Crypto - Currency haitapoteza kabisa uwezo wa BoT na sera ya fedha kudhibiti uchumi?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Sera ya Fedha(Monetary Policy) ni hatua za makusudi zinazochukuliwa na BoT ili kuthibit Uchumi. Leo katika Uzinduzi wa Jengo la BoT Mwanza, Gavana wa BoT, Prof Florens Luoga ambaye kwa taaluma ni mwanasheria nimeona ametaja matumizi ya fedha taslimu kuwa changamoto dhidi ya Sera ya Fedha.

Ukiachilia hilo, BoT ktk website yao wameweka wazi pia kuhusu Global Prices kuwa zinaathiri uwezo wa Sera ya Fedha, Global Prices ni pamoja na bei za mafuta ambayo kimsingi BoT hawana mamlaka nayo.

Aidha kuna suala la nchi kutumia fedha ya kigeni kufanyia manunuzi (Dollarization) huwa ni changamoto kwa sera ya fedha japo kwa studies za ndani zimeonesha kuwa dollarization sio tatizo kwetu, msome Kessy, P, Nyella, J, & Yabu, N. (2015). Lakini kifupi ni kuwa kiuchumi inatambulika kuwa Dollarization ni tatizo.

Shida nyingine ni cross border lending mabayo kwa kiasi kikubwa huwa ina import economic shocks, msome Kombe (2015) na (Montiel, Adam et al. 2012) aidha taarifa za fedha za BoT zimeonesha kukua kwa cross border lending hivyo uwezo wa Sera ya Fedha unazidi kuwa mashakani.

Msisahau ya kuwa CMSA imekiri wazi watu kuwa na ufahamu finyu wa masoko ya fedha hivyo ushiriki ni mchache na hivyo hufanya sera ya fedha kuwa na changamoto kwenye utekelezaji wake. Katika haya yote jumlisha na Magendo.

Leo mama ametaka BoT wajiandae na Crypto-Currency, nao raia wameona hayo mambo yaruhusiwe nchini, lakini kwa changamoto tulizo nazo na sera yetu ya fedha tukiongeza na hii ishu ya crypto-currency, Je, Sera ya fedha itakuwa na uwezo wowote? Au tutakuwa sawa na nchi iliyofanya hard pegs(Dollarization) ambapo hata ule uwezo wa Seignorage ukapotea kabisa na BoT wakashindwa kazi msingi ya kudhibiti uchumi.

Niweke wazi nimesoma maandiko kadhaa ya WB kuhusu Crypto Currency lakini na wao wako katika shida ya hii kitu kuhusu kuikubali kutumika.

Wale mnaodhani Rais ameruhusu Crypto-Currency mmefikiria haya, au ni matangazo ya uwekezaji mnayoambiana yamefanya muone ni jambo jema bila kuangalia long term effects?

Signed

OEDIPUS

References

Kessy, P., Nyella, J., & Yabu, N. (2015). Transaction Dollarization in Tanzania. Bank of Tanzania.

Kombe, C. A. (2015). The Relative Importance of Foreign and Domestic Shocks for Macroeconomic Fluctuations in Tanzania. Working Paper Series No 3. Bank of Tanzania

Montiel, P., Adam, C., Mbowe, W., & O’Connell, S. (2012). Financial Architecture and the Monetary Transmission. International Growth Centre.
 
Binafsi sina utaalamu lakini naona mama ameruhusu tuangalie tunaweza kuwa na sehemu gani kwenye eneo hilo. Ni kitu kizuri, siyo siku dunia inahamia Crypto halafu inatukuta hatujajiandaa kabisa.
 
Binafsi sina utaalamu lakini naona mama ameruhusu tuangalie tunaweza kuwa na sehemu gani kwenye eneo hilo. Ni kitu kizuri, siyo siku dunia inahamia Crypto halafu inatukuta hatujajiandaa kabisa.
Mataifa mengi yaliyoendelea hayajaruhusu hii kitu, inaweza kuondoa kabisa nafasi ya BoT, na uchumi hautaweza kuwa regulated na BoT

1. Crypto-currency haidhibitiwi na Central Banks
2. Kama inavyoitwa Block chain, maana yako haiwezi kuwa tracked, Sasa angalia nchi zilizoruhusu hizo payments kisha fananisha na uharamia uliopo
 
Tatizo hapa nchini kuna watu wanesoma uchumi na masuala ya fedha ila hawajitambui kabisa yaani hawana msaada kabisa.
 
Tatizo hapa nchini kuna watu wanesoma uchumi na masuala ya fedha ila hawajitambui kabisa yaani hawana msaada kabisa.

Kabla haujafika kwenye hii conclusion nikuulize, je umesoma machapisho ambayo yako BoT, (Working Paper series) Umeona recommendations wanazotoa kwenye kila andiko

My point wachumi wapo na wanaandika,

Theoretically BoT inabidi iwe mshauri wa serikali kwenye masuala ya kiuchumi, lakini kwa nchi yetu serikali ndio mshauri wa BoT, Means kama Rais amesema maneno yake, hakutakuwa na study ila wataanza kufanya kwa kuwa ni kama order, ilhali ni yeye Rais ili bidi aambiwe kwa facts kuhusu hizo kitu
 
Mataifa mengi yaliyoendelea hayajaruhusu hii kitu, inaweza kuondoa kabisa nafasi ya BoT, na uchumi hautaweza kuwa regulated na BoT

1. Crypto-currency haidhibitiwi na Central Banks
2. Kama inavyoitwa Block chain, maana yako haiwezi kuwa tracked, Sasa angalia nchi zilizoruhusu hizo payments kisha fananisha na uharamia uliopo
Ni vema wajiandae mkuu(mama kasema wajiandae). Dunia inakoelekea nguvu ya serikali inazidi kupungua. Wanasema kilele cha ubepari ni anarchy. Ndiko tunakoelekea. Kizazi cha sasa hakipendi centralized power kwa hiyo tutegemee uwezo wa Central bank kucontrol sera za fedha kuzidi kupungua. Naona ni vyema wakijiandaa kwa hali hiyo.
 
Binafsi sina utaalamu lakini naona mama ameruhusu tuangalie tunaweza kuwa na sehemu gani kwenye eneo hilo. Ni kitu kizuri, siyo siku dunia inahamia Crypto halafu inatukuta hatujajiandaa kabisa.
Hatuna ujanja kukwepa crypto, nashukuru kwa hili kwani tulichekwa sana wazee wa crypto
 
Hatuna ujanja kukwepa crypto, nashukuru kwa hili kwani tulichekwa sana wazee wa crypto
Niliangalia Documentary moja kuhusu Crypto, nilijifunza mengi sana. Zamani nilijua ni utapeli. Tunakoenda lazima kama nchi tujiandae. Miaka 30 ijayo sijui crypto itakuwaje?
 
Ni vyema serikali ikawaandaa wataalam wake wa uchumi ili wajifunze kuhusu crypto. Ili endapo dunia itahamia huko basi itukute tayari tuna wataalam ambao angalau wanaelewa ABC za crypto.
 
Mi teali nimeshafanya miamala ya pesa kupitia local bitcoin, ni nzuri ila inahitaji umakini kidogo ukizubaa unanapoteza pesa.
 
Back
Top Bottom