Criticism kwa jk after 5 yrs | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Criticism kwa jk after 5 yrs

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtazamaji, Oct 30, 2010.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  baada ya miaka mitano nawasilisha summary of some critical view zangu kwa Utawala/ Uongozi wa JK.
  NB
  Naomba Nieleweke kama rais anayemaliza lazima kuwe na critics hata angekuwa ni Nyerere, Obama, Mandela au hata Dr slaa . Kwa hiyo natarajia hata wale wanaomfagilia wataacha ushabiki.


  1. JKCCM chairman ana tatizo la kuuma na kupuliza. Hana msimamo.
  Jk Ni mwenyekiti wa CCM. Mwenyekiti wa chama na watu wake wa karibu wamepewa mdaraka na nguvu kikatiba(ya chama) kufanya baadhi ya maauzi kwa maslahi ya chama.

  CRITIC:Kwa nini CCM ilimtoa Bashe na mwakalebela kugombea ubunge bila vyombo husika kuthibitisha wana kosa lakini wakashindwa kufanya hivyo kwa watu wenye tuhuma nzito zaidi kama Chenge na Mramba?

  Serikali iliyowapeleka mahakamani Chenge na Mramba ni ya JK. ina maana mpaka serikali ya JK imewashataki imejiridhisha kuwa wana hatia. sasa kwa nini Chama kistumie rungu na uwezo wake kuonyesha JK na chama chake sio COMEDIAN
  2. JK kama Baba wa familia ya rais . Hawezi kucontrol
  Kama baba wa familia na rais JK aanatikiwa kuja familia yake inapata stahiki mbali mbali halali nyingi tu. Lakini alitakiwa ajue kuna baadhi ya faida zinakwenda na hasara.JK alitakiwa kutumia busara kuweka control kwa familia yake wasiibuke ghafla kisiasa ikiwezekana kuwaminya kisiasa akiwa madarakani. Binafsi naona ameshindwa ku control familia yake. Kwa nini asiwaambie washughulike na faida zilizopo mbele yao za mambo nyuma ya pazia i.e nje ya siasa. Huku kwenye siasa waje baadae???
  3. Jk kama rais wa watanzania.kashindwa kutekeleza ahadi
  Matumaini makubwa waliyokuwa nayo watanzaia wengi juu yake miaka mitano iliypita yamepotea kama mvuke. naamini ile kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtannzania hata yeye mwenyewe anaogpa na anaona aibu kuitamka.

  Uchumi: Nina hakika yale madeni yote iliyolipa serikali ya mkapa yamekuwa negated. Wananchi juzi juzi kwenye bajeti walidanganywa kuwa bajeti yetu inajitegema kwa 40% lakini ukweli ni kuwa wahisani waligoma kutoa misaada Serikali ikakimbilia Kukopa. Iweje Norway agome kukupa msaada sababu ya ufisadi uende kukpa kwa libya useme umejitegemea????

  Mgao wa umeme
  : kwa miaka mitatu mfululizo kwenye hotuba zake anasema ni Changamoto. Changamoto gani inashindwa kukabiliwa miaka mitatu mfululizo.Mgao wa umeme Sio mafuriko, au tetemeko la ardhi.linakuja ghafla.Wasomi wa kitengo cha Sera na mipango wanafanya kazi gani?

  4.JK kama rafiki wa watu- hawa ndo wanaomchimbia kaburi

  Binafsi naona JK alikuwa ceremonial leader. Alitakiwa kutafuta wachapa kazi hasa ili nyota yake izidi kupanda lakini marafiki na washkaji aliwaweka karibu yake kumsaidia hawafanyi kazi yao

  Sikatai lazima uchague watu unaowajua lakini lazima kuwe na clear line between kazi na urafiki sijui kama JK na Lowasa walikuwa wakikutana ofisini wanatofautisha mazungumzo ya Kikazi na kirafiki. His/ Her friend and close allies wameshindwa ku cover hata zile weakness zake.Hawafai


  Sijui wanajamvi mna mawazo gani?
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hapo chacha ndo pagumu! Jamaa kununuliwa na MAFISADI haaa nchi hii bwana!
  Halafu kweny mahojiano yake ya jana anasema waTZ tumkumbuke kwa kututoa hapa na kutupeleka pale! yaani uchumi umekuwa saana tofauti na kipindi cha Mkapa! sasa kweli hii ni haki! hana hata kwa kujisifia!
   
Loading...