CRDB mikopo kwa Wafanyakazi sector zote riba 14%-16% kiwango maximum 100 milions 1-7yrs

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
24,562
47,010
Habarini za muda huu wakuu,

Ukirejea kwenye kichwa husika, kuna promotion ambayo ime trend sana hivi punde toka CRDB juu ya mikopo inatolewa kwa wafanyakazi wa sector zote binafsi na za umma,kwa riba ya asilimia 14-16 yenye muda kuanzia 1year to 7years hii ni kwa wafanyakazi walioajiriwa wenye mikataba ya kazi ya kudumu, unaweza kopa kuanzia Milion1- Milioni 100.

Swali langu ni kwanini ukienda ofisini kwao maelezo yao yana kinzana na matangazo yao unakutana na mambo tofauti kidogo,hebu tusaidiane kwa yoyote humu ndani aliejaribu kuomba huu mkopo naomba anipe ufafanuzi kidogo kakutana na changamoto zipi.

Vivyo hivyo nasikia NMB wanatoa mkopo kama huo huo kwa wafanyakazi wenye riba 14%-16% miaja7 kuanzia 1m-100m, Je kwa NMB ni lazima mshahara upite kwenye bank yao.

Kati ya CRDB vs NMB wapi kuna unafuu kwenye kupata huu mkopo?

Tusaidiane kimawazo wakuu,tujikwamua tundwe sote kwenye uchumi wa kati
 
Shart l kwanza ukope mshahara lazim upitie bank husika.
Ili upate maelezo ya kina nenda na taarifa au chanzo cha taarifa kama evidence yako msikilize mtoa huduma akimaliza mwambia mbona maelezo tunayopata ktk matangazo yenu ni hivi then atoe maelezo
Wanalinda reputation yao ndiyo shida, maelezo ya kupata mkopo ndani ya masaa 24 huoni ni lugha ya kibiashara,

Pia kwenye kurasa zao kuna mdau analalamika yeye ni ameenda offisini kwao na mwajiriwa ila sector binafsi akaambiwa offisini kwenu mpo wachache na yupo kazini ndani miaka zaidi ya 7, ila kwakuwa offisi yao wako wachache bank haiwezi kumpa mkopo.
 
Wanalinda reputation yao ndiyo shida, maelezo ya kupata mkopo ndani ya masaa 24 huoni ni lugha ya kibiashara, pia kwenye kurasa zao kuna mdau analalamika yeye ni ameenda offisini kwao na mwajiriwa ila sector binafsi akaambiwa offisini kwenye mpo wachache na yupo kazini ndani miaka zaidi ya 7, ila kwakuwa offisi yao wako wachache bank haiwezi kumpa mkopo
Teh tehe..sipendi mikopo M/Mungu naomba niepushie
 
Nadhani kufanya biashara na makampuni makubwa pamoja na serikali kumezifanya hizi benki kuwa na kiburi kisichomithilika.

Kwa watumishi wa UMMA, hawana shida, nadhani wanaogopa kumkorofisha jamhuri mwenyewe.

Kwa taasisi binafsi, huko sasa ndio mpaka taasisi husika iwe ina-bank nao, wawe na makubaliano ya udhamini kwa wafanyakazi wao, idadi ya wafanyakazi isipungue 20 na blah blah nyingi tu.

Sasa kama unavyosema, mtu anapitisha mshahara kwao miaka saba, unashindwa kumuamini, ila akija na hati za shamba, unamuamini....

Wenzetu, mkopo ni kati ya Bank na mkopaji, huitaji kudhaminiwa na muajiri. Wao watakwambia, waTZ hatuna makazi/address za kudumu.

Wenzetu wanatumia elimu zao kurahisisha maisha kulingana na mazingira waishiyo, sisi kwakuwa tunakariri kufaulu mitihani, tunashindwa kufanya kwa mantiki.
 
Hivi huwa wanapigaje mahesabu yao! Ukisikia riba asilimia 14, 16% unaweza kutabasamu kabisa

Kivumbi kapigiwe hesabu au kachukue mkopo.

Mfano; Unakopa Milioni 10, utarudisha Total Milion 15 (Unachokopa, utarudisha riba ya karibia nusu).
Iko hivi unakopa milioni 10 lakini utakayopewa ni 7 na ushee tu, ingne watakuambia ni posho ya uchakataji wa huo mkopo. ila utakayolipishwa itafika au kuzidi milioni 15 kutegemea na muda wa marejesho. nchi ya uchumi wa kati
 
Teh tehe..sipendi mikopo M/Mungu naomba niepushie
Diana kachukue mkopo, uoga wako ndiyo umasikini wako,
Screenshot_20200711_103806.jpg
 
Hivi huwa wanapigaje mahesabu yao! Ukisikia riba asilimia 14, 16% unaweza kutabasamu kabisa

Kivumbi kapigiwe hesabu au kachukue mkopo.

Mfano; Unakopa Milioni 10, utarudisha Total Milion 15 (Unachokopa, utarudisha riba ya karibia nusu).
Apo kuna hesabu ya riba per annual/mwaka kuna processing fee kuna bima ya mkopo.. unakuta umekopa million 9 unalipa 16..
 
Iko hivi unakopa milioni 10 lakini utakayopewa ni 7 na ushee tu, ingne watakuambia ni posho ya uchakataji wa huo mkopo. ila utakayolipishwa itafika au kuzidi milioni 15 kutegemea na muda wa marejesho. nchi ya uchumi wa kati
Yes watakayo kata humo humo wanakata na bima ya mkopo
 
Back
Top Bottom