SaaMbovu
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 6,027
- 5,343
Habari zenu wana JF.
Jana nimefanya transaction kwa kutumia SIM BANKING na line ya simu ninayo itumia ni Airtel. Pesa niliitoa kwenda namba ya Vodacom na ilikuwa muda wa saa moja na nusu jioni.
Cha kushangaza mpaka sasa pesa yangu imetoka lakini haijaingia kwenye line ya M Pesa ya mtu niliyokuwa namtumia.. nimepiga namba ya huduma kwa wateja naambiwa hela yako itaenda tu nisubiri ni mtandao unasumbua.. lakini suala la ajabu ni kwamba baadae nilijaribu kutuma kiasi kidogo sana cha pesa kwa yule yule mtu ikafika bila shida.
Sasa najiuliza kama shida ni mtandao imekuwaje hiyo ndogo imeenda na nyingine bado. Pia nimeenda Bank nikaambiwa hela imetoka lakini bado haijaingia kwenye line ya M Pesa niliyotuma kwamba nisubiri.
Nikaomba kama bado haijaenda basi irejeshwe kwenye account yangu naambiwa haiwezekani hiyo ni hatua ya mwisho.
Jamani kuna mdau humu amewahi kukutana na kesi kama hiyo na kama amewahi vipi alifanikiwa kupata hela yake na alitumia process zipi.
Msaada tafadhali maana business imelala sasa na kuna mtu kaniambia yeye aliwahi kupata hasara ya 800k mpaka leo hajarejeshewa na ni zaidi ya mwaka sasa.