Pablo Blanco
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 7,328
- 6,591
Safi ndo dawa yake2.Kuna dogo alikuwa informer/snitch skuli ikawa kila mkifanya kitu bwenini au darasani anaenda kuripoti kwa displin masta tulipomgundua,tukavizia watu woote wako prepo tukarudi bwenini,tukatekenya tranka lake tukalifungua,ndani kaweka vitabu vyake,material na nguo kadhaa,tukamiminia bakuli la maharagwe na mchuzi wake alafu tukalifunga lile tranka then tukalitikisatikisa na kulisheki sheki vizuuri kabisa mpaka vitu vikajimiksi vizuri ndani,alafu hao tukarudi zetu klasi kujisomea.ebana jamaa alivyorudi alilia mpaka huruma,shida wengi walikuwa wanamchukia kwahyo wadau wakawa wanafurahia chini kwa chini na kuanzia hapo akakoma umbea,kama uko humu ndugu tusameheane ilikuwa utoto tu.