Critical Thinkers tusaidiane, ahadi hii ya Lowassa ilikuwa geresha?

mossad 03

JF-Expert Member
May 15, 2013
523
439
Wakuu,

Wakati akihamia na akipokelewa rasmi CHADEMA/ UKAWA mheshimiwa Lowassa alitoa kauli kama tatu hivi kuhusu uchaguzi huu,,,,among others Lowassa aliwaambia wana UKAWA/wapiga kura wake kuwa wapige/wampigie kura then walinde za ngazi za chini lakini kura zote za urais wamwachie atalinda yeye mwenyewe.Aliongea kauli hiyo kwa kujiamini na kwa msisitizo mkubwa na kutoa picha kuwa anakijua anachokiongea.

Lakini siku za karibuni viongozi wakuu wa CHADEMA hasa mwenyekiti Freeman Mbowe amekuwa akishutumu mamlaka halali kama vile tume ya uchaguzi,usalama wa taifa na hata TPDFkuwa wamejiandaa kufanya uhuni kwenye uchaguzi huu HASA URAIS.

Mbowe kaongea mambo mengi sana akielekeza shutuma zake kwa viongozi waandamizi wa taasisi hizi kila apatapo nafasi ya kuongea kwenye majukwaa mbalimbali kwa takrinani mwezi mmoja sasa.Tundu Lissu na viongozi wengine wameonyesha hofu zao pia.

Lakini kubwa kuliko yote ni viongozi wa UKAWA hasa CHADEMA kuendelea kusisitiza wafuasi wao kulinda kura kwa uwezo wao wote na kura inayoleta mashaka zaidi obvious ni kura ya urais, hili limepelekea mgogoro wa mita 200 toka kituoni na kesi iko mahakamani.Hilo limeibuka as a result of issue ya ulinzi wa kura.

Hivi viongozi wa CHADEMA hawakusikia ahadi hii ya Lowassa?its obvious waliisikia sasa kipi kinawafanya wawe na wasiwasi kuhusu kutangazwa washindi na kukabidhiwa ikulu kama wakishinda wakati mgombea wao aliwaahidi kuwa kura za uraisi wasihangaike wamuachie yeye mwenyewe atazilinda?

Hawamuamini mgombea wao?

Kama kashindwa kutimiza ahadi hii moja aliyoahidi juzi juzi tu around July na kupelekea wapiga kura wake kuwa kwenye hatari wakati wakilinda kura zake ataweza kutimiza ahadi zake lukuki anazoendelea kuahidi kila siku kwenye campaign zake?

Je, inawezekana ata hizi anazoahidi kwenye kampeni ni geresha tu ili ashinde uchaguzi then hazitatimizwa?

Karibuni kwa mjadala na hoja wakuu
 
Any way, So what do you want us to tell you? Keep on lamenting!
 
Siku zote ukitala kumsoma mtu vizuri tafuta marafiki zake utajua tabia yake ikoje sasa lwasa best yake alikiwa kkwte aina ya tabia yao ni.maneno mazuuri ambayo hushindwa kutekeleza na pia mtu muhimu kwetu ni mtendaji weka kazi za Lowasa na Magufuli halaf uone nani mtendaji utjua tu Magufuli is active in action.
 
Duh! Akili yako iko static na unataka kila kitu kiwe static na kila mtu awe hivyo unavyotaka, Impossible! Unapaswa kupata Elimu,Elimu,Elimu!
 
Duh! Akili yako iko static na unataka kila kitu kiwe static na kila mtu awe hivyo unavyotaka, Impossible! Unapaswa kupata Elimu,Elimu,Elimu!

Lendeyson
Mimi napima ahadi za mgombea na utelekezaji wake,,,akili yangu iko static vipi?
 
Mkuu, nimecheka sana,
siyo kwamba kasahau....maji yamezidi unga, hata ushauri wa yule IPP Boss, umeshindikana.
(rejea BBC enterview)
Na vipi ile ahadi ya kuja chadema na mawaziri 62, ma-DC 126, wabunge 82 !!!
ha ha ha ha haaaaa!
 
Duh! Akili yako iko static na unataka kila kitu kiwe static na kila mtu awe hivyo unavyotaka, Impossible! Unapaswa kupata Elimu,Elimu,Elimu!

Mkuu huyu ndugu kauliza maswali mengi tu kwenye huu uzi...wewe badala ya kumjibu maswali yake unaanza kuiponda akili yake...tulia na ufikiri vizuri utaona kati ya ww na yeye nani akili yake haiko sawa
 
Mkuu, mojawapo ya sababu ni mabadiliko ya rejareja yaliyofanywa mara kadhaa kwa wajumbe(?) wa tume ya uchaguzi. Huo mchezo hata mtoto mdogo angeushtukia.
 
Mkuu, nimecheka sana,
siyo kwamba kasahau....maji yamezidi unga, hata ushauri wa yule IPP Boss, umeshindikana.
(rejea BBC enterview)
Na vipi ile ahadi ya kuja chadema na mawaziri 62, ma-DC 126, wabunge 82 !!!
ha ha ha ha haaaaa!

Kwenye enterview ya BBC, Watanzania ndio tumejua Lowassa ni pumba kabisa!
 
Mkuu huyu ndugu kauliza maswali mengi tu kwenye huu uzi...wewe badala ya kumjibu maswali yake unaanza kuiponda akili yake...tulia na ufikiri vizuri utaona kati ya ww na yeye nani akili yake haiko sawa

Mkuu
Siasa za wapinzani hivi karibuni zinasikitisha sana,,,hawatoi na wala hawataki tena majadiliano ya hoja,,wao wanachojua ni kushambulia kwa matusi tuh,,,ccm ni chama kilichochoka na kinatumia mbinu zisizokubalika lakini kwa hivi karibuni upinzani nao wameadapt mbinu hizo hizo za ccm,,,wapinzani wameshindwa kujipambanua kama mbadala sahihi,,ndiyo mana kunakua na kundi kubwa la watu ambao wameichoka ccm lakini wakiuangalia upinzani in and out wanaona ni bora waweke hopes kwa magufuli na wakomae na hiki hiki chama tawala
 
Pole pole alishawaambia uchaguzi ukiwa huru na wazi,ccm wajiandae kukabidhi nchi,sasa viashiria vingi vimeonesha kwamba kutakuwa na uvunjivu wa maana
 
Mkuu, mojawapo ya sababu ni mabadiliko ya rejareja yaliyofanywa mara kadhaa kwa wajumbe(?) wa tume ya uchaguzi. Huo mchezo hata mtoto mdogo angeushtukia.

Hoja yako iko sahihi kwa upande fulani,lakini hiyo inanipa wasiwasi zaidi juu ya mgombea wetu huyu wa ukawa ,,kwanza inawezekana alikua na watu aliokua connected nao kama yule mkurugenzi wa uchaguzi aliebadilishwa thats y akajiamini,,lakini kubadilishwa kwa some officers wa tume ndo sababu pekee ya yeye kushindwa kutimiza alichowaahidi wapiga kura wake,?ina maana alikua na option hiyo hiyo moja?kwamba baada ya hiyo changamoto ndo ipelekee kukabidhi role ya kulinda kura kwa wapiga kura wake ambao aliwaahidi with a straight statement kuwa atalinda kura za uraisi yeye mwenyewe bila kuweka japo neno la kuonyesha kuwa kauli yake inategemeana na conditions fulani???

kama ni ndiyo basi hafai kabisa kuwa kiongozi wa nchi,,nakwambia hivi kwa sababu inawezekana kama kiongozi huyu akiapishwa na kuwa raisi na anakutana na changamoto katika kutimiza ahadi zake lukuki alizo ahidi(uraisi una changamoto kuliko tunavyoweza kufikiria) atabaki kusubiri kuja kutuambia baada ya miaka mitano kuwa "nimeshindwa kuteleleza ahadi zangu kwa sababu hii na hii" kitu ambayo sisi watanzania hatukitaki tena,,kama ambavyo umejionea watu hawataki kusikia tena idadi na hesabu za megawati na hata kulisikia neno "megawati" bali wanataka umeme wa uhakika uwake nchini
 
Lendeyson
Mimi napima ahadi za mgombea na utelekezaji wake,,,akili yangu iko static vipi?


Unajua Maana ya ahadi? Issue ya kulinda Kura tangu lini ikawa ahadi? Mbona unalazimisha hoja? Huna hoja hapo mkuu!
 
UMETOA MAELEZO mAREFU SANA, LAKINI SIJANA SEHEMU ULIPO ANDIKA KUWA LOWASA ALIUKANA USEMI WAKE, SASA SIJAJUA ULITAKA KUMAANISHA NINI KATIKA HIY POST YAKO.

YEYE ALISEMA NENDENI MKAPIGE KURA, KUHUSU NANI AATANGAZWA RAISI NIACHIENI MIMI.

CCM MUSIPENDE KUTUMIA AKILI ZA KUAZIMA MTAFIA KWENYE MAKABURI YASIYO YAKWENU. KHAAA MBONA MNATUMIA MUDA MWINGI KUMDISCUSS MTUMISHI HUYU KWANI AMEWAKABA KOONI AMA?
 
wakuu,

wakati akihamia na akipokelewa rasmi chadema/ ukawa mheshimiwa lowassa alitoa kauli kama tatu hivi kuhusu uchaguzi huu,,,,among others lowassa aliwaambia wana ukawa/wapiga kura wake kuwa wapige/wampigie kura then walinde za ngazi za chini lakini kura zote za uraisi wamwachie atalinda yeye mwenyewe,,,aliongea kauli hiyo kwa kujiamini na kwa msisitizo mkubwa na kutoa picha kuwa anakijua anachokiongea,

lakini siku za karibuni viongozi wakuu wa chadema hasa mwenyekiti freeman mbowe amekuwa akishutumu mamlaka halali kama vile tume ya uchaguzi,usalama wa taifa na hata tpdf kuwa wamejiandaa kufanya uhuni kwenye uchaguzi huu hasa urais,,mbowe kaongea mambo mengi sana akielekeza shutuma zake kwa viongozi waandamizi wa taasisi hizi kila apatapo nafasi ya kuongea kwenye majukwaa mbalimbali kwa takrinani mwezi mmoja sasa,,tundu lissu na viongozi wengine wameonyesha hofu zao pia

lakini kubwa kuliko yote ni viongozi wa ukawa hasa chadema kuendelea kusisitiza wafuasi wao kulinda kura kwa uwezo wao wote,,,na kura inayoleta mashaka zaidi obvious ni kura ya uraisi,,hili limepelekea mgogoro wa mita 200 toka kituoni na kesi iko mahakamani,,hilo limeibuka as a result of issue ya ulinzi wa kura,,,

hivi viongozi wa chadema hawakusikia ahadi hii ya lowassa?its obvious waliisikia sasa kipi kinawafanya wawe na wasiwasi kuhusu kutangazwa washindi na kukabidhiwa ikulu kama wakishinda wakati mgombea wao aliwaahidi kuwa kura za uraisi wasihangaike wamuachie yeye mwenyewe atazilinda?

Hawamuamini mgombea wao?

Kama kashindwa kutimiza ahadi hii moja aliyoahidi juzi juzi tu around july na kupelekea wapigakura wake kuwa kwenye hatari wakati wakilinda kura zake ataweza kutimiza ahadi zake lukuki anazoendelea kuahidi kila siku kwenye campaign zake?

Je inawezekana ata hizi anazoahidi kwenye kampeni ni geresha tuh ili ashinde uchaguzi then hazitatimizwa?

Karibuni kwa mjadala na hoja wakuu

kama chama tawala wanalalamika hivi where are we going.
Hivi wewe uko home unasubiria ada, halafu baba yako anarudi analalama, kama kijana unafanya nini, kama sio kumwambia abakie nyumbani ili wewe ukatafute?
 
Back
Top Bottom