Cristiano Ronaldo kuhamia Manchester City

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,906
25,180
20210824_212553.jpg
Habari zinazozunguka mtandaoni hivi sasa ni kwamba mshambuliaji mahiri wa ureno na klabu ya Juventus anaweza kuhamia klabu ya Manchester City kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili nchini Uingereza.

Inasemekana wakala wa mshambuliaji huyo Jorge Mendes anajaribu kuangalia uwezekano wa kufanya uhamisho huo unaotarajiwa kuchukuliwa vibaya na Manchester United ambao ni mahasimu wa klabu ya Man City.
 
Man City sio hasimu wa Manchester United ni mpinzani wa jiji moja. Liverpool ndio hasimu wa Man United
 
Maana ya hasimu ni nini ?
Adui yako. Mpinzani wako ni mtu unayeweza kaa nae meza moja mkayapanga. Zinedine Zidane hawezi kuinoa Barcelona na Pep Guardiola hawezi kuinoa Real Madrid kwa sababu timu zao ni mahasimu sio pinzani.

Unakumbuka kilichomtokea Luis Figo alipoihama Barcelona kwenda Real Madrid? Steven Gerrard alikuwa anahusishwa na ukocha Everton alisema mashabiki wa Liverpool wananiua kwa sababu hizo ni timu hasimu sio pinzani.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom