#COVID-19: Tuwajibishane

Sasa P rais wetu anapambania wapi? Sisi tulianza kuripoti case ya kwanza nyuma ya uganda. Lakini elimu na mwongozo alioutoa Mseven umeifanya Uganda kuwa nchi pekee EA ambayo bado haijapata.mtu aliyekufa kwa covid 19. Hata hivyo maambulizi yanabaki kuwa chini kuliko nchi nyingine za EA.

Sasa je tudharau uwajibikaji wa m7? Ona Rwanda Paul is doing very great na ataanza kuingiza wagen very soon see where we are as a nation number of infected people is increasing by double digits.

Do ypu still think it's ok?
Hata Rwanda haina vifo
 
Zitto, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulauniana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane. Huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united and fight as one.

P

Hii tabia ya kusubilia mpaka mambo yanaharibika Ndio tuonyeshe ushirikiano na mshikamano nafikiri sio sahihi. Nasema sio sahihi kwa sababu kabla mambo hayajafika kama yalivyo watu wengi sana wenye mlengo tofauti tofauti walijaribu kutoa mawazo yao namna tofauti tofauti ya kukabiliana na hili janga lakini walipuuzwa sana na Leo ndio tunaona matokeo ya hayo mapuuzo na sasa tunashauriwa tuungane!

Lakini pia jaribu kuwaza kwamba uko barabarani unasimishwa na trafiki wa usalama anakutahadharisha kwamba upunguze mwendo mbele kuna daraja limevunjika lakini wewe kwa jeuri yako na kujiona na kumdharau yule Askari unaamua kutotii ushauri wake na unaamua kuongeza mwendo na matokeo yake unatumbukia darajani.. Mungu saidia ukanusurika na kifo,huoni kuwa ni sahihi kumwajibisha huyo dereva kwa kupuuza warning ️?

Muda tunaendelea kuungana kwenye haya mapambano lakini pia ni muhimu kuwalaumu wanaotuongoza kuwa sehemu ya kuongezeka kwa hili tatizo.hawakuwa sahihi kuchukua maamuzi ya kupuuza ushauri wa watu wengine maana kama ni kuungana kungekuwa na thamani zaidi pale hata wale wote waliotoa ushauri toka mwanzo pia wangethaminiwa.
 
Watu wote tungelikuwa vigilant kama Zito, labda hali ingelibadilika
Upo sahihi
Ilipashwa watumie hata radio za uchochoroni wajirekodi kuwasaidia wananchi namna ya kupambana na hii kitu
Hali ilivyo serikali inaliangamiza Taifa kwa makusudi
Naomba wabunge wote wa sisiem tuuuu waende kwenye mwombezi ya Waziri Mkuu
 
Sasa atoke Chato aje wapi? Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Dar, Mtwara, Iringa au? kama anaweza kuwepo sehemu moja kwa wakati mmoja basi ata Chato sio shida.

Muhimu strategies ziwe na mrejesho chanya.
Mkuu IQ ya mtu na kinyume chake haipimwi maabara! Rais ni muajiriwa hivyo anakituo chake cha kazi ndiko anakotakiwa kuwepo!
 
Ndugu yangu, hii vita haipigani kama vita ya msituni ambayo adui anajulikana na kuonekana, you are fighting an invisible killer. Rais anaweza kuwa in contact na idara zote na watumishi wote 24/7.

Hoja ya yeye kuwa kwenye camera kila saa na kila dakika haina mashiko, haimaanishi kama rais akionekana ndio tutashinda vita au tutashindwa vita ya COVID-19. Nini maana ya waziri mkuu, nini maana ya waziri wa afya, nini maana ya mganga mkuu na wataalamu wote wa magonjwa nchini?
Kuna controversy nyingi sana wakati huu, ukimya wa mkuu hausaidii zaidi ya kuongeza panic.

Ilipaswa wakati huu ajitokeze ili kutupa wananchi uniting factor na motisha ya kuvuka kipindi hiki kigumu.

Invisible enemy huyo anapiganwa dunia nzima ina maana Trump na Kenyatta hawana mawaziri? Mpka wajitokeze kila wakati kutoa mrejesho.

Sasa makonda kasema lake, naibu waziri ndugulile lake, spika naye ana lake..... Hii chaos isingetokea kma Mkuu angetoa kauli yake! Hyo coordination unayosema iko wapi? Kungekua na hizi controversy tunazoona?

Case zinaongezeka, maybe maombi pekee hayajasaidia..... What's plan B? Big man bado haonekani, panic inazidi, then huoni kuna haja ya yeye kujitokeza kutoa way forward ili kutuepusha na hizi vutu nkuvute za viongozi wa kisiasa?
 
Sasa P rais wetu anapambania wapi? Sisi tulianza kuripoti case ya kwanza nyuma ya uganda. Lakini elimu na mwongozo alioutoa Mseven umeifanya Uganda kuwa nchi pekee EA ambayo bado haijapata.mtu aliyekufa kwa covid 19. Hata hivyo maambulizi yanabaki kuwa chini kuliko nchi nyingine za EA.

Sasa je tudharau uwajibikaji wa m7? Ona Rwanda Paul is doing very great na ataanza kuingiza wagen very soon see where we are as a nation number of infected people is increasing by double digits.

Do ypu still think it's ok?
Mkuu Gf Son Win, uhai umeumbwa na kifo pia kimeumbwa. Kila anayekufa ndio siku yake imefika, hivyo Uganda na Rwanda, hakuna vifo sio kwasababu ya hatua zilifuatwa na Kagame na Museveni ndio zimezuia vifo, vifo ni kazi ya Mungu na havizuiliki, tena hata hapa Tanzania ni kazi tuu ya Mungu, WHO wali predicts vifo 300, within the 1st month, lakini sisi kwetu vimetokea vifo 10 tuu!, ni ni kazi ya Mungu.
P
 
Mkuu Mhe. Zitto, kwenye hili, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulauniana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane. Huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united and fight as one.

P
Hivi sarcastic kwa Kiswahili ni nini vile... Kebehi au... Paskali unaongoza humu jukwaani. Wasiokusoma watakushambulia.
 
Hivi zile trilioni zaidi ya 400 za makinikia hatujalipwa bado?
 
Mkuu si ungejipa muda ukaelewa maana ya lockdown kwanza?

Lockdown haina maana ya watu kufungiwa vyumbani. Nchi zilizo kwenye lockdown, wakulima na shughuli muhimu zote zinaendelea wala hakuna watu wanaoteseka kwa kukosa chakula. Hizi tafsiri zenu mnapeana wapi?

Kabla ya ugonjwa kuingia serikali ilipaswa:

1. Kuzuia ndege na wasafiri tokea nchi zilizo kuwa na maambukizi.
2. Kuwaweka wageni wote tokea nje quarantine kwa siku 14 kabla ya kuwaruhusu kuingia nchini.
3. Kufunga mipaka kwa watu kupita (abiria) kasoro mizigo (kama kwingine wafanyavyo).

Hawakufanya hayo kwa uzembe wao japo waliambiwa sana. Ni kama wanavyoambiwa sasa hivi nini wafanye na bado hawachukui hatua na ugonjwa unazidi kusambaa.

Sasa ndugu yangu hapa unazungumzia lockdown au controlled migration. Huwezi kuzuia watu wasije nchini halafu hapo hapo unaruhusu watu wakalime na wakazalishe bidhaa viwandani. Hiyo sio lockdown kina Zitto &Co wanahubiri. Wenzako wanataka watu wafungiwe ndani kama kuku na wapewe Tshs 300,000 za kujikimu. Watanzania hayo hawayawezi, kama walivyoshidiwa South Africa, Ghana au hata USA, lockdown is a psychological time bomb.

Watanzania mnapenda kusikiliza wanasiasa ambao wengine sio wataalamu wa mambo wanayoyaongelea, leo hii nchi kama UK, Spain, France, na Italy wana mazao shambani ambayo yanakaribia muda wa kuvunwa na wavunaji hakuna, kisa nini, lockdown. Matokeo yake miezi michache ijayo nchi ambazo walikuwa wanagombea PPE na wengine kuibiana wataanza kupigana vikumbo wakinyanyana chakula.

Vitayetu ya corona inapigana kwa silaa ndogo sana na ya gharama nafuu ambayo ni BARAKOA (mask). Angalia wenzetu wa Czech Republic walivyofanikiwa kwa kutumia masks.

Strict measures—including compulsory face masks—help Czechs get grip on COVID-19 - Atlantic Council
 
Mkuu umesoma bandiko langu kuelewa?

1. Bandiko langu limegawanywa sehemu mbili kuonyesha nini serikali haikufanya au haifanyi.

2. Points zile tatu ambazo serikali haikufanya zingezuia ugonjwa kuingia. Hizo hazihusiani na lockdown.

3. Nimeandika kifupi kukuonyesha kuwa lockdown si kufungiwa watu vyumbani wala watu kuhangaika ba njaa.

Labda angalia hapa lockdown ni nini:

IMG_20200416_173646_378.jpg
 
Pascal Mayalla rafiki acha utoto, unisamehe! Utapambanaje hata gloves, mask, sabuni na maji huna? Mwenye kutoa vitu hivyo kafunga store haonekani?

Mna unite kivipi ebu twambie. Una unite wakati kauli anayo mtu mmoja hataki ushauri, how do you offer assistance? Kupanda kwenye pick up na msalaba kupita mitaani unaimba mapambio ya Bwana Yesu?

Shauri mtu afanyeje. Huyu Jiwe anaua watanzania and now we are going into millions some few days/weeks to come

Well said mkuu,! Anyone here defending the government on their pandemic handling needs to have their head checked out.
 
Zitto, kwenye hili, sisi tuliamua kila nchi iendeshe mapambano kivyake vyake bila kuiga, kama hao marais wengine wanaendesha mapambano kwa kuonekana sio wao.

Kwanini Magufuli awaige wakati kuna njia nyingi za kuendesha mapambano na sio lazima mpaka kila mtu aone, issue ni kuona au kupambana?

P
"sisi tuliamua " wewe na nani? na ni lini mlifanya hayo maamuzi? Nani aliwateua na kwa utaratibu gani?
Jamaàa sometimes unaandika pumba sana nimewasiliana najamiiforums wafikirie kukuondolea platinum membership hata kama umelipia.
Manake sio kwa mapumba unayoandika
 
Mkuu Mhe. Zitto, kwenye hili, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulaumiana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane. Huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united as one and fight as one unified army against one common enemy.

Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
P
How can we stand United as one while the ones who were suppose to lead and unite us against the disease are no where to be seen in the scene?
No 1 has isolated him self in his village.
No 2 is no where to be seen.
How can this be possible if we are realy serious in fighting against this pandemic
 
Kipi bora zaidi kati ya rais kubaki Chatto ambako ni salama na kuongoza mapambano remotely au aje mstari wa mbele na ku risk kuambukizwa!

Watu tumeisha sikia the consequences za Corona kwa watu wenye underlying symptoms za magonjwa mengine that has to do with uwezo wa mwili ku produce antibodies against Corona virus, do we have to kumu exposure Amiri jeshi Mkuu wetu to such risks ili tuu watu waone?.

No, Amiri Jeshi Mkuu wetu abakie mahali salama for as long as it takes.

P
Kwa hiyo unashauri kiongozi kuwa mstari wa nyuma wakati anaishi kwa kugharamiwa na kodi za wananchi.are you realy serious ?unakijua vizuri kiapo cha Rais ?
 
Sasa atoke Chato aje wapi? Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Dar, Mtwara, Iringa au? kama anaweza kuwepo sehemu moja kwa wakati mmoja basi ata Chato sio shida.

Muhimu strategies ziwe na mrejesho chanya.
Kama ingekuwa hivyo basi kungekuwa hakuna haja ya kujenga ikulu
 
Kuna controversy nyingi sana wakati huu, ukimya wa mkuu hausaidii zaidi ya kuongeza panic.

Ilipaswa wakati huu ajitokeze ili kutupa wananchi uniting factor na motisha ya kuvuka kipindi hiki kigumu.

Invisible enemy huyo anapiganwa dunia nzima ina maana Trump na Kenyatta hawana mawaziri? Mpka wajitokeze kila wakati kutoa mrejesho.

Sasa makonda kasema lake, naibu waziri ndugulile lake, spika naye ana lake..... Hii chaos isingetokea kma Mkuu angetoa kauli yake! Hyo coordination unayosema iko wapi? Kungekua na hizi controversy tunazoona?

Case zinaongezeka, maybe maombi pekee hayajasaidia..... What's plan B? Big man bado haonekani, panic inazidi, then huoni kuna haja ya yeye kujitokeza kutoa way forward ili kutuepusha na hizi vutu nkuvute za viongozi wa kisiasa?

Sorry to differ with you, Lakini Tanzania sio North Korea kwamba kiongozi asipoonekana hadharani au kutajwa kwenye TV basi nchi inatetemeka na watu kuulizana kuna nini. We are mature than that, kitendo cha sisi to keep our cool while the other in the region wanamalizana Kwa vita, inaonyesha ukomavu wetu.

Hivi nikuulize swali toka Trump amekuwa anasimama na kuongea na waandishi wa habari, kuna cha maana umeokota au ndio kutukana watu your fake na kusema Chinese virus. Hata huyo Kenyatta, mara ya mwisho ulimuona lini jukwaani tena anaingilia maamuzi ya madaktari na washauri wa mambo ya kiafya? Lakini huku kwetu watu wanataka wamuone Magufuli kila kona, huku anaongea mambo kuingilia wataalamu ili watu wapate cha kusema. Hao wengine sijui wakuu wa mikoa, mawaziri kila mtu anaongea to their capacity, wote hao wanawashauri wao wa mambo ya afya, iwe mkoa au wizara.
 
Ni ushamba wa wenu kutokujuwa serikali inafanyaje kazi, sio lazima mtu awe sehumu fulani ndio kazi inaendelea.

Acha kutetea upumbavu! Kiongozi gani anayeenda mapumzikoni wakati wa janga??mnavyomtetea sijui anawalipa nini? Na mwenzako hapo juu eti ni safe yeye kukaa Chato...huyo prince Charles mwenyewe ali test postive ndio itakua yeye???
 
Back
Top Bottom