CPC yafanikiwa kukuza maendeleo ya kasi kati ya China na Afrika

ldleo

Senior Member
Jan 9, 2010
163
250
W020200618302578146765.jpg
China na Afrika zilianza kuwasiliana mapema miaka elfu kadhaa iliyopita, lakini mpaka mwaka 1949 ilipoasisiwa Jamhuri ya Watu wa China chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, uhusiano kati ya China na Afrika ukaanza kuwa hai. Na katika miongo kadhaa inayofuata, pande hizi mbili zimekuza uhusiano wao kwa kasi sana.

Mwanadiplomasia mwenye uzoefu wa Afrika Kusini Gert Grobler hivi karibuni aliandika makala kwenye tovuti ya Independent Online, akisema uongozi bora wa miaka 100 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC umeweka msingi imara kwa nguvu kubwa na umoja wa taifa la China, na pia kukuza kwa haraka uhusiano wa kirafiki na kiwenzi kati ya China na Afrika. Aliyekuwa balozi wa Misri nchini China Mohamed Noman Galal alipohojiwa na shirika la habari la China Xinhua alisema, CPC imeiwezesha China kuwa kundi la pili kwa nguvu ya kiuchumi duniani, na pia kutoa pendekezo la ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ili kuweka jukwaa kwa washiriki mbalimbali wa pendekezo hilo zikiwemo nchi za Afrika kusaidiana na kushirikiana, ili kunufaisha dunia nzima.

Juhudi za CPC zinaweza kutambuliwa na Afrika, sababu ni kuwa China na Afrika zimefikia makubaliano ya kina katika kuimarisha ushirikiano wa kirafiki. Mwezi Aprili mwaka 1955, mkutano wa Bandung wenye maana ya kihistoria ulifanyika. Kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani zilizotolewa na hayati waziri mkuu wa China Zhou Enlai zilifungua ushirikiano kati ya Kusini na Kusini na uhusiano wa kisasa kati ya China na Afrika.

Baada ya mkutano wa Bandung, China na Afrika zilianza kujenga uhusiano wa kiwenzi wa aina mpya. CPC inaunga mkono sana nchi za Afrika kupambana na ukoloni na kutafuta maendeleo ya kujitegemea, huku vyama mbalimbali vya kisiasa vya Afrika vikijifunza uzoefu na maarifa muhimu kutoka China. Na kutembeleana kwa viongozi wa China na Afrika kulitoa mchango muhimu katika kukuza uhusiano wa kiwenzi kati ya pande hizo mbili.

Tayari ushirikiano kati ya China na Afrika ulikuwa umepata maendeleo, na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC lililozinduliwa mwaka 2000 liliinua uhusiano kati ya pande hizo mbili hadi kwenye kiwango cha juu zaidi, cha sekta nyingi zaidi na cha kimkakati zaidi. Juu ya hilo, mkurugenzi wa idara ya masuala ya China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Humphrey Moshi aliandika makala katika gazeti la Guardian kuwa CPC siku zote inaunga mkono na kuhimiza utaratibu wa pande nyingi, na kuchukulia “usawa na udhati” kama ni msingi wa ushirikiano kati ya China na Afrika, na FOCAC imepata matunda mengi katika miongo miwili iliyopita.

Katibu mkuu wa CPC na rais wa China Xi Jinping amesema mara kadhaa kuwa China inapenda kuona nchi za Afrika zikitumia fursa ya maendeleo ya China na kuhusisha maslahi ya maendeleo ya watu wa China na watu wa Afrika. Wazo lililotolewa naye la “kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja” limekuwa nguzo muhimu ya kukuza maendeleo ya kasi kati ya China na Afrika. Hivi sasa nchi za Afrika zinafanya juu chini kutekeleza ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika------“Afrika tunayoitaka”, kwa hivyo China na Afrika zinatakiwa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kufikia matokeo kabambe na ya kiutendaji. Inatarajiwa kuwa FOCAC na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” vitatoa fursa kwa China na Afrika kuchukua hatua kwa pamoja.

Mwaka huu, mkutano wa 8 wa mawaziri wa FOCAC utafanyika nchini Senegal, ambapo CPC “itasikiliza” tena sauti ya Afrika, kupanga kwa pamoja njia ya kusonga mbele, na kutekeleza kivitendo wazo la “ukweli, uhalisi, ukaribu na udhati” lililotolewa na katibu mkuu Xi juu ya uhusiano kati ya China na Afrika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom