Crazy Things You Did In Sec School | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Crazy Things You Did In Sec School

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Invisible, Nov 28, 2008.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Nov 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ~ Got chased by the headteacher and deputy head, a whole crowd of us in school uniform where in one area our school had been forbidden to enter by the school otherwise could result in expulsion, only 2 were caught, thank God I was not part of the two...

  ~ You used my camera to take photos of your sleeping friends, especially when they were drooling and posted it on the announcement boards...

  ~ Used to sneak out of school all the time as a day student and buy foodstuff that were all contraband...

  ~Would go to the dining hall before the lunch bell goes...

  ~ Used to write rylics of the artists of your preference... (remember 2Pac, Bob Marley?)

  ~ Ulizoea kujiandikia barua ili uonekane wewe ni mpokeaji mzuri wa barua.

  ~ Ukitumiwa EMS au TMO basi wewe unaonekana Baab kubwa!

  ~ Kuchomekea shati ilikuwa kero kwako, ulifanya hivyo wakati wa kukaguliwa Jumatatu baadae 'unapiga chini'.

  ~ Kufua soksi ilikuwa kero sana kwako, ulikuwa unazivaa mara 5 kwa wiki kisha unazifua Jumamosi (ukiwa na pair moja).

  Hizi ni baadhi, tena nyingi ni kwa upande wa wanaume... Ladies, what you used to do (crazy ones pls).
   
 2. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tehe tehe Tehee! Mkuu, mbona umenikumbusha mbali!

  ~Kwa kuwa mgao wa nyama mezani hautoshi, na nyama zenyewe ni mara moja kwa wiki, basi kiranja wa Bwalo akigeuka tu pembeni, umekwapua nyama kwenye dishi la msosi na kutia nyama kadhaa kwenye mfuko wa suruali !!! Kwikwi kwi...!
   
 3. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  ~Hata hizo barua unazojiandikia mwenyewe, hununui stamp hata siku moja! Stamp inafutwa muhuri na kutumika mara kadhaa! I think Shirika la Posta na Simu (jina la enzi hizo) halikupata chochote kwa barua kutoka mashuleni!
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Nov 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  I see tulofanya hivi tupo wengi sana. Nilikuwa nikipata barua basi najua 'deal' hilo. Stamp itatumika kwenda kwingine... Ufisadi ulianzia huku :)
   
 5. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Enzi za Ugumu na Utoto wa Kishua. Mtu anaamua kuogea Omo badala ya sabuni za kawaida eti aonekane mgumu.
   
 6. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  ~Ulitengeneza water heater kwa kutumia spring za vitanda. Usiku wa manane unachemsha mahindi ya shamba la shule. Container la kuchemshia mahindi ni plastic la nje la chupa ya chai iliyoondolewa flask yake, inashikiliwa upside-down, i.e mfuniko ndo unakuwa base, na bottom yake inafunguliwa kuwa ndo mdomo wa 'sufuria' lako. Heater inawekwa kwanza katikati, then mahindi yanakatwa vipande na kupangwa around the heater.

  Ukimaliza kuchemsha unarudisha waya wa umeme juu ya dari ambako ndiko connection ilikofanyika, kwani ni marufuku kutumia umeme wa socket!
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Nov 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Na siku ya kula wali unavaa nguo za mapigano. Uji ukiwa hauna sukari na maharage yamejaa wadudu lakini mnagombania!
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Nov 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha,

  Yani wewe umenirejesha enzi hizo kwelikweli. You kill my nerves!
   
 9. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu Invisible unanifurahisha lakini ndio ukweli wenyewe. Disco likipigwa na mademu jamaa wanapagawa wiki moja kabla.
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa shule za madume unaongelea wiki moja tu? Hata mwezi mzima mzee. Siku hiyo ni hatari. Ikibidi nguo zitaazimwa kwa washikaji town!

  Ila ukiingia kwenye muziki ni kuwa mwangalifu ili blues ikipigwa usiwe single vinginevyo utaondoka ukimbini. Na mademu wasiotaka kucheza blues kibano ni halali yao. Kwanza kwa nini wamekuja disco kama hawataki kucheza. Ila blues yenyewe inavyochezwa du, ni hatari tupu. Hata hivyo disco ni mara moja kwa muhula so enjoying for 3 or more hrs was something you wouldn't want to miss hata kama una malaria!!
   
 11. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Duuh! Kweli mambo yanafanana! Kwetu pale mabrazameni walikuwa wananyoa nywele mtindo mtindo special for disco aka debe. Halafu baada ya disco inabidi alazimike kuyoa tena kuondoa mtindo huo kwani darasani ni marufuku.
  Mnakumbuka nguo za OPP ?? Siku ya disco OPP kibao!
   
 12. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2008
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  kwa shule za bweni,madume watupu,siku ya disko ilikuwa ishu..matayarisho ni zaidi ya miezi miwili.....kuhusu viwalo ,kwenda library ilikuwa muhimu ie kuazima pafyumu na nguo...kachupa ka pafyumu huwa kanakuwa kamoja,mnapulizia kwa zamu...ukichelewa ukikuta imeisha,unavunja kale kamdomo ka chupa then unajaza maji ,unatikisa kidogo,nawe unapaka....ndo maana kuna kademu wakati wa bluzi kaliwahi kuniuliza mbona wote mnanukia harufu zinazofanana??..nikapata kigugumizi..nikabaki eeer ooh eerr...ndani ya disko ole wako usiopoe kademu hasa wakati wa bluzi...bwenini hautakaa...manake baada ya disko wenzio wataanza kuletewa barua zenye manukato ,wewe hola!!!
  kuhusu stempu ...kulikuwa na kaujuzi ka kufuta ule muhuri nafikiri kwa kutumia sponji na sabubi flani....then una reuse......maisha yalikuwa raha sana jamani!!!
   
 13. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2008
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Form 1 walivyopokelewa unakuta mmoja anaambiwa zima taa ya umeme kwa kuipuliza kama kibatari halafu eti nae anapanda kwenye cabinet anapuliza. Kicheko hadi basi.....
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Pale Shirati sekondari miaka ya 1973 na 1976 Siku ya wali na nyama nilivyokuwa nakuwa wa kwanza mstari wa kuchukua chakula then kwa dakika tatu nimesharudi kuchukua kingine kama sijala vile.
  Sie tulikuwa tunapanga mstari kugawiwa chakula.
   
 15. B

  Baba Lao Member

  #15
  Nov 30, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Zamazamani,sponyi na sabuni vilikuwa vinakwangua mihuri ya stemp.sisi tulikuwa kunafuta kwa NYUSI,Je ,unakumbuka zali la kutonyoa ndevu?
   
 16. Ngonalugali

  Ngonalugali JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2008
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Kwa wale akina yakhe kama mimi bajeti ya sabuni ni mchii mmoja kwa mhula basi kufua shati ni mara moja kwa wiki na kuoga ni Jumapili (unatoka bafuni kama umejipaka unga).

  Kutokuwa na pasi nako kulifanya ubunifu mkubwa wa kukunja nguo kiustadi na kuzilalia zikiwa chini ya godoro, aah no tandiko.

  Mmmhh msinikumbushe mie yaliyotokea wakati huo!!
   
 17. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,277
  Likes Received: 4,260
  Trophy Points: 280
  Yeah Mkubwa OPP za draft
   
 18. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,277
  Likes Received: 4,260
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka siku ya kula wali J4 lakini viongozi wa chakula anajichotea wali wa kutosha anakulahadi Ijumaa
   
 19. Ngonalugali

  Ngonalugali JF-Expert Member

  #19
  Dec 1, 2008
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha jamaa mmoja aliyekuwa anatafuta nafasi ya ku-serve siku ya wali na akiipata utakiona kivumbi chake maana siku mbili hadi tatu anakula wali tena bila hata kuchemsha.
  Jamaa huyo aliendelea kuwa tabia yake maana nilipata habari kuwa kwenye harusi ya mdogo wake huko kijijini alijiwekea pilau kwa ajili ya safari kesho yake. kilichotokea ni kuharisha karibu njia nzima.

  jamani tabia za shule zingine zafaa kuachwa uanpofika uraiani.
   
 20. Ngonalugali

  Ngonalugali JF-Expert Member

  #20
  Dec 1, 2008
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Wakati wa uji vyombo vilikuwa SADOLIN, kuna jamaa namkumbuka na sadolin lake lililokuwa limeandikwa DON'T SPY ME. jamaa anajaza na kumaliza peke yake.
   
Loading...