CPA ya Tanzania ni ya kipekee duniani

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,904
Elimu ya Tanzania haiishi vituko.

Ndio maana hatuendelei. Maana flaw kwenye mifumo yetu ya elimu ni mingi mno.

Ndio maana unashangaa, unakua na CPA ya Tanzania, ukitaka kufanya mitihani ya ACCA hupati exemptions kwa kuwa CPA yetu haieleweki.

Kwa wahasibu watanielewa, ni rahisi Tanzania kupata CPA hata kama wewe sio mhasibu na huna taaluma ya uhasibu, ili mradi tu ufaulu mitihani yake.

Yaani unaweza kuwa Certified Public Accountant huku huna academic qualification ya accountancy.

Kwa nchi nyingine kitu cha kwanza kupata CPA ni lazima uwe na academic qualifications then uombe kuwa certified. Nchi nyingine lazima uwe na module hours nyingi sawa na masters ili uwe eligible na CPA.

Huku mwetu unaweza kumaliza form four, ukaanza na atecs hadi CPA.

Sasa imetokea shida ofisini kwetu, wanataka senior accountant, awe na bachelor degree na CPA, aliyepo ana CPA ila hana bachelor degree, ni form four leaver, aliajiriwa kama accounts clerk.

Ikija kigezo cha CPA anayo, ikija kigezo cha bachelor degree hana. Unajiuliza mtu anakuaje certified public accountant huku hana academic qualification ya accountancy?

Ni sawa na mtu kuwa registered electrical engineer huku hajasoma hata certificate ya umeme. Mradi tu amelipia na amefaulu mitihani.

Certification ni profession na ili uwe professional lazima uwe na academic qualifications kwanza. Hapa Bongo unakua certified profession without academic qualifications. Mambo ya hovyo kabisa.

Elimu ya Tanzania haiishi vituko.
 
Mfumo wetu wa elimu kwa ujumla wake nadhani upo nyuma sana ya wakati.

Na mbaya zaidi hakuna jitihada zinazofanyika kuokoa jahazi na ndio maana wasomi wetu wengi haswa wa kuanzia miaka ya tisini mwishoni hadi leo wanashindwa kujiuza kwenye masoko ya ajira nje ya nchi.
 
Japo mimi ni mhasibu ila kiukweli taaluma yetu imeingiliwa. Ukiwa na pesa na muda wa kupitia past papers tayari wewe ni mhasibu aliyeidhinishwa. Pia ninaye classmate yuko Tanapa nilisoma naye akafeli form 4 wakati sisi tunaenda advanced yeye akaanza ATEC.

Leo hii ni mhasibu mzito huko.

Taaluma pekee Tanzania ambayo haijaanza kutiwa najisi ni taaluma ya sheria na udaktari.... Vingine ni ukanjanja tu
 
Japo mm ni mhasibu ila kiukweli taaluma yetu imeingiliwa. Ukiwa na pesa na muda wa kupitia past papers tayari ww ni mhasibu aliyehidhinishwa. Pia ninaye classmate yuko tanapa nilisoma naye akafeli fomu4 wakati si sisi tunaenda advanced yeye a kaanza ATEC.... Leo hii ni mhasibu mzito uko.
Taaluma pekee tz ambayo haijaanza kutiwa najisi ni taaluma ya sheria na udaktari.... Vingine ni ukanjanja tu
Yeah.

Huwezi kupewa leseni ya udaktari kama hujasomea udaktari na hujafanya intern.

Huwezi kupewa mhuri wa uwakili hadi uwe ulisoma sheria na pia ukasoma law school.

Hata wahandisi, huwezi kuwa registered engineer kama huna bachelor ya hiyo fani na ukaandika report ya mradi. Ingekua ni rahisi hivyo hata form four leaver wangeandika tu miradi wakapeleka bodi ya wahandisi wakaitwa engineer.
 
Japo mm ni mhasibu ila kiukweli taaluma yetu imeingiliwa. Ukiwa na pesa na muda wa kupitia past papers tayari ww ni mhasibu aliyehidhinishwa. Pia ninaye classmate yuko tanapa nilisoma naye akafeli fomu4 wakati si sisi tunaenda advanced yeye a kaanza ATEC.... Leo hii ni mhasibu mzito uko.
Taaluma pekee tz ambayo haijaanza kutiwa najisi ni taaluma ya sheria na udaktari.... Vingine ni ukanjanja tu

We subiri tu ipo siku Magufuli atatimua timua woteeee.....watu wanapenda shortcuts saana
 
Unajua maana ya ATEC 1 na ATEC 2 mkuu....soma ingia NBAA halafu soma vigezo vya mtu anayetakiwa kufanya mitihan ya CPA
 
Japo mm ni mhasibu ila kiukweli taaluma yetu imeingiliwa. Ukiwa na pesa na muda wa kupitia past papers tayari ww ni mhasibu aliyehidhinishwa. Pia ninaye classmate yuko tanapa nilisoma naye akafeli fomu4 wakati si sisi tunaenda advanced yeye a kaanza ATEC.... Leo hii ni mhasibu mzito uko.
Taaluma pekee tz ambayo haijaanza kutiwa najisi ni taaluma ya sheria na udaktari.... Vingine ni ukanjanja tu
Wewe si mhasibu bali ni karani wa hesabu, mhasibu mwenye CPA hawezi kuandika hiki ulichoandika, kwani mtu akifeli form four hawezi kurudia na akajiendeleza? Wewe nina wasiwasi hata chuo hukufika
 
Nyie acheni kashfa za kipuuzi. Tena bora NBAA maana huko ACCA experience tu ni sehemu ya qualification za kufanya mitihani yao. ATEC hawasomi failure huu ni uongo! Nenda kaone qualification za kuanza ATEC. Halafu hivi unaweza kufananisha mtu aliyefanya professionals exams zaidi ya 20 na hizi njia zingine?

Hivi mnafikiri mtu alifanya professional exams kuna kitu unamzidi? Tena zaidi technically humsogelei! Edson tutor wa CPA exams kasoma computer science then kasoma kuanzia ATEC hadi CPA unamuweza yule? Unamjua mwl Paul? Yule baada ya form six kapiga ATEC hadi CPA, nafikiri wanaomjua wanajua habari yake.

Vipi Rashidi tutor maarufu wa CPA, yule kasoma Bcom finance na kwa qualification hizo alianzia module B hadi CPA na inshort ufahamu wake umejengwa na professional exams, je unamuweza yule? Weka mbali Mkulo (aliyekuwa waziri wa fedha awamu ya nne) huyu baada ya form six kapiga professional exams.

Dr Makongoro Mahanga naye ni form 4, ATEC to CPA. Reginald Mengi form six to ACCA. Kashonda ambaye vitabu vyake mnatumia hadi vyuo vikuu ni form six to ACCA. Dr Mndolwa aliyekuwa partner PWC ni form six to ACCA. Niendelee?

Inshort professional qualifications kama CPA ni zaidi ya undergraduate degree ndio maana all reputable universities wanaikubali kama direct entry to masters bila kujali umeipata kupitia njia ipi.
 
UKWELI TUPU
 
Mifumo ya elimu ni tofauti. Sisi tunafata mfumo wa elimu ya Uingereza ndio maana kwao unaweza kufanya ACCA kama ukiwashawishi hata kwa work experience kwa kuanzia kwenye mitihani inayofanana na ATEC ukifaulu then unaanza ACCA. Ndio maana wahindi wa bongo wengi huwaoni vyuoni huko. Wakimaliza secondary wanapiga ACCA tu then kutana nae kazini uone. Marekani ndio wana mfumo tofauti wa elimu ambao ni tofauti kabisa na Uingereza. Hata ukiwa na ACCA hupati exemptions kwenye CPA ya Marekani...ni mifumo tu
 
Hii kitu niliwahi bishana na mtu hadi nikampia mawe. Mbona Mainjinia, wanasheria na madaktari hawana huu ujinga
 
Hii kitu niliwahi bishna na mtu hadi nikampia mawe. Mbona Mainjinia, wanasheria na madaktari hawana huu ujinga
Mkuu hupaswi kukariri. Sisi hii elimu tumeletewa tu na wazungu. Huko kwao wanafanya hivi hivi tena ni rahisi zaidi kwa entry qualification tofauti na hapa. Udaktari na shule kama engeneering lazima ukae darasani ni too practical. Lakini hata hiyo sheria wapo watu wanaipiga kwa mitihani tu wanalamba degree nchi za wenzetu labda mnataka NBAA waanze kutoa degree kwa watu walio clear intermediate kama wanavyofanya ACCA ili kuwaridhisha watu kama nyie mnaotaka kuona cheti hicho tu. Hivi mnafikiri mtu aliyepiga professional exams ni short cut au njia rahisi? Basi kila mwenye degree si angekuwa anajibebea tu CPA? Nenda kafanye hiyo CPA uipate ndio utajifunza adabu kidogo.
 
Kwa hiyo una maana kuwa hakuna haja ya academic qualification, bora mtu afanye tu profession exams afaulu awe professional?
 
Kwa hiyo una maana kua hakuna haja ya academic qualification, bora mtu afanye tu profession exams afaulu awe professional?
Hapana. Ukipitia Academic advantage kubwa ni kupata exemption kubwa kufanya CPA au other professional exams inayokufanya utambulike rasmi. Institute of accountancy ya Wales ndio iliyofanya assessment ya CPA ya Tanzania na kushauri watu wanaotoka vyuoni wapunguziwe exemptions ili kiuwezo wawe sawa na waliofanya exams from the scratch. Watu wanaotaka vyuoni control ni ndogo sana ndio maana wakashangaa NBAA kutoa huge exemptions kwa watu ambao haijulikani walichonacho academically. Kwasasa wenye degree za Accountancy wanaanzia intermediate na si final tena. In short usiombe kufanya zaidi ya 20 professional exams ingawa kibongo utasikia wengi wanachukulia kama shortcut lakini struggle yake wanajua waliopitia.
 
Back
Top Bottom