#COVID19 Tovuti /Kanzidata ya waliochanjwa iwepo.

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,365
7,608
Nietafakari umuhimu wa kuwa na Kanzidata au Tovuti yenye taarifa za waliochanjwa chanjo ya UVIKO19.

Kwa kuwa chanjo Ni Hiari na si Lazima Kuna Ambao watachanjwa na wengine hawatachanjwa.

Kwenye familia Kuna maamuzi ya kifamilia lakini pia ya kibinafsi. Kuna Uwezekano wa kusalitiana. Endapo Familia tumeamua Wote Kuchanjwa, Tovuti/Kanzidata itatusaidia kujua kama kweli Wote tumechanjwa. Na pia kama tumeamua tusichanjwe itasaidia kujua aliyechanjwa kwa Siri.

Kuna watu Mungu katujalia Kinga asili (Natural Immunity) ya Magonjwa ambukizi na yasiyoambukizi na tusingependa kuona ugeni katika miili Yetu unaweza kuleta mabadiliko katika Kinga zetu tulizokirimiwa na Muumba. Mshirika wa tendo la Ndoa akichanjwa kwa Siri inaweza kuleta athari kwa mwenzake.

Naomba Serikali Yetu iwaweke kwenye DB (KD) au Tovuti wachanjwa Wote Ili kuhamasisha uchanjwaji.

Usimlazimishe mtu, Chanjwa/Usichanjwe kwa Hiari!
 
Back
Top Bottom