Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala fikirishi, elimishi na hamasishi uzalendo za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo hutolewa kwa mfumo wa maswali, makala ya leo ni kuhusu utoaji wa taarifa za Corona, COVID-19: Nani Mkweli Kati ya Serikali Yetu na Ubalozi wa Marekani?!. Jee Tanzania Tunawaogopa Sana Wamarekani?!. Kwanini Wamarekani Waseme Uongo Mkubwa kama Huu halafu Waachwe tuu hivi hivi?!.
Nimesoma with disbelief hii taarifa ya leo ya ubalozi wa Marekani, kwanini ubalozi unatoa taarifa ya uongo kuhusu hali ya COVID-19 nchini kwetu na wanaachwa hivi hivi?!, Jee hawa Wamarekani tunawaogopa?.
Taarifa yenyewe inapatikana hapa kwa wale wa kimombo
Tanzania International Travel Information
Kama rais Magufuli juzi kasema Corona imepungua, jana Waziri Ummy kathibitisha kwa data, leo Marekani inaibuka na kesema hizo taarifa zinazotolewa na viongozi wetu ni taarifa za uongo, na kutusingizia serikali yetu inaficha data, nani mkweli na nani muongo?.
Kwanini Wamarekani waseme uongo waachwe?!. Kama serikali yetu itawanyamazia hawa Wamarekani bila kuwaonya au kuwachukulia hatua yoyote kwa uongo wao, then waelewa wataelewa nani ni muongo kweli na nani ni mkweli, na pia huu utakuwa ni uthibitisho kuwa Mmarekani tunamuogopa, hata utusingizie uongo gani sisi, tunanyamaza tuu!.
Tanzania na rais wetu Magufuli na serikali yetu tumekuwa tukisingiziwa uongo mwingi na sometimes hata kutukanwa na kudhalilishwa na media za nje, lakini tunanyamaza ama kwa kuwapuuza, ama kwasababu Tanzania kwa sasa hatuna watu wenye the capacity kujibu tuhuma kama za The Economist, lakini enzi za Kikwete, aliposingiziwa na balozi wa Marekani kuwa amehongwa suti, Ikulu yetu haikunyamaza, baada ya kupiga kelele humu, Marekani walikanusha.
Lakini sasa leo rais wetu anasema ukweli, kesho Waziri wetu wa Afya anasema kweli, halafu kesho yake, ubalozi uliopo hapa hapa Tanzania unaibuka na taarifa za uongo kuonyesha serikali yetu inaficha ukweli!, ukificha ukweli maana yake unachoripiti ni uongo!. Sasa huu uongo unaosemwa nchini, na ubalozi fulani, usipokanushwa, itaamaanisha ama tunawaogopa Wamarekani, ama tunachoelezwa na serikali yetu ni .. na wanayoyasema Wamarekani ndio ukweli wenyewe, ilaikitokea hawa Wamarekani ni waongo, swali linabaki "Hivi hawa Wamarekani wanatutakia nini?!. Kwanini watutungie uongo na kuueneza dunia nzima?. What is their motive behind and what do they wish to achieve?.
Paskali
Hili wala siyo jambo kubwa kivile; ni suala la Wamarekani kujihami... labda tungewauliza data zao labda wao wana namna nyingine ya kujua idadi ya wagonjwa nchini nje ya taratibu za serikali...