CRDB Tanzanite imeshidwa USA Kwasababu ya kutokujua Utamaduni wa Watanzania wa huko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CRDB Tanzanite imeshidwa USA Kwasababu ya kutokujua Utamaduni wa Watanzania wa huko

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kamundu, Sep 7, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tanzania kampuni nyingi hazina mafunzo ya kutosha ya biashara na hii ndiyo sababu kampuni nyingi zinakufa.

  Kwa Upande wa CRDB: CRDB wanaamini wamefanya kila kitu kuhamisisha watu wa USA kufungua Account ikiwa ni pamoja na kuanzisha Internet Banking na kuruhusu pesa ya Account iwe kwenye Dollars. CRDB Wamejigamba mbona eti wamefanikiwa sana Botswana.

  Kwa Upande wa Watanzania wa USA: Wanaona CRDB hawafanyi kazi nzuri na wamejaa uzembe na uswahili hivyo hawawezi kufungua account ya Tanzanite ya CRDB.

  Tatizo ni nini hapa? Tatizo ni utamaduni.
  CRDB na Watanzania wengi wamesahau kwamba utamaduni wa Watanzania wa USA sio sawa kabisa na utamaduni wa Watanzania wa Botswana au ambao wako Tanzania. Kwasababu wote ni Watanzania haina maana utamaduni wa kufanya vitu ni sawa mfano: Mtanzania wa USA akiandika email ya kuuliza kitu kwenye account anategemea kujibiwa sio zaidi ya siku mbili lakini CRDB Tanzania wanaweza kuchukua hadi wiki mbili kujibu email. Mfano mwingine Watanzania wa USA hawanashida kama ukiwasiliana nao na kuwaambia mfano kufungua account ni wiki nne lakini kama ukiwaambia ni siku mbili halafu ichukue mwezi mzima wanafunga account. Hivyo inabidi kama unafanya biashara na Watanzania wa USA Uwape muda wa ukweli. Hii sio kwasababu yeyote ya kujifanya nani zaidi lakini ni utamaduni waliozoea wa kufanya shughuli za kila siku za kijamii huku USA. Watanzania wa Botswala wanaelekea kuwajua zaidi kiutamaduni Watanzania wanaoishi nyumbani hivyo hawaweweseki kwa mammbo mengi kama wale wa USA. Kama kuna Watu wanaotaka kufanya biashara na Watanzania wa Diaspora mimi ningeshauri kujifunza utamaduni wao au kuajiri mtu aliyeishi kwenye diaspora.
   
 2. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Maajabu ya ulichokiandika ni kwamba ukiongea na Mmarekani aliyeajiri Mtanzania (huyo ambaye unamwita ana utamaduni wa Marekani) huko Marekani na yeye atalalamika kama wewe unavyolalamika, kwamba anapata shida sana kufanya kazi na Mtanzania kwa maana ya tofauti ya Utamaduni sio mwaminifu hajui kufwata muda, muongo, MVIVU, saa zote anawaza wanawake tu n,k
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ndio kwana wanaanza kuwa international bado wachanga wakitaka mafanikio ya haraka inabidi wajifunze makosa yao haraka sana na kuyarekebisha.
   
 4. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ooh kumbee,tunahama na kauswahili ketu sio?
   
 5. h

  hargeisa JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  swahili banking systin ni ya kishenzi teiller anatoka ktk chumba chake huku mstari mrefu au anapiga simu kwa mpz wake
   
 6. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Nilichomaanisha ni kwamba tunalalamika sana, hakuna jambo jema litakalofanyika bila watu kulaumu, kila kitu kitachambuliwa kuanzia ndani mpaka nje ili mradi tu apate kaupenyo ka kulaumu!
   
 7. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Walikuwa na Agent hapa USA ilibidi ajiuzulu kwani walikuwa wakimwambia account za wateja zimeshafunguliwa na wakituma pesa inarudi kwamba hakuna hata account!. Hivyo jamaa akaanza kuonekana kama anadanganya wateja lakini tatizo lilikuwa ni kwamba CRDB hawakuwa serious. Watanzania wa USA wakishadanganywa mara moja basi. Huwezi kukaa wiki nzima hujajibu email ya kutoka USA unakosa biashara kwani mawasiliano makubwa USA sio simu ni email!.
   
 8. 2015ready

  2015ready JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45


  Well said and well put. Watanzania wengi wanania ya kununua Tanzanite account lakini wanna Shaka sana na destuli za ufanywaji wa benki za Tanzania. Kweli ni watanzania lakini they think like Americans, plan like Americans, and expect the same service like the one on this side of the world (first world). CRDB, please improve your internate services and you will get most of the Tanzanians living in the USA.
   
 9. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Unaweza kuwa hata na mapacha watatu mmoja China, Tanzania na USA kama wamekaa kwenye hizo nchi kwa miaka 10 utamaduni wao wa kufanya vitu hautafanana ni mazingira ya makazi. Hivyo kabla ya kufanya biashara na kundi fulani ni lazima ujue unatakiwa kufanya nini na mazoea ni yapi
   
Loading...