OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Tuwaangazie wahitimu ambao husemekana wanatakiwa kuwa na sifa ya ziada. Naandika makala haya nikiwa najua uwepo wa Bodi nyingi nchini ambazo huwapa sifa za ziada wahitimu mbalimbali wa kada tofauti tofauti.
Wahasibu wakisimamiwa Bodi ya Wahasibu NBAA, ambo kuwa muhasibu mwenye sifa ya ziada utatakiwa kufanya mitihani yao na ukipata CPA (T) Basi inakuwa ni sifa ya ziada kwako kwenye soko la ajira.
Bankers wanasimamiwa na TIOB, ambao hawa hutoa CPB kwa bankers kama watafaulu mitihani yao na kuendelea kuwa mwanachama ili kujiongezea sifa ya ziada
Wagavi wanasimamiwa na PSPTB.
Hizo bodi nilizozitaja hapo zinatoa certification kwa mtu kwanza kufanya mitihani ambayo inahitaji ada, na kama mtu akishindwa basi huwa hawezi kupata cheti husika.
Ziko bodi nyingine ambazo zinahitaji uwe memba tu, kwa kulipa ada ya mwaka, bodi kama ya wahandisi, ERB, au hata hii ya walimu ambayo iliombwa kipindi fulani, najua mtaongeza bodi nyingine ambazo hudai mitihani ili kupata cheti au zile zinazotaka uwe meber tu
Hoja yangu!
Ieleweke kuwa wanafunzi wengi hutegemea mikopo kusoma masomo yao ya elimu ya juu. Bodi ya mikopo humpa mtu mkopo kwa muda ambao yuko chuoni tu! hizo bodi hazihesabiki kama ni sehemu ya chuo, hivyo mtu anayetoka chuoni hutegemea kujisomesha kwenye bodi hizo ili kupata sifa hizo za ziada.
Vitu kama CPA hugharimu si chini ya milioni kwa mitihani yake, CPB halkadhalika, hawa wengine ni zaidi ya laki mbili. Sasa mtu aliyetoka chuoni aliposomeshwa kwa mkopo anatarajia atapata wapi hela ili ajisomeshe kama sio kuongeza gap kati ya wenye nacho na wasio nacho, kwa kuwa wenye nacho wataweza kusoma na kuongeza sifa za ziada huku wasionacho wakisubiri ajira ili watumie mishahara kujipa sifa ya ziada, wakati wao wanasubiri kazi zinasema CPA is an added advantage.
Kitawafanya wasote mtaani huku wanye CPA wakipata mashavu kirahisi
Nadhani hii ni sababu nyingine ya kupunguzana
USHAURI:
Hii inaonyesha degree haitoshi kumfanya mtu aweze kuajiriwa, Je kwa nini mitihani ambayo wanaifanya katika bodi mbalimbali isiongezwe kwenye mtaala wa elimu ya Chuo Kikuu ili mtu akihitimu shahada yake anakuwa tayari yuko na sifa zote, ili kwenye soko la ajira mchuano uwe fair?
Signed!
OEDIPUS