CRDB Tawi la Usa-River kwanini mnakaa na mishahara ya watu bila kuiingiza kwenye akaunti za wahusika?

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,127
6,130
Hii benki ya CRDB imekuwa na unyanyasaji kwa wateja wake. Kuna hili tawi lao la Usa-River lililoko wilaya ya Arumeru Halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani Arusha kuna taasisi zinapitishia mishahara ya wafanyakazi wao kupitia hili tawi. Tatizo wafanyakazi wa hili tawi hukaa na mishahara ya wahusika hata kwa siku 3 bila kujua sababu ni nini. Je ni kwamba kuna deal wanafanya na wahasibu wa taasisi husika au kuna mchezo gani unaendelea, je ni uzembe?

Wamekuwa wakifanya hivi kwa muda mrefu, kwa mfano tangia jana Ijumaa kuna mishahara imepelekwa benki ya CRDB kupitia hili tawi lakini mpaka muda huu haijaingizwa kwenye akaunti za wahusika. Wanataka wakae nazo mpaka Jumatatu, swali ni kwanini mnanyanyase watu kwa ajili ya pesa zao? Kwanini mtu asifanye shopping au shughuli zake hii weekend? Huu ni ujambazi, uonevu, unyanyasaji na ukatili wa hali ya juu. Uongozi wa ngazi za juu wa benki tunaomba shughulikieni tatizo hili vinginevyo watu waweza kuchukua hatua yoyote wanayoona inafaa
 
Kosa sio la hiyo benk,kosa la hiyo taasisi ,wanatakiwa waharakishe kupeleka check mapema,ili kufidia siku hizo tatu
 
Pole sana mhanga nadhani kuna shida mambo cheque labda lazima iwe cleared....pole sana
 
Hivi bank nzuri ni Hipi nataka kujiunga na Moja wapo au yoyote ni sawa
 
Back
Top Bottom