ni pamoja na bei za mafuta ambayo kimsingi BoT hawana mamlaka nayo.
Aidha kuna suala la nchi kutumia fedha ya kigeni kufanyia manunuzi (Dollarization) huwa ni changamoto kwa sera ya fedha japo kwa studies za ndani zimeonesha kuwa dollarization sio tatizo kwetu, msome Kessy, P, Nyella, J, & Yabu, N. (2015). Lakini kifupi ni kuwa kiuchumi inatambulika kuwa Dollarization ni tatizo.
Shida nyingine ni cross border lending mabayo kwa kiasi kikubwa huwa ina import economic shocks, msome Kombe (2015) na (Montiel, Adam et al. 2012) aidha taarifa za fedha za BoT zimeonesha kukua kwa cross border lending hivyo uwezo wa Sera ya Fedha unazidi kuwa mashakani.
Msisahau ya kuwa CMSA imekiri wazi watu kuwa na ufahamu finyu wa masoko ya fedha hivyo ushiriki ni mchache na hivyo hufanya sera ya fedha kuwa na changamoto kwenye utekelezaji wake. Katika haya yote jumlisha na Magendo.
Leo mama ametaka BoT wajiandae na Crypto-Currency, nao raia wameona hayo mambo yaruhusiwe nchini, lakini kwa changamoto tulizo nazo na sera yetu ya fedha tukiongeza na hii ishu ya crypto-currency, Je, Sera ya fedha itakuwa na uwezo wowote? Au tutakuwa sawa na nchi iliyofanya hard pegs(Dollarization) ambapo hata ule uwezo wa Seignorage ukapotea kabisa na BoT wakashindwa kazi msingi ya kudhibiti uchumi.
Niweke wazi nimesoma maandiko kadhaa ya WB kuhusu Crypto Currency lakini na wao wako katika shida ya hii kitu kuhusu kuikubali kutumika.
Wale mnaodhani Rais ameruhusu Crypto-Currency mmefikiria haya, au ni matangazo ya uwekezaji mnayoambiana yamefanya muone ni jambo jema bila kuangalia long term effects?
Signed
OEDIPUS
References
Kessy, P., Nyella, J., & Yabu, N. (2015). Transaction Dollarization in Tanzania. Bank of Tanzania.
Kombe, C. A. (2015). The Relative Importance of Foreign and Domestic Shocks for Macroeconomic Fluctuations in Tanzania. Working Paper Series No 3. Bank of Tanzania
Montiel, P., Adam, C., Mbowe, W., & O’Connell, S. (2012). Financial Architecture and the Monetary Transmission. International Growth Centre.