Croatia Kolinda Grabar-Kitarović: Hakuna namna tunaweza kumualika Rais huyu mrembo akaja kutung'arishia vivutio vyetu?

Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwani hakuna namna tunaweza kumualika na kumshawishi Rais huyu mrembo na mchangamfu (Kolinda Grabar-Kitarović) kutoka katika nchi ndogo ya Croatia akaja kutung'arishia vivutio vya Tanzania yetu?

View attachment 1626834

Inasemekana kwamba huyu mama si Rais tena wa Croatia alistaafu 18 February 2020. Sasa hatuoni kwamba kumshawishi Rais mstaafu ni rahisi zaidi kuliko ambavyo kama angekuwa bado yupo madarakani, na ukizingatia Croatia ni nchi ndogo sana katika siasa za dunia?

MWEZI JULY MWAKA 2018: Rais wa Uswisi Mhe. Alain Berset akizungumza na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya wiki mbili akiwa na familia yake nchini Tanzania. Kwa wiki mbili alizokaa nchini rais Alain amefanya ziara binafsi katika mbuga za wanyama Serengeti na kutembelea visiwani Zanzibar

View attachment 1626828

World Cup ilimalizika na moja kati ya mambo yaliyovuta hisia za wengi ni Rais wa Croatia Mwanamama Kolinda Grabar. Wengi tumezoea kuona Rais akilindwa na walinzi lukuki lakini hali ni tofauti kwa Mwanamama Kolinda.

Baadhi ya Picha zake pia zimezua utata mwingi hata kuna video zikimuonyesha akiwakumbatia mashujaa wa Croatia walioloa jasho baada ya mechi kumalizika wengi wanajiuliza inawezekana vipi kwa Rais huyu Mwanamama kufanya yote haya?

View attachment 1626843

Kolinda Grabar mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Croatia kwa muda mrefu sana amefanya historia yake ya uongozi kukumbukwa zaidi katika World Cup ya mwaka 2018 zilizofanyika nchi Russia.

Swali la Msingi: Je, tunaweza ama hatuwezi?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kwa namna hiyo unawezaje ukamnyima kura, hana haja ya kuiba kura mwenyewe utaipeleka.
 
Ila km tunaye balozi ktk nchi ya Croatia (sidhani) au ukanda huo haswa Russia afanye mchakato wa kidiplomasia atafanikiiwa kumleta tu ila mabalozi wetu wapowapo tu kula kodi zetu, mambo km haya ndo inatakiwa watuletee watalii kwa njia km hizo.
Mabalozi wazidi kukazana katika kutuletea world-class celebrities huku Tanzania...
 
Njia ya mabalozi kutafuta watu maarufu ktk nchi wanazotuwakilisha ndo njia rahisi na ya haraka ya kuutangaza nchi yetu huko nje, ila wao wanataka sijui rahisi ndiye aseme kila kitu ndipo nao waanze kujipendekeza kwake badala ya kuwa wabunifu binafsi.

Mabalozi changamkieni tutangaza vivutio vyetu na mlete watalii msibaki kubugia kodi zetu huko ughahibuni.
Ipo siku Tanzania itafanikiwa zaidi ya hapa
 
Back
Top Bottom