Crazy things you did in secondary school

hahahaaa mm nakumbuka mwaka 2008 niko form 4 galanos tanga, kuna mwalim mmoja alikuwa anaitwa macmaster Luziro, alinidaka mtaani..., Sasa akajifanya mjanja et ananiita ananiuliza kijana unasoma wapi, nikamwambia nguvumali sec. Akasema bas nimekufananisha na mwanafunz wang nilimfundisha Ecknford.., Nikamuambia umenifababisha... Sasa hapo wote tukawa tumedanganyana wakat mm nilikuwa namsoma...

Ila alikuja akajua akaniambia we dogo ulinichezea sana akili
 
Siku za mvua hatutaki enda morning prepo so tunaweka vitanda kwenye entrances zote za bweni, tunapanda dalini na kutoa bulbs then tunakaa juu mpaka mvua ikate. A friend of mine almost fell down kwa kupitiliziwa na usingizi, ahahahahaha remembering this makes me laugh
 
kwa shule za bweni,madume watupu,siku ya disko ilikuwa ishu..matayarisho ni zaidi ya miezi miwili.....kuhusu viwalo ,kwenda library ilikuwa muhimu ie kuazima pafyumu na nguo...kachupa ka pafyumu huwa kanakuwa kamoja,mnapulizia kwa zamu...ukichelewa ukikuta imeisha,unavunja kale kamdomo ka chupa then unajaza maji ,unatikisa kidogo,nawe unapaka....ndo maana kuna kademu wakati wa bluzi kaliwahi kuniuliza mbona wote mnanukia harufu zinazofanana??..nikapata kigugumizi..nikabaki eeer ooh eerr...ndani ya disko ole wako usiopoe kademu hasa wakati wa bluzi...bwenini hautakaa...manake baada ya disko wenzio wataanza kuletewa barua zenye manukato ,wewe hola!!!
kuhusu stempu ...kulikuwa na kaujuzi ka kufuta ule muhuri nafikiri kwa kutumia sponji na sabubi flani....then una reuse......maisha yalikuwa raha sana jamani!!!
DAH SIJUI KWANINI NILIKUWA MZEMBE
 
~Ulitengeneza water heater kwa kutumia spring za vitanda. Usiku wa manane unachemsha mahindi ya shamba la shule. Container la kuchemshia mahindi ni plastic la nje la chupa ya chai iliyoondolewa flask yake, inashikiliwa upside-down, i.e mfuniko ndo unakuwa base, na bottom yake inafunguliwa kuwa ndo mdomo wa 'sufuria' lako. Heater inawekwa kwanza katikati, then mahindi yanakatwa vipande na kupangwa around the heater.

Ukimaliza kuchemsha unarudisha waya wa umeme juu ya dari ambako ndiko connection ilikofanyika, kwani ni marufuku kutumia umeme wa socket!

Hii tuneifanya sana watoto wa Tanga School....
 
Kukwepa kukaa mstarini kisa kuadhibiwa kwa viboko msimu wa baridi.

Nakumbuka nilikuwa kidato cha kwanza mwezi agosti, ilisikika sauti mwanafunzi wa kidato cha nne akiongea assemble, tulipigwa wote. Tangu siku ile nilikaa assemble siku ya national and Mock exams tu (Form 2 $ 4)
 
~Ulitengeneza water heater kwa kutumia spring za vitanda. Usiku wa manane unachemsha mahindi ya shamba la shule. Container la kuchemshia mahindi ni plastic la nje la chupa ya chai iliyoondolewa flask yake, inashikiliwa upside-down, i.e mfuniko ndo unakuwa base, na bottom yake inafunguliwa kuwa ndo mdomo wa 'sufuria' lako. Heater inawekwa kwanza katikati, then mahindi yanakatwa vipande na kupangwa around the heater.

Ukimaliza kuchemsha unarudisha waya wa umeme juu ya dari ambako ndiko connection ilikofanyika, kwani ni marufuku kutumia umeme wa socket!
Wewe ulikuwa Ifunda technical nimekustukia!!!
 
Ulikua Nan
1538633600421.jpeg
 
Karatu high school..... Muda wa kulala Kuna jamaa alikuwa anatoa ushuzi balaa siku ya makande sasa siku moja alijisahau akawa amazungushia kitanda chake Na shuka Ile kutoa ushuzi harufu ikamzidia ndani ya shuka jamaa akatoka nduki...toka siku hiyo alikoma tabia hiyo
ii ii
 
kuna kijamaa tumesoma nacho high school vile vinatumwa na jimbo kilikua kinajifungia kupiga msuli kuanzia sa moja asubuhi mpaka kumi na mbili jioni eti kikitoka huko madini yanajaa kichwani mpaka sauti inapotea inakua ukikisemesha kinaongea kwa shida kama ile ukinigwa na moshi wa bangi unavokua kinaongea sauti haitoki eti!!

nyingine nilikuaga na tabia ya kutoroka shule usiku naenda kuangalia miziki ya kikongo kwenye tv kwenye vibandaumiza kijiji cha jirani siku moja mida ya saa tano usiku kuna ki mbalamwezi niko narudi shule kwenye njia ninayopita kama mita 25 hivi kushoto nikaona fisi kama tisa wanagombania fisi jike mmoja!!!

aisee asikwambie mtu binadam anaweza kufanya vitu vikubwa sana anapokua kwenye hali ya kufa ama kupona na sifaham hata nilivuka vipi pale manake mbio nilizotimua siku hiyo hata uchukue bodaboda hunikuti, umbali ambao kikawaida nilikua natembea dk 20 siku hiyo sikuzidisha dakika nne nilikua nishapanda kitandani nimelala.

sitaki kuikumbuka hiyo siku make hua napata uoga sana
 
Back in the days mi na wanangu tulikua boarding school sasa karibu kila siku hatuli chakula cha skuli (hata ukiwa wali) usiku tunaenda kula chips au tambi nk tukirudi shule hatusomi ni stori tupu na kuchat thanks God group letu tukawa na div 1 na 2 basi

Kuna Dem nilivokua fm2 siku namuona tu nikampenda alikua chotara basi nikampa smart phone,canteen kila siku namlipia but nikawa namuogopa akanilia hela zangu akamaliza skul coz alikua form 4 aka fail akabaki home,
Aliniendesha sana kila atakacho nampa ,elfu 10 mpaka 50 najibana pocket money, nilivofika form 5 akaolewa then akani block whatsapp,
Dah toka kipindi kile simuamini kiumbe anayeitwaga mwanamke, na hata mahusiano yangu mengine yanadumu mpaka week 2 tu napiga chini
Nikikumbuka dah am sad
Ulikuwa fala sana wewe
 
Back
Top Bottom