Crossroads: Ex wa mke wangu wanaendelea kuwa karibu na wife hadi sasa

Andaa mission ya miezi mitatu ambayo itahitimisha mapenzi yenu. Kumsamehe msaliti ni kujiwekea kitanzi.
 
Willy Wills

Umesikia mengi. Bottom line is, you had life before her, with her and surely you will have life after her.

Hoja yangu ni ongea na mkeo kwa upole na hekima. Mjulishe kwamba unafahamu anayofanya na ex wake. Kisha mwambie achague baina yenu wawili.

Akishindwa kuchagua, mwambie yako ya moyoni. Akiyakataa mpe nafasi akuache uanze maisha yako upya. It hurts, but that is the truth. And it shall set you and your lovely wife free thus you may proceed with your side cheek!
 
thanks guys kwa concern yenu! na ushauri. niafuatilia kila ujumbe ninaoupata hapa na kuuweka kwenye mizania. Nilifikiri nijaribu kuongea na dada yake ambaye anamuheshimu na kumsikiliza sana, nami pia tunasikilizana sana. Je wazo langu hili mnaljona vipi?

Mapenzi ni wawili, Dada'ke usimshirikishe.
 
Mkuu unaonekana wewe ni "wale watu", sasa kwanini usitumie mbinu za medani

Kwanza unaweza kum face huyo jamaa na kumwambia ukweli kwamba anatembea na mke wa mtu, na mke wa mtu ni sumu.

Pia, kwakuwa unaujua ukweli na unaona njia ya kuongea na mke wako inaweza isifanikiwe, tumia mbinu za medani kujua weekness za mpinzani wako (wanasema kila mtu ana mambo yake ambayo hataki binadamu mwingine duniani ayafahamu,kila mtu ana side A na B), tumia weekness kum blackmail jamaa, ili jamaa abwage manyanga, yaani apotee kwenye maisha ya mwanamke wako

Njia ya tatu, mpige mimba wife, inaonekana ana muda mwingi wa kufanya ujinga. Sasa ni wakati wa kuwa bize kulea.

Hayo ya juu yakishindikana, hatua KUBWA ZAIDI utakayoichukua kwa mla mke wako, hata Mungu atakusamehe

Lakini ingekuwa mimi, ningembwaga mara baada ya kupata ukweli
 
I'm


Thanks brother, nikiri sina hakika kama ninaweza kukubali kumpoteza. Nahitaji zaidi aachane nae.
Brother, kwanza nikupe pole Sana. Pili mkeo hawezi kuachana na jamaa hata ufanye nini. Amini usiamini tangu ulipofanya mbinu za kumpata alikua hakupendi wewe bali huyo jamaa ila aliolewa nawewe kwakua alipata hasira jamaa yake wa mwanzo alimcheat.

Alimjibu kwa hasira mbele yako ili kumuumiza lakini baadaye waliyamaliza ikabidi wafanye kwa siri kwakua tayari wewe umeshamuweka ndani.

Mbaya zaidi mkeo ni mwanamke wa kushindana na mwanaume na hupenda kulipiza usaliti kitu ambacho huenda ikawa ni tabia yake. Kwako alikubali kuolewa baada ya kukerwa na huyo jamaa na alifanikiwa kumuumiza mpinzani wako lakini sio kwamba hampendi pia kama nawewe ulimkera huenda hata mtoto kazaa na jamaa ndio maana amekua msaada kwake na kwa wazazi wake maana anaandaa maisha ya mtoto.

Siku utakapokuja kujua mengi utalia na huenda ukatamani upoteze maisha yako. Ushauri wangu ukishindwa kumuacha basi kubali aendelee kubebwa na mwanaume huyo maana hawata achana kamwe na kuna siri kubwa nyuma yake ambazo wewe huwezi kuzijua
 
Uwezekano mkubwa hapo ni kuwa "umeshaachwa". Formalize tu hiyo separation, mrudishie mwenye naye.

Ukiua kwa upanga, utauwawa kwa upanga pia.

Pole sana. Anza upya tu, miaka 31 bado ni kijana mdogo tu. Acha woga, jikaze kiume.
 
Nimechelewa kutoa ushauri
Ila pole sana mapenz yanauma sana especially umpendae akuumize
Cha maana mpe mapenz mazur sana kuliko uliowah kumpa apo kabla, hakikisha yur mind is clear

Then baadae unamfata na kumwambia jins gan unampenda na jins gan umeumia baada ya kugundua anakucheat with evidence
Baada ya apo unamtakia maisha mema then unajitoa maishan kwake for good
NB
Kuwa serious na sura ya kuumizwa, na ukitoka apo usimtafte hata mara1

Hii itamfanya aanze kujiuliza kiakilin kama anakupenda wewe au yeye, una advantage ya kuwa tayr mna mtoto
With time ataanza kukumiss sana na kutaman ata asikie saut yko au akuone, akifanya hvyo ongeeni tu kuhusu mtoto na kataa mkutane( this is the best part)
With time atamchukia sana jamaa ataanza kukupenda
 
Hakuna mahusiano yoyote yale yaliyodumu yakawa hayana historia. Kila mwanaume anaweza kumshawishi msichana atakapa anachokihitaji,but when a girl's sense comes back, sio wako tena

Vijana tengenezeni strong bond kwenye mahusiano kiasi kwamba mtu akitaka kukuacha akikumbuka gharama ya mahusiano yenu na mliyopitia anaacha wazo Hilo mara moja.

Sasa huyu jamaa yetu anasubiri eti watu wagombane ndio aoe, anajua kabisa msichana alimuacha jamaa Kwa sababu alimsaliti,yeye naye akaamua kumsaliti halafu anasema hayuko tayari kumpoteza. Huu unaweza kuwa ni utani zaidi ya unaofanywa na serikali ya jiwe
Ngumu kumeza hiyo,
No way mzee baba hapo kuyatenganisha hayo mapenzi ni kama kusema 2020 jiwe atoke madarakani,never hawawezi kuachana kirahisi kiasi icho,
Only one thing"let her go"
 
Honestly ni ufala sana. Wife aliteswa sana baada ya kugundua jamaa anamcheat na kumdump, the moment naanza naye relation alikua ameugua sana baada ya maumivu ya kulia sana takribani wiki nzima alilazwa....i saved her from that situation....i used a lot of money kumrudisha katika hali ya kawaida. Leo the guy aliyemtesa ndio ananicheat naye..... i never cried lakini wa mara ya kwanza
'Wagombanao ndio wapatanao.'Huu usemi unaishi mapaka leo. Wewe ulitumia advantage ya kuumizwa kwa huyu binti na boyfriend wake ukaonekana ni mwema sana na hapo ukatangaza ndoa. Binti hakua na jinsi ukizingatia ulishamtia mimba tayari. Angefanyaje?? Pengine kwa mawazo yake alifikiri huenda ukawa ni mzuri zaidi (kitandani) kuliko huyo boyfriend wake lakini imekuwa sivyo. Mwanamke mmjamzito anapo fanya maamuzi ni tofauti sana na angefanya maamuzi wakati akiwa hana ujauzito kwa sababu ya mabadiliko mengi yanayo tokea ktk mwili wake.
 
Mkuu pole malipo ni hapa hapa duniani.
1) Ulitengeneza figisu umpate mpenzi wa mtu hiyo tubu kwanza
2)jiandae kisaikolojia kuwa single father sababu jamaa angekuwa kapuku ungemuweza naye yuko vizuri
3) Ulitegemea mimba ndio mtego wa kumtenganisha .Umesahau ulikuwa unatenganisha mwili ila si nafsi
4) Usitegemee mafanikio ukiwa na huyo binti labda jamaa aoe
5) 31 bado una mda wa kujipanga upya
6) kazà roho ongea na wife umueleze ukweli achague. Jione huruma kunakulea mtoto wa watu plus maradhi, Jela ,kifo.
 
Uliingilia mapenzi Ya watu hii ndio price unayopay. Huyo mke hakupendi tena, hasira kwa jamaa zimeshamuisha. Mapenzi yamerudi kama mwanzo, ni ngumu sn kumuacha jamaa huyo. Wew jitahid kuongea na mkeo ujue yeye atasemaje kulingana na mashtaka yake hayo.. Khaa kuna watu wanapitia majaribu mazito saana
 
Nimeshavuta embassy now i can say something!

Ni vyema tuanzie kwenye msingi wa tatizo lenyewe.

Ni dhahiri kuwa huyo mkeo alikua anampenda sana huyo ex wake, na wewe ulimuoa kipindi akiwa desperate naye akakubali. So alifanya maamuzi bila kuwa huru. Jambo la Pili ni kuwa wife baada ya kuwa na amani na mfumo mwingine wa maisha yawezekana kuwa akagundua wewe humfikishi kimapenzi, na ikachagizwa zaidi na wewe kuwa na michepuko hivyo ndipo nae akaamua kutafuta alipopaacha kama kumwaga mboga. (kwa ujuzi wangu mdogo wa saikolojia na naona iko hivyo).


Ushauri....jaribu sana kwanza wewe uache michepuko yako na jaribu kuonyesha kuwa uko faithful ili upate moral authority ya kuanza kumbana.

Pili jitahidi utengeze ukaribu naye sana, sababu inaelekea wife wako wamekaa muda mrefu tangu utoto na jamaa hivyo wamezoeana sana. Ukiwa na ukaribu naye atatengeneza mazingira ya kuwa huru sana kwako. kama ulivyosema jamaa anamuhudumia vitu vidogo vidogo na yuko huru zaidi kwa jamaa kuliko wewe.

Mwisho tengeneza mkakati maalum wa kudeal na jamaa. mface umchane wazi kuwa aachane na mkeo.
Alafu mara nyingi wake za watu huwaga huru na ma ex wao kuliko waume zao walio waoa sijui kwann
 
Hello guys!

Kama unasoma ujumbe huu naomba nikushukuru kwa kupoteza muda wa kusoma nyuzi zingine na kujua ni kipi hasa ninahitaji unishauri. Nitaanzia mbali kidogo ili upate mtiririko mzuri wa matukio na nitajaribu kuweka kila detail ya msingi ili ukiweza kunishauri, unishauri vyema. Yawezekana niko desperate kiasi cha kuonekana kuwa nauliza ushauri kwa ajabu ambalo ni la kawaida katika jamii.

Mimi ni mwanaume wa miaka 31 ni mzaliwa na mkazi wa mkoa wa DSM. Nimeoa na mke wangu ana mtoto mmoja. Ni mtumishi wa umma katika 'ofisi kuu' ya Nchi yetu.

....ilipoanzia....

Miaka mi4 iliyopita nilifahamiana na binti mmoja(wife) yeye akiwa ni mtumishi katika ofisi moja ya 'uchunguzi' HQ. Frankly nilimoenda sana at glance na hadi leo nikiri ninampenda sana, sina hakika kama niko tayari kumpoteza. Nikaanza kumfuatilia na kugundua yuko kwenye relation na jamaa mmoja ambaye ni mwanafunzi wa law SAUT mwanza, na binti alikua deadly in love with the guy ambaye wamekaa for almost 3 years back then since wakiwa High school. Jamaa anatoka mkoa mmoja na binti(lake zone). Hivyo nikaona ugumu ulipo kumpata. Nikaendelea na hustle za kumfuatilia ili nijue vita ikoje, nikichukua advantage kuwa binti niko naye dar na jamaa yuko huko mwanza. Nikaja gundua pia jamaa angalau twice per month huwa anakuja dar kwa binti na alikua akifikia nyumbani kwa binti ambapo wanaishi na sista yake. Pia nikaja gundua financially jamaa hakua vibaya sana (though hakunizidi) kwani mzee wake alikua ni 'kigogo' wa council moja huko kusini, na alikua akisimamia projects kadhaa za ujenzi za mzee wake hapo Mwanza, pia alikua na mkopo chuoni. sources ziliniambia jamaa alikua akimpiga tafu binti kwa issues nyingi kama house rent kidogo, issues mbili tatu za kimaisha. Nikagundua pia binti alikua akimumini sana jamaa, ingawa jamaa alikua ni player wa siri sana na mtu wa pombe sana... nilihisi kushindwa pambano....

...2015 march nipata info kuwa jamaa ameenda weekend kuspend uganda na ameondoka na rafiki yake na madem wawili bila kumuambia binti. Nikafanya makeke taarifa zikamfikia binti. Hapa binti akaanza kuloose trust na jamaa. To me ilikua ni point tatu. Aliporudi Uganda jamaa akaja dar, kisha binti akagundua messages za mapenzi na dem mmoja wa jamaa.. sikujua what happened next.

....few days later nikapata taarifa binti yuko frastruated na anaumwa baada ya kugundua nasty things za jamaa yake. I took advantage na nikawa close na binti nikamcare sana....siku moja tuko naye jamaa kapiga dem akamjibu dry kuwa yuko namimi hawezi ongea na simu. I told myself that im about to win... Nikawa close na binti finally nikamtia mimba na punde nikatangaza ndoa, binti aka convert kufuata dini yangu and we married. from then hakua binti tena bali wife and she gave me baby girl.....Thanks God shem zangu hawakua na shida na Mimi wala mama mkwe wangu 2015-2017 things were cool na nilijiridhisha kuwa binti hakua na mawasiliano na binti...

bahati mbaya tuliingia kwenye quarrels kadhaa baada ya kunigundua red handed mara kadhaa kuwa nina mcheat. We peacefully solved shida zetu...

But i started kunote tofauti fulani fulani. Wife hakutaka tena nishike simu yake on ground kuwa mimi sitaki ashike yangu. Mwaka huu mwanzoni nikakuta namba fulani imempigia, nikampigia na nikapokelewa na mwanaume, nikamwambia mpigie fulani (wife) alikua anakutafuta, jamaa akanijibu yeye anayo namba yangu kwanini asinipigie mwenyewe. Nikakata simu.

baada ya wiki kadhaa, nikaona namba ya jamaa imeweka d.p picha ya wife kilichonistua ni kuwa that pic sikuwahi iona..it was like my wife selfied herself and sent a pic straight to the guy. Nikachat na jamaa na kumtumia picha za wife zingine na kumuambia... weka na hizo profile....but hakunijibu chochote cha kumfanya nione kuwa wako naye kimahusiano. Jamaa alikua smart sana kwenye majibu yake akiavoid kuwa caught, nikampigia simu wife kumlalamikia kuwa kwanini mtu anaweka picha zako dp. wife akaniambia mimi ndio nina makosa zaidi na kama ningekua namuheshimu nisingemtumia picha zake zingine. Nikawa mpole i deleted those pic i sent to the guy...
some few minutes dp ya jamaa ikabadilishwa na kuwekwa pic ya dem mwingine. Namba nikainote kuicheck mpesa ina jina la kike. Nikachukua jukumu la kutrace msgs za jamaa using my position, sikuona kitu cha maana chochote zaidi ya salam. Na kuna mgs za kushukuru wife ametumiwa pesa na jamaa. Nothing shocking i noticed. Baada ya kama mwezj ile namba haikuwa hewani tena..

.....shida kubwa ikaja hapa miezi kama miwili imepita.....

as u all know public offices zinahamia dom, na mimi niko huku almost 4 months now. Nilichokuja gundua wife ananicheat. Na ananicheat kwa mtu mmoja tu, naye ni yule yule jamaa yake aliyemuacha na mimi kumuoa.

kama wiki 3 zilizopita, jamaa yangu alinitaarifu kuwa shem nimemuona lodge fulani magomeni kwa nje its like anampigia simu mtu, bahati mbaya hakujua kinachoendela sababu alikua kwenye shughuli za kiofisi. Kumpigia simu wife kumuuliza alipo, akajibu yuko ofisini. Nikamuuliza informer wangu pale ofisini kwake, akanijibu yeye hayupo ingawa gari yake ipo. i took it easy. Siku 4 baadae nikarudi dar, sikunotice shida yoyote kwa wife. nikaka kama wiki 1 pale dar nikifanya upelelezi wangu pale lodge aliyofikia. Nikipata msaada wa binti mmoja nikaonyeshwa Cctv footage ya ile hotel. Niliumia sana niliyoyaona. wife amefika pale mara tatu. Ya kwanza ndio ile aliyoonwa na jamaa yangu, second one ilikua saa 11 asubuhi na kutoka saa 3. Nikajiuliza ina maana siku hiyo hakwenda kazini. nikafuatilia na kugundua siku hiyo alitoka nyumbani saa 11 na kisha kureport kazini saa 3. What hurted me the most ni mara ya tatu... Hii ilitokea a day before, nami nikiwepo. Siku hii nakumbuka nilimuaga wife naenda town kurekebisha gari by saa 10 jioni nitakua nimerudi, mida hiyo ni saa 6. Nikiwa garage wife alinipigia sim kuwa atatoka for almost 2 hours ana issue kazini, nikamuambia poa. footage ilinionyesha kuwa aliingia pale saa 7 na ilimuonyesha akitoka saa 9 na robo. alitoka akiwa anasindikizwa na jamaa kavaa vest na boxer tu kutoka floor ya 3 hadi ground floor na jamaa akarudi. Siku hii kilichonishangaza wife alitumia uber. Bila shaka nikathibitisha wife ananicheat, na ananicheat kwa mtu ambaye yule yule niliyemdhania miaka mingi..

But nature i dont take quick judgement. Nilijipa muda wa kutafakari na kujua how deep wako na huyo jamaa this time around.

Nikafanikisha kupata namba ya jamaa. kwanza imesajiliwa kwa jina la kike.

nikagundua wana chat zaidi whatsapp hii sikuweza kung'amua kipi ni kipi. Ikabidi nicheck text messages. niliyoyakuta, hurted me the most.

1. wife na jamaa walikua wakikumbushiana ni jinsi gani walivyokua wana enjoy sex. Kila mmoja akimsifia mwenzake kuwa yuko vizuri. Lakini wife ndiye aliyekua akimsifia zaidi jamaa kuwa ni mwanume pekee anayemjua vyema na kipi cha kufanya kuwa the guy knows how to satisfy a woman. This pained me much

2. walikuwa wanazungumzia sexual fantasies zao. kila mmoja akimwambia kipi wanatamani wafanyiane. hapa paliniumiza sana, kwani wife alimuambia jamaa wakikutana atampa vyote anavyotamani na ambavyo hawakuvifanya. wife pia amemuambia jamaa they have to arrange for threesome na jamaa amekua tasked atafute dem ambaye anamuona anafaa and they guy promised to work on it.

3. wife na jamaa wanasaidiana mambo mengi hasa financially, mfano jamaa alimuongezea wife 1 M ya kununua kiwanja huko kwao, pia jamaa alimnunulia sim wife, ambayo nilijua kwa kazi yake wife simu kununua sio issue kubwa. na vitu vidogo vidogo vingi jamaa anafinance wife. Pia maza wake na wife jamaa ana msupport sana as wanaishi the same town. wife anakiri kwa jamaa kuwa yeye ndiye mwanaume pekee ambaye yuko free sana kumuambia chochote na akamsikiliza.

4. hakuna point hata moja niliyonote kuwa walishawahi kunizunguzmia, hilj linanipa shida sana. je wife hajamwambia jamaa kuwa hajaolewa? au jamaa

Guys, nimenote mengine sana, ingawa naamini kuwa mengi zaidi yapo kwenye whatsapp. nikiwa na wife, i never doubted wala openly noticing kuwa ananicheat, sim yake yuko free nayo muda mwingi na usiku hata nikiwa naye haipigiwi.. mimi ni as a man i know how hard it is to cheat na kuficha, hivyo i trusted wife 100%.


I deeply seek a wise advice from you guys on basisi kuwa siko tayari kumuacha wife, najua kiasi gani ninavyompenda, i believe she loves me, na she respects me sana, anaihandle family yangu vizuri na mtoto also family businesses.

Ninachoomba kujua ni kuwa nitafanya vipi ili aachane na jamaa, huu ndio mtihani mkubwa kwani it seems wife ni sex addicts kwa jamaa, mwezi huu ana likizo ya kwenda kwao, na jajamaa yuko the same town wife ndiyo kwao, je nimzuie asiende?... niko njia panda.. sijamuambia wife chochote na hajanotice chochote kuwa najua nini kinaendelea.. thanks guys kwa time yenu, nitashukuru kupata ushauri wenu.. Na ninaahidi kuufanyia kazi.

NOTE:KULINDA HESHIMA YANGU, KAZI YANGU I HAD TO COME WITH THIS ID
Pole sana mkuu,suala lako ni zito sana,tafuta wazee wa busara wakwe zako na mkeo mlizungumze na kulitafakari kwa undani. Ila ningekuwa Mimi talaka ndio suluhu
 
Honestly ni ufala sana. Wife aliteswa sana baada ya kugundua jamaa anamcheat na kumdump, the moment naanza naye relation alikua ameugua sana baada ya maumivu ya kulia sana takribani wiki nzima alilazwa....i saved her from that situation....i used a lot of money kumrudisha katika hali ya kawaida. Leo the guy aliyemtesa ndio ananicheat naye..... i never cried lakini wa mara ya kwanza
Hakukupenda ila alikubali kuolewa na wew ili amkomeshe jamaa, ile ilikuwa ni hasira na si upendo.. Pia yawezekana alikubali kuolewa na wew sababu ya kukuonea huruma kwa uliyomfanyia
 
Hakuna mahusiano yoyote yale yaliyodumu yakawa hayana historia. Kila mwanaume anaweza kumshawishi msichana atakapa anachokihitaji,but when a girl's sense comes back, sio wako tena

Vijana tengenezeni strong bond kwenye mahusiano kiasi kwamba mtu akitaka kukuacha akikumbuka gharama ya mahusiano yenu na mliyopitia anaacha wazo Hilo mara moja.

Sasa huyu jamaa yetu anasubiri eti watu wagombane ndio aoe, anajua kabisa msichana alimuacha jamaa Kwa sababu alimsaliti,yeye naye akaamua kumsaliti halafu anasema hayuko tayari kumpoteza. Huu unaweza kuwa ni utani zaidi ya unaofanywa na serikali ya jiwe
Point. Kaenda kufanya aliyofanya mwenzie mwanzon..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom