CRDB badilikeni, tutawakimbia sana msipoangalia

Ndugu wanabodi,

Heshima sana kwenu. Naomba nijielekeze kwenye mada mohja kwa moja. Tangu niifahamu sekta ya fedha niliiona CRDB kama moja ya benki zenye kasi, ubunifu na hata umakini kiutendaji. Kutokana na hayo niliamua kwa hiyari yangu pamoja na wenzangu kujiunga na benki hii miaka kadhaa iliyopita baada ya kuchoshwa na benki fulani hivi hapa nchini (sitaitaja jina kwa sababu za kibiashara).

Mwanzoni nilifurahia sana huduma za CRDB na sikua na shaka iliposemekana ni premier bank kwa customer service nzuri na ya haraka kwa nchi yetu. Lakini kwa siku za karibuni nimekuwanakutana na huduma zisizorishisha ndani ya benki hii katika matawi mbalimbali. Siku moja nilienda pale CRDB mlimani city kiroho safi kabisa kusukuma mambo yangu. Huwezi amini nilikaa foleni ndefu sana huku tellers wakiwa wawili tu wanaohudumia msururu mrefu wa wateja kede kede walioonekana kutokuridhishwa na huduma walizokutana nazo pale. SBaadhi ya wateja walihamaki walipoona ni tellers wawili pekee wanaohudumia ilihali mstari ni mrefu huku tawili liko kwenye potential area kama ile.

Siku nyingine nilienda CRDB waterfront pale. Hali ni hiyo hiyo. Mstari ni mrefu na tellers ni wawili tu ilhali kuna clearing agents kibao wanaotaka ku-deposit mamilioni ya kodi, tozo mbalimbali na hata malipo makubwa kwa makampuni mbalimbali karibu na bandari kubwa ya nchi (Dar es Salaam). Hali hii huzua mitafaruku ya kuwahiana foleni kwa wateja na hata kujibizana sometimes (jambo ambalo si afya) na kama litaendelea kuna hatari ya benki kupoteza wateja wengi kwa muda mchache ujao kama hawatakuwa makini.

CRDB Azikiwe Premier nako kuna wateja wengi ila angalau kwa mbali japokuwa sometimes kunakuwa na mstari mrefu sana. CRDB Makumbusho nako ni vile vile. Watu wengi na tellers wachache. CRDB Masika morogoro nadhani ndiyo branch kubwa zaidi kwa mkoa ule na ina watu wengi sana japo niliwahi kuhudumiwa pale wanajitahidi sana (mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni). Office space yao ni ndogo sana na Morogoro inazidi kuwa mji mkubwa kila siku. Tafadhali Director of Procurement na Director of Administration shughulikieni hili jambo kwa haraka. Pale Masika morogoro wanapiga kazi sana lakini muwawezeshe office spec kubwa zaidi. Sina shida nao kwa kweli.

List ni ndefu sana lakini jambo nililoligundua ni kwamba CRDB kuna upungufu mkubwa wa wafanyakazi jambo linalopelekea kuzorotesha huduma kwa matawi yao mengi makubwa hasa hapa jijini Dar es Salaam. Uongozi wa CRDB hauna budi kulishughulikia suala hili mapema kabla halijageuka kuwa kansa itakayodumaza utendaji wa taasisi. Na kwa ulimwengu huu wa ushindani ninawajibika kusema kama CRDB wasipojipanga, basi soko litawapanga.

Lingine ambalo linazidi kuwa chukizo kwa watu wengi ni makato makubwa tunayokutana nayo wateja pale tu tunapofanya miamala na hata kupata huduma mbalimbali. Siku moja nilitoa pesa pale CRDB Lumumba ghafla nikaona nimekatwa elfu 12. Nikashanga na sikuridhishwa. Nilijiapiza jioni ile kuwa kutakjapokucha mguu wangu mguu wa branch manager anieleze hayo makato yametoka wapi. Nilisogea pale customer service na walichonieleza kiliniduwaza kwa kweli. Waliniambia hayo makato niliyokatwa yanaitwa annual card fees. Nilishangaa na kujawa na hasira kali kwa sababu sikuelezwa hicho kitu mwanzoni kabisa.

Siku nyingine nilienda ku-renew kadi yangu iliyoisha muda ila nikaelezwa kwamba gharama yake ni Tshs 25,000/=. Nilighafirika sana ila kwa sababu nilikuwa na shida nilikubali utaratibu uendelee ili nitoa akiba yangu iliyokuwepo wakati huo. Matukio hayo yaliniacha na vidonda vikubwa kiasi cha kuanza kutafuta mbadala wa CRDB bank mapema kabisa. Hivi sasa nasubiri nimalizane na mkopo wao niondoke kama wataendelea na utaratibu huu usioridhisha.

Wito wangu kwa uongozi na menejimenti ya CRDB, mnapaswa kuchukua hatua mapema kabla hamjakimbiwa na wateja kwa mpigo. Soko linabadilika na malalamiko kwa utendaji wenu yamekuwa makubwa sana siku za karibuni. Msipochukua hatua na kujipanga mapema, soko litawapanga aminini nawaambia.

Ninaipenda sana CRDB bank lakini mwenendo wake kwa siku za karibuni unanikatisha tamaa kabisa.

Am out.

Nawasilisha hoja.
Kimei ameondoka na crdb ndugu, even mm ni mteja wao kwa miaka 12
 
Kuna mtu nilimshauri ahame NBC aende CRDB sababu ya mambo flani.
Kafungua fixed account muda ukafika akaenda kuweka tena awamu ya pili.
Wakampigia hesabu faida yake na kuweka tena.
Kabla hajafika nyumbani kwake anapigiwa simu tulikosea mahesabu njoo ujaze upya fomu akawaambia nipo mbali labda siku nyingine. Aliyempigia simu akamuambia nitumie kwenye simu fedha ya ziada niliyokosea mahesabu ili fixed account yako iendelee.
Yule mteja akamjibu nitakuamini vipi kama haunitapeli na wizi wote huu wa mtandaoni/simu?

Baada ya siku chache kakuta pesa yake imeingizwa kwenye account yake ya kawaida(savings account) amekatwa faida yake yote. Ni kwamba alitunza pesa yake bure bila faida.

Walishindwa nini kumsubiri apate ruhusa kazini aje ajaze fomu zao hadi wamekula faida yake yote?
Kukotoa walikosea wao watumishi wa bank.

Suala hili tukipata muda tunakwenda kuwashitaki bank na kuwadai fidia wajiandae CRDB tawi la UDSM. Walimuona yule mdau siyo mjuaji wa sheria au mtu wa kawaida hatawasumbua, hawakujua ANA WATU wajuaji na watata.
Samahani naomba kujua ukiweka hela katika saving account wanakata shilingi ngapi kwa mwezi au makato yao yakovipi kwa ujumla
 
Nchi za wenzetu, hasa hasa Sweden na Uholanzi.

1.Hakuna makato ya kutoa pesa
2. Hakuna makato ya kuhamisha au kutuma pesa
3. Unaweza kuweka pesa kwenye baadhi ya ATMs. Hakuna haja ya kwenda bank.
4. Makato ninayojajua ni monthly card maintenance fee ambayo ni kati ya Tsh 5000 - 7000/= kutegemea na bank.
5. Kwa wanafunzi, including University students, hakuna makato yoyote.
 
CRDB wako wapi, wajibu tuhuma hizi, na Dodoma ATMs zao fedha ni za kubahatisha unaweza tembea hata branch tatu bila mafanikio, Mwisho wa siku ukaamua kutolea tawi jingine tofauti kabisa.
Tunawasubiri waje waseme neno
 
Ume
Kuna mtu nilimshauri ahame NBC aende CRDB sababu ya mambo flani.
Kafungua fixed account muda ukafika akaenda kuweka tena awamu ya pili.
Wakampigia hesabu faida yake na kuweka tena.
Kabla hajafika nyumbani kwake anapigiwa simu tulikosea mahesabu njoo ujaze upya fomu akawaambia nipo mbali labda siku nyingine. Aliyempigia simu akamuambia nitumie kwenye simu fedha ya ziada niliyokosea mahesabu ili fixed account yako iendelee.
Yule mteja akamjibu nitakuamini vipi kama haunitapeli na wizi wote huu wa mtandaoni/simu?

Baada ya siku chache kakuta pesa yake imeingizwa kwenye account yake ya kawaida(savings account) amekatwa faida yake yote. Ni kwamba alitunza pesa yake bure bila faida.

Walishindwa nini kumsubiri apate ruhusa kazini aje ajaze fomu zao hadi wamekula faida yake yote?
Kukotoa walikosea wao watumishi wa bank.

Suala hili tukipata muda tunakwenda kuwashitaki bank na kuwadai fidia wajiandae CRDB tawi la UDSM. Walimuona yule mdau siyo mjuaji wa sheria au mtu wa kawaida hatawasumbua, hawakujua ANA WATU wajuaji na watata.
Umepiga mkwara.walijua huyo atakuwa mwanafunzi wa UDSM siyo mwekezaji
 
Mimi crdb sijadeposit kitambo wamezid makato. Leo nachungulia balance nakuta nina -1800
 
Kuna mtu nilimshauri ahame NBC aende CRDB sababu ya mambo flani.
Kafungua fixed account muda ukafika akaenda kuweka tena awamu ya pili.
Wakampigia hesabu faida yake na kuweka tena.
Kabla hajafika nyumbani kwake anapigiwa simu tulikosea mahesabu njoo ujaze upya fomu akawaambia nipo mbali labda siku nyingine. Aliyempigia simu akamuambia nitumie kwenye simu fedha ya ziada niliyokosea mahesabu ili fixed account yako iendelee.
Yule mteja akamjibu nitakuamini vipi kama haunitapeli na wizi wote huu wa mtandaoni/simu?

Baada ya siku chache kakuta pesa yake imeingizwa kwenye account yake ya kawaida(savings account) amekatwa faida yake yote. Ni kwamba alitunza pesa yake bure bila faida.

Walishindwa nini kumsubiri apate ruhusa kazini aje ajaze fomu zao hadi wamekula faida yake yote?
Kukotoa walikosea wao watumishi wa bank.

Suala hili tukipata muda tunakwenda kuwashitaki bank na kuwadai fidia wajiandae CRDB tawi la UDSM. Walimuona yule mdau siyo mjuaji wa sheria au mtu wa kawaida hatawasumbua, hawakujua ANA WATU wajuaji na watata.

Japo sijui sheria sana ila kama walihamisha fedha kutoka fixed akaunti yake kwenda akaunti ya kawaida lugha rahisi ni kwamba wamevunja mkataba walioingia na jamaa maana fixed deposit akaunti ni mkataba.

Nendeni nao taratibu zitawatoka fedha kwa sababu wamevunja mkataba plus usumbufu kwa mteja
Huyo alopiga hesabu vibaya ajiandae kurudi kijijini kuendeleza mashamba ya familia yake kama namuona
 
Wapumbavu hao, Wana Makato balaa, alafu ukiwaambia hata hawashughulikii kero kwa kujivunia wateja
 
Absa wako vizuri sana sio hizi bank zakibongo full mizinguo Hata ukitaka kutumia online banking mizinguo,ATM sasa network full kugoma unaamua utumie sim banking nayo mizinguo
 
Labda wapo kwenye mpango wa kupunguza wateja, maana mfano airtel walikuwa na watu wengi wakazingua now offer kila siku. Wako wapi NBC walilinga hadi basi sasa naona full matangazo
Wamerudi na ligi kuu ya NBC Premier League. Naona wanarejea taratibu
 
Absa wako vizuri sana sio hizi bank zakibongo full mizinguo Hata ukitaka kutumia online banking mizinguo,ATM sasa network full kugoma unaamua utumie sim banking nayo mizinguo
Na ATM zao zinaishiwa sana kwa sasa tena maeneo prominent kabisa
 
Kumbe ku renew card makato ni elfu 25,nilitaka kwenda kurenew card yangu ya CRDB,Mara ya Mwisho nimemtumia mwaka 2015 na ikaisha muda 2016
Bora nifungue Account mpya sasa
 
DIASPORA account $ to $
3 months of account opening request tena kwa mbinde.

Sijawahi kukutana na upuuzi wa namna hii.
Mpaka kupeana ahadi za kupelekana kwenye sheria ndipo wakafungua account

Mara ya kwanza kufanya deposit ya $50 tu for a start as a trial, nikapigwa.
(Imani yangu ilikua na mashaka juu yao)

Technically kosa ni la kiufundi kwangu kutuma TSH kuingia kwenye $ account lakini walishindwa KuConvert iyo pesa ndogo iingie kwenye $ acc’ nikaomba wafanye refund MPAKA LEOOOOO 2022 na issue ya
IMG_5589.png

2020.

SHAME CRDB.

Azikiwe bruch
Attendants LUCY & JOSEPH.
 
Back
Top Bottom