COVID 19: Mko wapi wataalamu wetu, Wanasayansi wetu wa Afrika?

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Shime kwa wahudumu na watoa huduma wa afya wote katika vituo vya kutolea tiba Nchini na dunia nzima kwa ujumla. Kama sisi tuko kwenye hatari ya kupata mambukizi mitaani, ni dhahiri wao wako kwenye hatari mara nyingi zaidi kuliko sisi. Mungu aendelee kuwalinda na kutulinda sisi

Nikirudi kwenye mada, najaribu kujiuliza katika kupigana vita hii ya corona virus mbona hatuwasikii wataalamu wa madawa wa Afrika wakijihangaisha na kutafuta tiba au kinga ya virusi hawa?

Macho na Masikio tumeviacha visikilizie tambo za chanjo na dawa kutoka huko mataifa makubwa. Afrika kama bara kuna mchanganyiko wa watu mbalimbali wenye tamaduni mbalimbali ambao tumerithi vitu mbalimbali.

Kwa karne zote kabla ya ukoloni kuja Afrika Babu zetu walikuwa wanaumwa na kujitibu wenyewe na ushahidi upo waliishi miaka mingi kuliko hata miaka tunayoishi sisi.

Imekuwa ni kawaida dawa zetu kuzipa majina ya "local medicine" (dawa za kienyeji) Tafsri ambayo kwa maoni yangu naona si sahihi. Tafsri ya kutudogosha

Sasa hivi tunao wasomi wengi sana katika bara hili. Wanajua njia zote za kufanya tafiti na kufanya kitu kitambulike na kukirasimisha.

Kama Afrika, tunamchango gani katika kutafuta tiba na kinga za magonjwa mbalimbali yanayotukumba? Kwa miaka yote hiyo watafiti katika magonjwa wameshindwa kutoa ushawishi kwa serikali zao kufadhili tafiti zao ili angalau watu wetu watibiwe kwa tiba zetu wenyewe?

Leo Tanzania tunaendesha maombi ya Kitaifa kuliombea Taifa dhidi ya janga la corona. Kwanini juhudi kama hizi zisionyeshwe katika kuunga juhudi za wataalamu wetu? Hatukatai maombi ila hatuna budi kukubali ukweli kwamba maombi bila juhudi ni sawa na kelele tu! Huwezi kubweteka halafu ukajipa matumaini eti Mungu atakusaidia kupitia maombi yako tu! Hii miujiza haipo!

Wakristo wanajua kwamba Yesu mahali fulani alisema "ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa"...Sio mtaalamu wa theolojia, ila naamini hapa alilenga kuwahimiza watu kujishughulisha wanapokuwa na hitaji fulani. Kufanya maombi tu bila kufanya juhudi za kutumia vipawa alivyotujalia haya yatakuwa makelele tu

Dawa zetu zinaitwa za kienyeji kwasababu tumebweteka na wasomi wetu wamekubali kubaki kuamini vitu vya kimagharibi badala ya kupigania kufanyia tafiti dawa zetu ili ziwe rasmi. Tunajua figisu za wamagharibi katika masoko lakini mi naamini tukiweka juhudi ipo siku tutafanikiwa tu! KAMA BARA NASEMA HATUJAAMUA BADO! WASOMI WAMELALA!

Pa kuanzia ni hapa kwenye corona! Tusibeze sana dawa zetu za asili. Tuzijaribu, tufanye tafiti, tuunganishe tamaduni za kimatibabu za jamii hii na ile kwa magonjwa yanayofanana. Tuangalie wahaya walijitibu vipi homa? Wandengereko walitumia nini? Kule Uganda, Rwanda, Burudi na Kenya walijitibu vipi magonjwa ya mafua, kikohozi, kifua enzi hizo? Tupeleke maabara mizizi. majani, na kila aina ya dawa walizotumia na zinazosemekana kuleta matokeo. Tuboreshe tunapoona panafaa kuboresha kulingana na wakati. Lazima tutatoka na kitu ambacho hakitakuwa na jina bovu la kienyeji!. Hata hizo dawa zao ni matokeo ya vitu mbalimbali vilivyokusanywa kulingana na matumizi katika jamii zao. Tufanyie tafiti mimea tuliyonayo inayosemekana ni dawa. tuanze kujitibu wenyewe. Tusione sifa kuitwa wasomi wakati hatuna cha kujivunia kama waafrika

Bila ya hivi hawa wanaosemekana kuweka vitu wanavyovijua wao kwenye dawa zao kwa malengo yao wanayoyajua wataendelea kufanya hivyo na watafikia malengo yao tu.

Yangu ni hayo tu karibuni tujadili kwa pamoja
 
Saiv ndo naona kuwa zile laboratory zinazojengwa mashuleni hazina faida Bali zinatumika ili tusio na akili tusiweze kufaulu tu na sio kumjenga mwanafunzi aweze kufanya tafiti za kimaabara bila kuchungulia maabara za nchi zilizoendelea.

Nakumbuka nilikula D ya biology kisa practical ilinipiga chenga
 
Afrika itafanikiwa kutumia akili zilizopo vichwani mwa wasomi wetu endapo tu suala la ubinafsi litaisha.
 
Shime kwa wahudumu na watoa huduma wa afya wote katika vituo vya kutolea tiba Nchini na dunia nzima kwa ujumla. Kama sisi tuko kwenye hatari ya kupata mambukizi mitaani, ni dhahiri wao wako kwenye hatari mara nyingi zaidi kuliko sisi. Mungu aendelee kuwalinda na kutulinda sisi

Nikirudi kwenye mada, najaribu kujiuliza katika kupigana vita hii ya corona virus mbona hatuwasikii wataalamu wa madawa wa Afrika wakijihangaisha na kutafuta tiba au kinga ya virusi hawa?

Macho na Masikio tumeviacha visikilizie tambo za chanjo na dawa kutoka huko mataifa makubwa. Afrika kama bara kuna mchanganyiko wa watu mbalimbali wenye tamaduni mbalimbali ambao tumerithi vitu mbalimbali.

Kwa karne zote kabla ya ukoloni kuja Afrika Babu zetu walikuwa wanaumwa na kujitibu wenyewe na ushahidi upo waliishi miaka mingi kuliko hata miaka tunayoishi sisi.

Imekuwa ni kawaida dawa zetu kuzipa majina ya "local medicine" (dawa za kienyeji) Tafsri ambayo kwa maoni yangu naona si sahihi. Tafsri ya kutudogosha

Sasa hivi tunao wasomi wengi sana katika bara hili. Wanajua njia zote za kufanya tafiti na kufanya kitu kitambulike na kukirasimisha.

Kama Afrika, tunamchango gani katika kutafuta tiba na kinga za magonjwa mbalimbali yanayotukumba? Kwa miaka yote hiyo watafiti katika magonjwa wameshindwa kutoa ushawishi kwa serikali zao kufadhili tafiti zao ili angalau watu wetu watibiwe kwa tiba zetu wenyewe?

Leo Tanzania tunaendesha maombi ya Kitaifa kuliombea Taifa dhidi ya janga la corona. Kwanini juhudi kama hizi zisionyeshwe katika kuunga juhudi za wataalamu wetu? Hatukatai maombi ila hatuna budi kukubali ukweli kwamba maombi bila juhudi ni sawa na kelele tu! Huwezi kubweteka halafu ukajipa matumaini eti Mungu atakusaidia kupitia maombi yako tu! Hii miujiza haipo!

Wakristo wanajua kwamba Yesu mahali fulani alisema "ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa"...Sio mtaalamu wa theolojia, ila naamini hapa alilenga kuwahimiza watu kujishughulisha wanapokuwa na hitaji fulani. Kufanya maombi tu bila kufanya juhudi za kutumia vipawa alivyotujalia haya yatakuwa makelele tu

Dawa zetu zinaitwa za kienyeji kwasababu tumebweteka na wasomi wetu wamekubali kubaki kuamini vitu vya kimagharibi badala ya kupigania kufanyia tafiti dawa zetu ili ziwe rasmi. Tunajua figisu za wamagharibi katika masoko lakini mi naamini tukiweka juhudi ipo siku tutafanikiwa tu! KAMA BARA NASEMA HATUJAAMUA BADO! WASOMI WAMELALA!

Pa kuanzia ni hapa kwenye corona! Tusibeze sana dawa zetu za asili. Tuzijaribu, tufanye tafiti, tuunganishe tamaduni za kimatibabu za jamii hii na ile kwa magonjwa yanayofanana. Tuangalie wahaya walijitibu vipi homa? Wandengereko walitumia nini? Kule Uganda, Rwanda, Burudi na Kenya walijitibu vipi magonjwa ya mafua, kikohozi, kifua enzi hizo? Tupeleke maabara mizizi. majani, na kila aina ya dawa walizotumia na zinazosemekana kuleta matokeo. Tuboreshe tunapoona panafaa kuboresha kulingana na wakati. Lazima tutatoka na kitu ambacho hakitakuwa na jina bovu la kienyeji!. Hata hizo dawa zao ni matokeo ya vitu mbalimbali vilivyokusanywa kulingana na matumizi katika jamii zao. Tufanyie tafiti mimea tuliyonayo inayosemekana ni dawa. tuanze kujitibu wenyewe. Tusione sifa kuitwa wasomi wakati hatuna cha kujivunia kama waafrika

Bila ya hivi hawa wanaosemekana kuweka vitu wanavyovijua wao kwenye dawa zao kwa malengo yao wanayoyajua wataendelea kufanya hivyo na watafikia malengo yao tu.

Yangu ni hayo tu karibuni tujadili kwa pamoja
If you live like you're in the past,the future will never find you
 
Back
Top Bottom