CRDB wang'ang'ania mishahara ya watu ya mwezi mei hadi leo

Mateso

JF-Expert Member
Aug 6, 2008
259
19
Wajameni ni jambo la kushangaza na kwa upande mwingine kusikitisha.

Nashindwa kuelewa kama CRDB wamechoka wateja au wametosheka na kipato hivyo kutokujali tena wateja wao. Amini usiamini mpaka leo hii tarehe 7.6.10 kuna watu wengi sana ambao mishahara yao inapitia CRDB hawajapata mishahara yao. Nashindwa kuelewa tatizo ni nini.

Nadhani wakati umefika sasa wa wafanyakazi wote wa umma na mashirika ya umma kupitishia mishahara yao NMB kwa kuwa wanaopoitishia huko huwa wakichelewa kuvuta mshiko wao sana sana huwa ni tarehe 28 ya kila mwezi.

Nashauri waathirika wa tukio hili kuhama CRDB iwapo tatizo hili litarudia tena kwa mwezi June. Hatuwezi kuona watu wanahaha huku na huku kukopa wakati pesa zao zimekaliwa na wazembe fulani kwa kisichojulikana.
 
Mkuu inawezekana una point ila unatakiwa kuchukua hadhari kuwaambia watu wahamie specific bank wakati Tanzania kuna mabank mengi tu. Unapofanya hivyo una sound kama NMB marketing manager.

Ni kweli CRDB wana matatizo yao moja wapo ni kucharge commissions zisizokuwa na maelezo ya kutosha. Ila waache watu waamue wenyewe kama wanaridhika na huduma au la kwani soko huria litafanya kazi.
 
Nashindwa kuelewa kama CRDB wamechoka wateja au wametosheka na kipato hivyo kutokujali tena wateja wao. Amini usiamini mpaka leo hii tarehe 7.6.10 kuna watu wengi sana ambao mishahara yao inapitia CRDB hawajapata mishahara yao. Nashindwa kuelewa tatizo ni nini.

Nadhani wakati umefika sasa wa wafanyakazi wote wa umma na mashirika ya umma kupitishia mishahara yao NMB kwa kuwa wanaopoitishia huko huwa wakichelewa kuvuta mshiko wao sana sana huwa ni tarehe 28 ya kila mwezi.

Nashauri waathirika wa tukio hili kuhama CRDB iwapo tatizo hili litarudia tena kwa mwezi June. Hatuwezi kuona watu wanahaha huku na huku kukopa wakati pesa zao zimekaliwa na wazembe fulani kwa kisichojulikana.
Peleka malalamiko yako kupitia anwani hii
CRDB Bank PLC
Makao Makuu: Azikiwe Street
P.O. Box 268 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2117442-7 Faxi: 255 22 2116714
Barua Pepe: customer-hotline@crdbbank.com
Tovuti: CRDB Bank Tanzania

Mkurugenzi wa Marketing & Research
dmr@crdbbank.com
Mkurugenzi wa Alternative Channels Banking
dabc@crdbbank.com

Ukishindwa kuhudumiwa niambie nitakupa namba ya Kimei, angalia usitumie jukwaa hili kupromote benki zingine tena zilizo na harufu ya kununuliwa/kuanzishwa KIFISADI
 
Mto mada hafanyi promotion, ametaja NMB kwa sababu mishahara ya watumishi wote wa umma huwa inapitia NMB kabla ya kwenda benki nyingine.Hivyo hakuna benki nyingine ambayo itaweza kuanza kuweka mishahara ya watumishi wa umma kabla ya NMB.
 
Mimi ni mtumishi wa umma nina account CRDB ,ni kweli mishahara inachelewa lkn siwezi kuacha kupitishia mshahara CRDB kwasababu ni nje ya nchi mali naTZ lakini naweza pesa yangu kupitia visa Card ya crdb lakini NMB hawana kadi za ATM unazoweza kutumia nje ya TZ. hata kuna benki nyingine huko bongo zina Visa cards au master cards ambazo ukitoka nje ya tz huwezi tumia
 
Lengo langu siyo watu wafunge akaunti zao bali wasipitishie mishahara yao huko CRDB iwapo CRDB hawatachukua hatua za haja mwezi huu Juni. Mimi mwenyewe nitahamisha mshaahara lakini akaunti sitafunga.
 
Waungwana kuchelewa kwa mishahara inawezekana ni uzembe wa watumishi wa benki lakini pia inawezekana serikali haina pesa.

Kumbukeni serikali sasa hivi inatafuta mikopo katika mabenki sasa inawezekana cheki ya mishahara ya wafanyakazi haijaletwa CRDB na hivyo na wao hawawezi kuwapeni pesa.

Ninachokushauri nenda katika branch husika uwaulize kistaarabu kitu gani kinachoendelea wakikwambia bado hawajapewa ruhusa kupost ujue ndio hivyo idara husika haina kitu hivyo wanasubiri mpaka pesa ziingizwe ndio na nyie mpate mshiko
 
Kuna wengine wamenielewa vizuri lakini wengine wamenielewa tofauti. Mie siyo marketing manager wala mfanyakazi wa benki hiyo wala sina akaunti huko. Lengo langu ni kuwarekebisha hawa CRDB ndo maana nikashauri kwamba iwapo mwezi huu watachelewesha tena watu wahamishie mishahara yao NMB kwani kule wakichelewa sana ni tarehe 28 @ mwezi. Wadau wengi wanalijua hilo.:A S tongue:
 
Mto mada hafanyi promotion, ametaja NMB kwa sababu mishahara ya watumishi wote wa umma huwa inapitia NMB kabla ya kwenda benki nyingine.Hivyo hakuna benki nyingine ambayo itaweza kuanza kuweka mishahara ya watumishi wa umma kabla ya NMB.

You don't have full information you better say "I don't know". Kama wewe ni mwalimu huenda ukawa na ukweli kidogo but Mshahara wa wafanyakazi wa umma kupitia NMB kwanza kabla ya kwenda Bank yoyote is false, false,false, untrue. Is NMB a Treasury?
 
Kwani hamjui maana ya biashara/soko huria? Acha soko liamue tu, wenyewe watanyooka kama huamini utaona tu. Kwani kina Greenland bank wako wapi sasa hivi, hamusikii wengine wanatoa mastercard bure na bado!! hata simu walikuwa hivihivi, huoni sasa hivi walivyonyooka, wenyewe wanabembeleza hadi line za bure na zawadi juu, aagh!!
 
Mtoa maada umecheki na mwajiri wako kama alipeleka cheque ya mshahara wako kwa wakati? mimi napitishia mshahara wangu CRDB na hawawahi kunicheleweshea mshahara, mara nyingi napata tarehe 26 (+ or - a 2 days). Na hali hii ni kwa miaka 7 iliyopita
 
1.BENKI ZOTE INAFIKA MAHALA WANAJISAHAU HADI WAKIONA WATU WANAFUNGA ACCOUNT KA WINGI.
2.KUNA WAKATI HAWA CRDB WALIKUWA WANAONGOZA.KWA HUDUMA BORA....SASA HIVI NI MATATIZO.
3.ACHILIA MBALI KUCHELEWESHEWA MISHAHARA,PIA HATA TRANSACTION ZA AJABU AJABU UNAKUTA UMEKUWA DEBITED.
4.INASHANGAZA ACCOUNT YAKO INA CREDIT BALANCE,UKIWEKA PESA BALANCE HAIONGEZEKI SAMBAMBA NA AMOUNT DEPOSITED.
5.HII NI BENKI NZURI LAKINI NADHANI NA KUNA UVUMI KUWA TAYARI KUNA WAFANYAKAZI WAJANJA WACHACHE WAMEIVAMIA.HAO JAMAA HUTOKA BENKI HII NA KUINGIA NYINGINE KWA KUAJIRIWA. UKIAJIRI KIKUNDI HICHO KWENYE BENKI YAKO ANDIKA UMEUMIA.
6.KWA WENYE MIKOPO USISIKIE,DEBITS ZINAZOINGIZWA HAPO..Mhhhhhh.UKIULIZA Aaaaah chap chap unarejeshewa pesa yako USIPOULIZA/GUNDUA JE?
7.LABDA TUTUMIE LUGHA YA KIUHASIBU ZAIDI.......ACCOUNT IKISHAKUWA DEBITED......INATAFUTWA ACCOUNT NYINGINE IWE CREDITED..
HAPO HESABU ZINABALANCE....LAKINI MTEJA UMEUMIA.
8.KWENYE MAIL ORDER USISIKIE...KABLA HUJAJIUNGA WAFANYAKAZI WENYEWE WANAKUONEA HURUMA....WANAJUA UTALIZWA TU.
9.BENKI ZINGINE KUBWA YAPO MATATIZO KAMA HAYA.CRDB INA NAFUU WALA SIMSHAURI MTU AHAME....ILA NASHAURI
1.MTEJA KAGUA ACCOUNT YAKO MARA KWA MARA UKITUMIA NYARAKA ULIZOINGIZIA PESA NA ZILE ULIZOTOA.JE ZINAOANA?
2.CRDB JIREKEBISHENI BANA? WENZENU WACHACHE WATAHARIBU SIFA NZURI YA BENKI.....WAFICHUENI (KAMA WAPO)
3.KAMA MASILAHI NI MADOGO SI WAELEZENI TU AKINA KIMEI WAWAONGEZENI MISHAHARA?
 
Kuna wengine wamenielewa vizuri lakini wengine wamenielewa tofauti. Mie siyo marketing manager wala mfanyakazi wa benki hiyo wala sina akaunti huko. Lengo langu ni kuwarekebisha hawa CRDB ndo maana nikashauri kwamba iwapo mwezi huu watachelewesha tena watu wahamishie mishahara yao NMB kwani kule wakichelewa sana ni tarehe 28 @ mwezi. Wadau wengi wanalijua hilo.:A S tongue:

Hilo lengo lako ni Mission Impossible. CRDB Bank wameshiba sana pesa. Hawajali kabisa wateja wao. Mimi nilikua na account pale Vijana Branch karibia miaka 10. Customer service yao kwa kweli ilikua zero. Kila mara makosa ya kizembe na hakuna ku apologise kwa mteja. Yaani take it or leave it.

So one day, when I had had enough, I left. Na barua yangu ya kufunga account ilieleza kabisa kwamba nahama benki maana huduma kwa wateja wao ni mbaya. I don't think they cared then or now.

Ushauri wangu? We nenda kafungue account benki nyingine. Mbona mabenki yako mengi tu?
 
Back
Top Bottom