Cryogenically Frozen: Sehemu zinatumika kuhifadhi miili ya watu waliofariki

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,425
Nchini Marekani, Kuna zaidi ya Sehemu 100, ambazo zinatumika kuhifadhi miili ya watu waliofariki.

Sehemu hizo zimejengwa katika Hali ya kuweza kuifanya miili hiyo isiharibike na kubaki katika Hali ya kawaida.

Hii inatokana na imani ya kwamba katika miaka ijayo, Binadamu watakuwa na uwezo wa kurudisha maisha ya watu waliofariki.

Hivyo, watu wengi kabla ya kufa hutoa Order yao kwamba hakifa haifadhiwe huko, ili ikitokea siku Binadamu akafanikisha kurudisha uhai Kama wanavyo tumaini Basi nao wawe moja yao Kati ya hao.

Wapo wengi walio hifadhiwa huko akiwemo, Walty Elias Disyney, mmoja Kati ya waanzilishi wa kampuni ya kutengeneza films, ya Walty Disyney.


CHIMBUKO LAKE

Mtu wa kwanza aliyekuwa amehifadhiwa katika mfumo huu wa "Cryogenically frozen" alikuwa mwanasaikolojia mwenye umri wa miaka 73, Dk. James Bedford, ambaye aligandishwa mwaka wa 1967. Mwili wake mpaka sasa bado una hali nzuri huko Alcor Life Extension Foundation.

Nadharia ya watu waliohifadhiwa na kisha akafufuliwa wakati teknolojia ikiwa mbali sana kutokana na kitabu "THE PROSPECT OF IMMORTALITY" kilichoandikwa na mtaalamu wa fizikia Robert Ettinger mwaka wa 1964. Neno "cryonics" linatokana na Neno la Kigiriki kwa "baridi."

Mwishoni mwa miaka ya 1970, kulikuwa na makampuni sita ya cryonics nchini Marekani. Lakini kulinda na kudumisha kila mwili kwa muda usiojulikana ilikuwa bei mbaya sana, watu wengi wa makampuni haya walipiga pesa za maana kwa miaka kumi mfululizo.

Leo, watu wachache tu wa makampuni hutoa huduma kamili za cryosuspension, ikiwa ni pamoja na Alcor Life Extension Foundation huko Arizona na Taasisi ya Cryonics huko Michigan. Mapema mwaka 2004, Alcor alikuwa na wanachama zaidi ya 650 na wagonjwa 59 katika cryopreservation.
 
Cryonics itafanikiwa but very late kabisa compared na mafanikio ya mind aploading...

Kwa msaada wa Nanotechnology kuna uwezekano wa kufanya mind( mental intelligence) apload in the future time kuliko cryonics...

Tayari kampuni ya Spacee X imeingia mkataba na kampuni ya McMullan ambayo ipo sweden tayari kuanza kutengeneza chips ambazo zitapandikizwa kwa kila embryo aliyopo tumboni kwa mama mjaamzito kwa kutumia micropipete injection au Direct Chip Innoculation(DCI) au kwa kutumia Vaccine Innoculation ili akizaliwa tayari inakuwa ishafika na kuji embed kwenye brain kisha kuanza kumonitor mind process na kuhifadhi data zake kwenye hizo subchip ambazo zina GIGABYTE ya kuhifadhi katika kufanya mind apload yake ..

Mtu akifa tayari kichipi kitakuwa kimebaki kwenye brain na tutakitoa kisha kikiweka kwenye machine ambayo tutaaanza kuona mawazo yake na process nzima ya mfumo wake wa ubongo na jinsi unaavyofanya kazi kuanzia akiwa tumboni mpaka amekua na source of death...


Manake tutakuwa tushafanya total mind apload kwa yule mtu na kuihifandhi kwenye chip.

Kumbuka mind ndo uhai wa kiumbe yoyote...hivyo ukiweza kuhamisha mind tayari umehamisha ufahamu ( consciousness ) yake...na ufahamu ndo maisha halisi ya mtu husika...

Ukifa sisi tunatoa kichip chetu kwenye ubongo ambacho kilikuwa kimelink na neural circuit zako hence kufanya mtiririko mmoja wa mind...

Hivyo consciousness yako itakuwa ipo kwenye chip coz linkage yake imefanyika since embryology yako..

Kwa hiyo kwa kuwa ufahamu wako wote utakuwa kwenye ki chip ,tutaweza kuendeleza ufahamu wako kwa kuupandikiza kwenye Artificial Human Body ambazo zitaanza kutengenezwa kwa msaada wa "Human body cloning" kupitia process za "Somatic Cell Nuclear Transfer" ambapo mtu anayehitaji kurudishwa maisha baada ya kufa atatakiwa kudonate( kutoa) cell yake moja tu kishaa tutaiprocess na kuihifadhi ili akifa tunaitimia hiyo cell yake moja kufanya exactly body cloning yake...

Kwenye human body cloning tutaweza tengeneza copy yako halisi kwa kuwa tutakuwa na access ya cell zako pindi ukiwa hai...hivyo tutakuclone ili tupate exactly copy ya mwili wako kisha kuweka ile chip yako iliyosynchronize kwa kuhifadhi intelligence yako ....hapa tutaweza kuseparate intelligence ya clone na yko kwani kwenye ile cell yako tutaweza kuitoa gene inayohusika na intelligence ili tutakapofanya cloning ya mwili wako basi ubongo uje ukiwa hauna Intelligence make accesss ya intelligence yako tunayo kupitia ile chip...tutatakiwa kuipandikiza tu kisha kufanya total memory back up kwa mashine maalumu na mwili utaaanzaa kufanya kazi na ufahamu wako utakufanya ukukumbuke kabisa kuwa ni wewe na utajiona ulikuwa umelela usingizi mzito na sasa umeamka..

Baada ya hapo utaweza kuwa hai tena ,ikumbukwe kuwa kuanzia process zote tangu ulipozaliwa na kukua na kuinteract na watu mpaka ulivyokuwa na mpaka ulipofikia hatua ya kufa taarifa zipo kwenye ubongo wako ambao ndo ile chip yako ..

So that's how human being is going to survive under several phases huku kumbukumbu yako ikiwa ndo msaada pekeee wa kukurudisha ulipoishia...

So Cryonics inaweza ikafeli au ikachelewa kama nanotechnology itawahisha utengenezaji wa chip amazo zitakuwa na bytes maalumu katika kufanya mind apload ...

All in all science is fantasy .......
 
Mind apload ndo habari ya muuujiniiii kwa wenye pesa..

Unawekewa kifaa cha kuwa kinahifadhi kumbukumbu zako na pindi unapokufa tunakitoa kisha tunamuwekea clone wako kisha unakuwa wewe...

Hakutakuwa na utofauti na original (ulivyokuwa )kwani uhalisia wa mtu ni ufahamu halisi.
PhotoGrid_1552813510407.jpeg
 
Mind apload ndo habari ya muuujiniiii kwa wenye pesa..

Unawekewa kifaa cha kuwa kinahifadhi kumbukumbu zako na pindi unapokufa tunakitoa kisha tunamuwekea clone wako kisha unakuwa wewe...

Hakutakuwa na utofauti na original (ulivyokuwa )kwani uhalisia wa mtu ni ufahamu halisi.View attachment 1047503
Kwa hiyo huyu mtu mpyaa atakuwa hauguii wala kufa tena si ndio
 
Lakini mkuu hii mambo haitawahusu walioharibika miili kama waliopata ajali wakabondeka, waliopigwa risasi n.k au ikoj hiyo?
soma vizuri maelezo yangu...lazima kuwe na human body cloned kwanza...ukifa ukabondeka bondeka tunachukua cell yako moja kisha tunarudisha copy ya mwili wako kama ulivyokuwa halafu tunapandikizia hiyo intelligent microchip ambayo tutaitoa kwenye ubongo wako( kama ulikuwa ushewekewa kifaaa cha kuapload mind kichwani mwako)

Ni process tata sana but itafanikiwa tu...its like joking but its going to happen real...
 
Watu waliohifadhiwa kwa hizi technology baada ya kufa ni matajiri tu na wanasiasa maana kuuhifadhi mwili malipo huwa yanaendelea kutolewa tu,,kikubwa nikwambie mkuu kama quantum physics ingelikuwa kwenye mtaala wetu ingefaa upate mda wa kufundisha..ila inapokuja unaongelea suala la imani huwa unakinzana na sisi wafia dini.
mtoa mada nadhani anaelewa utofauti kati ya Cryogenics na Cryonics. ....ukielewaa hizo terminology mbili basi utakuwa unajua paa kuanzia na utajua maanaa halisi.
 
Inaonyesha bado kuna hatua za kufanyika hadi ije kuwa official; hilo lakuhifadhi is possible hadi hivi sasa kama unaweza kumudu gharama zinazotakiwa.
 
Endeleeni kujidanganya tuuu

Umeandika maneno machache na yenye ukweli muhimili,maneno yanaweza kuandikiwa vitabu vyenye kurasa nyingi sana na zenye kutajika na kupewa jina "FITINA ZA UONGO WA KISAYANSI" na watu na watu wakasoma na kuondokewa na ujinga walio nao sasa.

Nipo .....!
 
Kwa hiyo huyu mtu mpyaa atakuwa hauguii wala kufa tena si ndio
Cloned human anaweza kuwa subjected kwenye mazingira yoyote yale yanayomwaffect binadamu pia...

It's like Wako Jacko...

He died since then but his clone was surviving na alikuwa anapatiwa matibabu kama kawaida akiugua n.k ....So ni binadamu ambaye kapewa ufahamu kupitia chip mind controller na anapata kuwa mtu katika mazingira yote ..
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom