COVID-19 na ukubwa wa tozo zilizopitishwa Bungeni haviendani, uzalishaji umeshuka

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Unapokabiliwa na ugonjwa Kama covid 19 unawafanya wananchi wako wengi kutumia muda wao kwenye mambo yafuatayo;

1. Kuhudumia wagonjwa, Kuchukua taadhari za afya ikiwemo kuacha kufanya kazi kwa waliopo kwenye majukumu yanayohitaji kukutana na watu wengi, Kutumia muda mwingi kwenye nyumba za ibada kumwomba Mungu atujaalie afya njema.

Kama nguvu kazi ya Taifa itajikita kwenye yaliyoainishwa hapo juu Basi itawalazimu kutumia kiasi walichonacho (akiba) zaidi kuliko kuzalisha. Kwa uwezo wetu wa kiuchumi hakuna watu wenye akiba ya mwezi tunaishi kwa pato la siku. Lakini pia hakuna anayetaka kufa hivyo tutaendelea na harakati za maisha.

Kwa nchi zote Duniani hakuna miradi mikubwa ya maendeleo inayotegemea wananchi inayofanyika kwa sababu wananchi kwa kipindi hiki uchumi wao ni mbovu Sana. Mfano sekta ya Utalii, baada ya serikali kuripoti kesi nyingi za kirusi Delta hasa kaskazini utalii umeporomoka. Wale waliokuwa wanategemea utalii wapo nyumbani wakitegemea fedha kutoka kwa watu walio kwenye sekta nyingine ambazo azijaathirika Sana. Wakati huo huo wakati sekta zikiathirika na sisi tunaona hivyo mipango ya serikali nikuwafanya wananchi wasiweze kutumiana fedha kutokana na too ya line na tozo ya uzalendo.

Kibaya zaidi haya yanafanywa na serikali moja, Waziri wa fedha anatoa katazo la watu kukusanyika ambalo lina impact kwenye biashara na uchumi kwa ujumla lakini Waziri wa fedha anatoka na tamko na sheria kali ya Kodi. Tunawaza juu ya Watanzania au tunawaza juu ya vitu? Je, tunawahitaji Hawa Watanzania kesho?

Kibaya zaidi Spika anatoka adharani nakuwasimanga kwa kejeli wananchi kwamba yeye na wawakilishi wa wananchi bungeni wamepitisha sheria na lazima watu walipe too wakajenge barabara. Inamaana afya za Watanzania ambao hawana gesi wahospitalini siyo kipaombele Bali kipaombele ni barabara, umemee? For 60 yrs Hali ilokuwa shwari hatukuja na hizi too Leo tumekuja nazo za kazi gani?

Lakini ukiangalia mjadala bungeni utagundua hakuna tozo Wala Kodi iliyopelekwa kwenye sekta Kama Utalii kwa sababu wanaamini sekta hiyo imeathiriwa na covid- 19, endapo tunaona wazungu hawapaswi kulipishwa Kodi kubwa ili tuwavutie je Nani muhimu? Mtanzania au Mgeni?

Niombe serikali mnapofanya haya mambo kaeni pamoja. Katibu Mkuu kiongozi aliwahi kusema kwamba serikali inakosa coodination, nashangaa yeye ndio coodinator lakini mambo yanakwenda vibaya kuliko hata hapo awali.

Covid na tozo havikai pamoja, ndo maana tunaomba misaada means Hali si shwari. Kama serikali inaomba misaada inaiweka hazina badala ishushwe ikanunue mitungi ya gesi au kama wao barabara ni muhimu Basi chukueni fedha za covid mkajengeee hiyo miradi yenu mtuachie Uhuru wakutumia miamala ya simu kuwasaidia ndugu zetu elfu kumi japo za chakula kipindi hiki Cha madhila ya covid
 
Tumezaliqa ili tukafw Kwa ufalq wetu Tanzania, ndio maana bungen waliondoa vichwa wakabaki maboha
 
Hawawezi kukuelewa kwa sasa! Mobile money itakapo poromoka na kufa, watakuja na ngonjera zao za kutukejeli. WANAUWA UCHUMI KWA NGUVU ZAO.
 
Back
Top Bottom