COVID19 Tanzania: Mambo ambayo Wizara ya Afya inapaswa kufanya

Winter99

New Member
Apr 16, 2020
1
1
Si jambo jipya tena, maambukizi ya corona Tanzania yapo kwa kasi kubwa sana kwenye jamii, pia tumeendelea kuona vifo vikiongezeka siku hadi siku.

Tuna maswali mengi sana kama watanzania juu ya mikakati ya wizara ya Afya ya Tanzania kukabiliana na Tatizo la Corona. Je sekta ya Afya imejiandaa vipi kukabiliana na ongezeko la wagonjwa wanaotakiwa kulazwa.

Ni dhahiri kwa tafiti nyingi ni asilimia 20% tu ya wagonjwa watakaopata maambukizi ya corona watahitaji kulazwa, tukifikiri kwa nadharia ya kimahesabu tukasema tumefanya hatua nzuri za kinga watu laki tano tu Dar es salaam wakapata maambukizi kwa kipindi cha miezi mitatu wagonjwa ambao watahitaji kulazwa ni Laki moja kwa Dar es salaam tu. Je tuna vitanda vingapi vya kulaza wagonjwa jijini dar es salaam?

Hospitali mpaka sasa iliotengwa kwa tatizo hili ni moja tu, Je, hii ni sahihi? Je, tunawafanyakazi wa afya wa kutosha? Je tunavifaa tiba vya kutosha? Je tunauwezo gani wa kupima wagonjwa? Mimi kama daktari sina haya majibu, je nifanyaje kazi bila mipango thabiti.

Corona ni vita, ni askari gani anaenda vitani bila mipango. Tumezoea longolongo sana watanzania katika hili hatupaswi kuwa na kigugumizi, je Rais Nyerere alikuwa na kigugumizi dhidi ya Iddi Amini, la hasha.

Kama nilivyosema kama Daktari na mtumishi wa Afya nina maswali Mengi sana, na nitaendelea kuuliza. Lakini kuna mambo ambayo majibu tunayo kwa muda mrefu kuhusu hili tatizo. Ningependa kushauri Mambo saba ya Muhimu kabisa ambayo wizara ya Afya inabidi iyafanye kukabiliana na tatizo hili.

1. Kuongeza uwezo wa Kupima virusi hivi: Hili halikwepeki, linihitaji fedha nyingi za vipimo na logistics, Kadiri uwezo wako wa kupima ukiongezeka ndio kadiri unavyoweza kugundua wagonjwa wengi na kushauri self isolation kwa positive cases/Matibabu ya nyumbani na kulaza wale wanaumwa sana.

Tanzania ina machine 200 za gene Xpert, na zipo kwenye mikoa yote, kinachohitajika ni kununua cartridges za COVID-19, na hii ndo njia wanayotumia South Africa kupima watu wengi. Ndio ni gharama, lakini kama tumenunua ndege zetu wanyewe kwa fedha zetu hatuwezi kushindwa. Kwa makadirio cartridge moja ni $19, haifiki hata robo ya per diem ya mbunge akiwa kwenye vikao.

2. Kuongeza sehemu za dharura za kutibu wagonjwa wa corona: Hatutaweza kuongeza hospitali, hatuna fedha na muda huo kwa sasa, lakini haimaanishi kwamba hatuwezi kubadilisha majengo na kumbi tulizonazo na kufanya kuwa vituo vya kutibu. Ukweli ni kwamba ugonjwa huu mpaka sasa hauna tima kwa maana kwamba utapewa dawa na itakuponyesha.

Tatizo kubwa la ugonjwa huu ni kuathiri mapafu, na kwakweli ni pneumonia ya muda mrefu. Wagonjwa wanaohitajika kulazwa ni wale wanaopata shida ya kupumua. Na kati ya hawa wengi huwa ukiwapa high flow oxygen wanaendelea vizuri, na wachache hushindwa kabisa kupumua na uhitaji mashine za kupumulia ambo matokeo yake sio mazuri kwa wagonjwa wengi.

Hivyo basi matibabu ya msingi kwa sasa ni supportive; hivyo tunahitaji vitu vichache tu yaani chumba cha wagonjwa, vitanda, vifaa vya kumonitor wagonjwa na oxygen support. Tumechewa kujiandaa, tusichelewe zaidi.

3. Mkakati madhubuti wa kuwakinga watu wenye umri mkubwa na wenye magonjwa sugu: Kwa uzoefu mfupi tulionao mpaka sasa wa kutibu wagonjwa wenye tatizo hili, wengi wanaopata madhara zaidi ni wenye umri mkubwa na wenye magonjwa sugu ikiwemo kisukari, magonjwa ya moyo na figo, magonjwa sugu ya kifua, shinikizo la damu na unene uliopitiliza.

Ndio nchi yetu imeamua kutofanya lockdown, lakini tunauwezo wa kulinda baadhi ya watu, hasa waliotajwa hapo juu. Serikali inauwezo wa kutoa likizo ya lazima kwa makundi hayo au wafanye kazi wakiwa nyumbani kama inawezekana.

Wizara inaweza ikaja na muongozo wa jinsi vijana wanavyoweza kuwahudumia na kujitenga na wazee wao. Ndio kujitenga haimaanishi usiwahudumie, huu ndo muda wa vijana kuonesha upendo mkubwa kwa wazazi.

Naamini hili linaweza kufanyika katika level za kifamilia, lakini linhitaji muongozo. Jamani wataalamu wa public health mko wapi?
 
Mleta mada fungua hospital yako ya corona iite corona hospital halafu yafanyie kazi hayo mawazo yako kwenye hospitali yako ingependeza zaidi
 
Back
Top Bottom