Cristiano Ronaldo kuukosa mchezo wa Manchester Derby, United wapata presha

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Manchester United inatarajiwa kumkosa mshambuliaji wake mkongwe, Cristiano Ronaldo katika mchezo dhidi ya Manchester City, leo Jumapili Machi 6, 2022 kutokana na kuwa majeruhi.

Hizo ni taarifa mbaya kwa United kwa kuwa mchezo huo ni muhimu kwao dhidi ya City ambayo inaonekana kuwa vizuri kuliko United.

Straika mwingine mkongwe wa United, Edinson Cavani inaelezwa naye hayumo katika mipang ya Kocha Ralf Rangnick.

Kwa mana hiyo United inaweza kumtegemea Marcus Rashford kusimama kama mshambuliaji wa kati.

Taarifa hizo zimewapa presha mashabiki wa United kwa kuwa wanajua timu yao haipo katika kiwango kizuri, hivyo kumkosa Ronaldo inawezekana kukaongeza nguvu kwa City katika mchezo huo wa Premier League.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom