Igande
Member
- Jun 10, 2021
- 41
- 60
Habari za wakati huu Great thinkers!
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Ni kawaida kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoa pesa kutoka katika account zao za benki kidogo kidogo.
Huo ndio mwanya wanaotumia CRDB kuwatapeli fedha zao, kivipi?
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS). Mara nyingi, kama ilivyo kwa wanafunzi wengi, natoa pesa kidogo kidogo. Hilo hupunguza hata risk ya kuibiwa, natoa pesa ambayo nina matumizi nayo tu!
Tangu naanza kupokea Boom la kwanza, nilikuwa na wasiwasi kwamba pesa yangu inapungua. Lakini pasipo kufuatilia na pasipo kujua nika'assume' kwamba itakuwa nyingine inaishia kwenye makato!
Lakini ile hali ya kwamba pesa inapungua haikunipa amani kabisa!
Baada ya Boom la mwisho kwa mwaka huu ambapo kwa MUHAS tunapokea Takribani Tsh 665,000/= nikatoa laki 3 kwa ajili ya kulipa madeni na matumizi mengine.
Nilipokuja kutoa tena kiasi cha fedha elfu 50, nikashangaa kuona imebaki 190,000/=!! Hata kama ni Makato yanakuwaje makubwa hivi?
Nikaenda kuwauliza CRDB Kariakoo Branch wakasema hawawezi kunisaidia labda niende kwenye Bank niliyosajilia bank account yangu. Hivyo basi nikaenda Azikiwe branch na baada ya mvutano mrefu mwisho wakaniambia niombe bank statement.
Nikaomba ya June na July, nilichokikuta ndio hicho hapo chini! Hizo sehemu zenye duara ni malipo madogo madogo ambayo sija yafanya na wanadai nimeyafanya.
Ikumbukwe kwamba sijalipia premium kwenye App au sehemu nyingine yoyote na wala sifanyi manunuzi ya mtandaoni.
Itoshe kusema kwamba, CRDB ni wezi! Na huenda ikawa wanaibia wengi kwa staili hii hii bila wao wenyewe kujua. Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba wanafunzi wengi sio wafuatiliaji.
Na je, hivi ni kweli hizi Tembo card zinaweza kutumika kwenye kulipia malipo ya mtandaoni? (iTunes)
Nimelileta hili jukwaani, ili watu walitambue. Binafsi nitaangalia namna ya kuwahama japo ni process ndefu kwa mujibu wa taarifa nilizopewa. Lakini je, huko kwingine vipi?
Inauma sana!