COVID-19 na SAIKOLOJIA: Dr. Albanie Marcossy, PhD.

Phb_himself

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
221
184
Mshauri mmoja wa mambo ya saikolokjia na jamii aliyefuatilia mlipuko wa Corona unaosababishwa na Virusi vya. Covid-19 ameshauri ifuatavyo:

1. Jitenge mwenyewe usipate taarifa mbaya za ugonjwa huu kila mara (kwa kuwa mambo mengi unayohitaji kujua juu ya Corona umeshayajua, yaliyobaki ni marudio tu)

2. Usitafute habari za vifo. Huu sio mchezo wa mpira kwamba unataka kujua matokeo: mumeshinda ngapi au mmefungwa.

3. Usitafute habari za nyongeza kwenye mitandao. Zitanyong’onyeza hali yako ya afya ya akili. Kujua namna ugonjwa unavyoathiri kunakuongezea Msongo wa mawazo na woga.

4. Epuka kutuma ujumbe wenye taarifa mbaya ya corona. Wengine wana udhaifu mkubwa kwenye uwezo wao kuhimili habari mbaya (baadala ya kuwasaidia unaweza kuwasababishia madhara ikiwemo msongo wa mawazo).

5. Ikiwezekana kaa nyumbani na usikilize muziki kwa sauti laini katika hali tulivu. Tafuta michezo ya kuburidisha watoto na familia. Simulia hadithi, angalia sinema au hata vipindi vya ucheshi. Usiache kuzungumzia mipango yako ya baadae na ya kifamilia.

6. Tunza nidhamu nyumbani kwako haswa ya utaratibu wa usafi kuepuka maambukizi. Nawa mikono kwa sabuni mara kwa mara na uwafuatilie wote nyumbani wafanye hivyo.

7. Kuwa na mtazamo chanya kunaimarisha hali ya kinga ya mwili huku mtazamo hasi unaweza kuthangia msongo wa mawazo na kuharibu kinga ya mwili wako. Pia mtazamo wako chanya utawajengea matumaini unaoishi nao nyumbani kwako.

La muhimu zaidi ni kuamini kuwa hata hili litapita! Na kwamba wewe na jamii yako mtakuwa salama.

IBADA : SALA NA KUSOMA MAANDIKO MATAKATIFU PIA NYUMBANI KWAKO NI MUHIMU KUONDOA STRESS. KUMBUKA HUJAWAHI KUJILETA WEWE DUNIANI, NI KUDRA TU ZA MWENYEZI. JIKABIDHI KWAKE, NA MWOMBE ULINZI, MWAMBIE YEYE AJUAYE MWANZO WAKO, NDIYE PEKEE AKAHUSIKE NA HATMA YAKO HAPA DUNIANI.

# Stop panic, StayPositive
#StaySafe, protect your family and others!!
 
Back
Top Bottom