Crazy things you did in secondary school

Unachukua makande mchana unayatunza hadi kesho kesho upige na uji
Hahahaha,achana na makand3 hata ubwabwa pia unautunza af kesho yake asubuhi unaupga na uji au unauchanganya kwa pamoja uji na ubwabwa.

Yan hatari tupu af chakushangaza hata tumbo haliumi wala ubwabwà kuchacha....
 
Ndanda boys high school, weekend tulikua tunaenda masasi na washkaji zangu wawili tukiwa tumevaa suruali zetu nyekundu, mashati ya tomato na tai zetu .

Tulisikia masasi girls wanatokaga pass jumamos wanaenda town halafu huwa wanawashobokea Ndanda boys kwaio sisi tulikua tunaulamba uniform then tunaenda kuzugazuga town. Kiukweli tulikua tunauza sana.
 
I was thief I steal mathematics books but when I finished form 4 I got F in math exam now I know there no advantage of being thief (Kingereza kilikuja na boat poooh)
Pole mkuu, f ya math? Daah kweli genealogy ya math imepita kushoto kwenye ukoo wenu
 
hahahahahaha umenikumbusha mbaaaaali miaka yangu yote shuleni sikuwahi kutumia maji lakini cha ajabu nikirudi likizo situmii makaratasi.........kuna wakati magodoro unakuta limenyofolewa wamekwenda kujiswafia.
Jamani jamani magodor magodoro yetuuuuu, hakika ya kale dhahabu
 
Nilichokigundua ni kwamba Watanzania haswa vijana tulipokuwa shuleni basi tabia zetu, mienendo yetu karbia yote ilikuwa sawa, nakumbuka enzi za shule siku za disco, ni ubishoo hadi basi, siku za mikusanyiko za sherehe za dini, za shule na pale shule X ilipokuwa inakutana na shule Y kwakweli hali ilikuwa ni tofauti(RUGAMBWA SECvs IHUNGO SEC) kwakweli hapa siwezi kusahau tulipokuwa tunakutana.
 
1.Kuna madogo walikuwa na tabia ya kuja kuiba zaga bwenini kwetu,leo wamebeba tisheti,kesho sabuni, keshokutwa sahani, tulipowagundua wala hatukuwauliza kitu, madogo wenyewe wakishua wanajifanya wamepinda kisa wanakula ganja

basi nkaa na kikosi kazi changu tukajadili cha kuwafanya,tukavizia visiting day wameletewa mazagazaga na mapokopoko ya kumwaga jumapili, jumatatu yake watu wako class tukarudi dorm tukawasafisha kila kitu mpaka mashuka, vunjavunja matranka beba nguo zote, Nido, Mabiskuti, nguo, juisi tukawaachia yunifomu,madaftari na vitabu,ilikuwa operesheni ya dakika kama 15 hivi alafu hao tukarudi class kama sio sio sisi vile.
 
Back in the days mi na wanangu tulikua boarding school sasa karibu kila siku hatuli chakula cha skuli (hata ukiwa wali) usiku tunaenda kula chips au tambi nk tukirudi shule hatusomi ni stori tupu na kuchat thanks God group letu tukawa na div 1 na 2 basi

Kuna Dem nilivokua fm2 siku namuona tu nikampenda alikua chotara basi nikampa smart phone,canteen kila siku namlipia but nikawa namuogopa akanilia hela zangu akamaliza skul coz alikua form 4 aka fail akabaki home,
Aliniendesha sana kila atakacho nampa ,elfu 10 mpaka 50 najibana pocket money, nilivofika form 5 akaolewa then akani block whatsapp,
Dah toka kipindi kile simuamini kiumbe anayeitwaga mwanamke, na hata mahusiano yangu mengine yanadumu mpaka week 2 tu napiga chini
Nikikumbuka dah am sad
 
2.Kuna dogo alikuwa informer/snitch skuli ikawa kila mkifanya kitu bwenini au darasani anaenda kuripoti kwa displin masta tulipomgundua,tukavizia watu woote wako prepo tukarudi bwenini,tukatekenya tranka lake tukalifungua,ndani kaweka vitabu vyake,material na nguo kadhaa,tukamiminia bakuli la maharagwe na mchuzi wake alafu tukalifunga lile tranka then tukalitikisatikisa na kulisheki sheki vizuuri kabisa mpaka vitu vikajimiksi vizuri ndani,alafu hao tukarudi zetu klasi kujisomea.ebana jamaa alivyorudi alilia mpaka huruma,shida wengi walikuwa wanamchukia kwahyo wadau wakawa wanafurahia chini kwa chini na kuanzia hapo akakoma umbea,kama uko humu ndugu tusameheane ilikuwa utoto tu.
 
Back
Top Bottom