CRANE toka nje, itakuwa inaweza kubeba tani 26 na inaizidi vipi CRANE XCMG 56000 KG yenye kuweza kubeba tani 90?

Mbeba Rawama

Member
Apr 10, 2020
11
45
MILANGO YA BWAWA LA UMEME, TANI 26, KUKODI WICHI TOKA NJE, NIKUTUPIGA WATZ NA KITU KIZITO

Watu wengi wameonekana kushangazwa na maelezo ya Waziri wa sekta husika baada ya kujibu hoja mbungeni kuhusu maendeleo ya mradi wa bwawa la umeme Lililopo kati ya Rufiki na Morogoro.

Ambapo Waziri alisema, Hatua ya kwanza ya kujenga ukuta imeishafanyika isipokuwa hatua ya pili ambayo nikuweka MILANGO YA CHUMBA YENYE TANI 26 ndiyo bado haijakamilika kwa sababu INASUBIRIWA CRANE (WICHI) YA KUKODI TOKA NJE YA NCHI KWA AJILI YA KUJA KUSETI HIYO MILANGO.

WAZIRI kama umeambiwa basi maelezo uliyoambiwa na unayotakiwa kuyatoa kwa umma wa Watanzania yalitaliwa kuwa na ufafanuzi mzuri na wenye kueleweka.

Haiwezekani Crane zilizoko ndani ya mradi wa umeme zishindwe kubeba mzigo wa tani 26. Wakati Crane ZILIZOKO KWENYE MRADI ZIKO ZENYE KUBEBA TANI 25, 50, 60, 90, 120 NA HATA 200

Waziri CRANE ILIYOPO KWENYE MRADI WA UMEME AINA YA XCMG (Total Mass: 36000 Kg Ukichomoa Boom Angle ya Lenght 10.3 na boom ikawa kwenye mlalo wa Mita 4 INAWEZA KUBEBA TANI 43.5, 53 na TANI 55 ILA ITAWAKA ALAMA YA NJANO KUONESHA NI HATARI

Crane XCMG 36000 Kg ikiwa na Counter weight 7.6 boom ikawa Mlalo wa 20.6 na radius ya Mita 3, Crane hii INAWEZA KUBEBA MZIGI TANI 26.0 HADI 27.6.

Hii CRANE ya kusubiriwa kutoka nje ya nchi ina uwezo gani wa ziada kuzidi crane zilizoko ndani ya mradi au ina maajabu yapi kuliko crane zilizopo.

Hii CRANE inayosubiriwa toka nje ni ya nani na inakodiwa dola ngapi kwa saa na itatumia siku ngapi?

Hii CRANE toka nje, itakuwa inaweza kubeba tani 26 na inaizidi vipi CRANE XCMG 56000 KG yenye kuweza kubeba tani 90.

Hii CRANE YA KUKODIWA ina maana inaizidi LIBBER CRANE ambayo inaweza kubeba TANI KATI YA 50, 90 na 120.

CRANE HII TOKA NJE INAIZIDI CRANE AMBAYO IKO KWENYE MRADI NA INAWEZA KUBEBA TANI 200 mbona kama nikuwapiga Watanzania na kitu kizito.

CRANE Toka nje inazizidi uwezo Crane Tower zote zilizoko kwa Mchina, Mwarabu, AFFCO na zinginezo, Hapana Mh, Waziri maelezo hayawaridhisha Watanzania.

Watanzania wa sasa wameishaelimika na wanahitaji ufafanuzi yakinifu ili kuwaridhish
FB_IMG_1637167289047.jpg
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
9,246
2,000
Mtoto wa mstaafu huyo, muacheni alete mabadiliko ahahahaa...

Kule wizara ya mazingira alikuwa anapiga deal tu 😂, ukipeleka vision yenu kama taasisi fulani yeye anaigeuza inakuwa yake daa hii nchi.

👉🏾 Naendelea kujifunza tabia ya binadamu!.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom