Covid-19 lockdown: Mahakama Kuu Zanzibar Yasitisha Shughuli za Kimahakama Kwa Siku 30

Ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
5,697
4,729
Mahakama Kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesisitisha shughuli zake za kimahakama kwa siku 30.

IMG-20200326-WA0065.jpeg
IMG-20200326-WA0066.jpeg

=====

MAHAKAMA Kuu Zanzibar imesitisha usikilizwaji wa kesi zote kwa muda wa siku 30 kuanzia March 26 hadi Aprili 24 kutokana na kuchukua tahadhari za kujikinga maambukizi ya virusi vya corona (covid-19).

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Vuga Mjini Unguja, Mrajisi wa Mahakama kuu Zanzibar, Mohamed Ali Mohamed amesema kwamba wamefikia uwamuzi huo kutokana na maagizo yaliyotolewa na Serikali mnamo tarehe 17 March mwaka huu juu ya kujikinga na kuenea kwa virusi vya Corona (COVID- 19).

Alisema usititishwaji wa kusikiliza kesi kwa muda wote wa siku 30 ni kwa mahakama zote kutokana na kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.

“Kuanzia leo March 26 kutasitishwa usikilizwaji wa kesi kwa muda wa siku 30, kwa zile kesi ambzo zipo hatua ya kusikiliza ‘Submisition’,Mahakama itawashauri Mawakili au wenye kesi kuwasilisha kwa njia ya maandishi” alisema Mrajisi huyo.

Pia alisema kwa kipindi hicho Mahakama zitashughulikia kesi za dharura na kwa washtakiwa wenye kesi nzito na maombi ya dhamana hivyo muombaji na wakili wake au wadhamini ndio watakaruhusiwa kuingia Mahakamani.

“Kwa Makosa yenye dhamana, Majaji na Mahakimu wanatakiwa kutoa dhamana yenye masharti nafuu ili kupunguza mrundikano wa katika Chuo cha Mafunzo (Magereza) kwa kipindi hichi cha mripuko wa mripoko wa virusi vya Corona” alisema Mrajisi huyo.

Aidha alisema katika kipindi hichi watendaji wote wa Mahakama wataendelea kuwepo kazini hivyo kumbi za Mahakama (Open Court) hazitatumika.

“Kwa Majaji na mahakimu wenye hukumu na maamuzi (Ruling) watatumi kipindi hichi katika kuzikamilisha” alieleza Mrajii huyo.

Hadi sasa Zanzibar imeripoti visa vya wagonjwa wawii ambao wamebukizwa virusi ambapo wanaendelea vizuri na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua hatua kadhaa za kujikinga na miripuko wa virusi hivy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We should stop shughuli zote ambazo sio za uzalishaji mali, mahabusu wote waachiwe!. Corona ikipita wakamatwe tena.

Wafungwa karibu wote waachiwe msamaha Maalum wa Corona.
P
 
Hako ni branchi ka Tanzania ,hakana madhara ya Mona kwa moja
Mahakama Kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesisitisha shughuli zake za kimahakama kwa siku 30.

View attachment 1399819View attachment 1399820

=====

MAHAKAMA Kuu Zanzibar imesitisha usikilizwaji wa kesi zote kwa muda wa siku 30 kuanzia March 26 hadi Aprili 24 kutokana na kuchukua tahadhari za kujikinga maambukizi ya virusi vya corona (covid-19).

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Vuga Mjini Unguja, Mrajisi wa Mahakama kuu Zanzibar, Mohamed Ali Mohamed amesema kwamba wamefikia uwamuzi huo kutokana na maagizo yaliyotolewa na Serikali mnamo tarehe 17 March mwaka huu juu ya kujikinga na kuenea kwa virusi vya Corona (COVID- 19).

Alisema usititishwaji wa kusikiliza kesi kwa muda wote wa siku 30 ni kwa mahakama zote kutokana na kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.

“Kuanzia leo March 26 kutasitishwa usikilizwaji wa kesi kwa muda wa siku 30, kwa zile kesi ambzo zipo hatua ya kusikiliza ‘Submisition’,Mahakama itawashauri Mawakili au wenye kesi kuwasilisha kwa njia ya maandishi” alisema Mrajisi huyo.

Pia alisema kwa kipindi hicho Mahakama zitashughulikia kesi za dharura na kwa washtakiwa wenye kesi nzito na maombi ya dhamana hivyo muombaji na wakili wake au wadhamini ndio watakaruhusiwa kuingia Mahakamani.

“Kwa Makosa yenye dhamana, Majaji na Mahakimu wanatakiwa kutoa dhamana yenye masharti nafuu ili kupunguza mrundikano wa katika Chuo cha Mafunzo (Magereza) kwa kipindi hichi cha mripuko wa mripoko wa virusi vya Corona” alisema Mrajisi huyo.

Aidha alisema katika kipindi hichi watendaji wote wa Mahakama wataendelea kuwepo kazini hivyo kumbi za Mahakama (Open Court) hazitatumika.

“Kwa Majaji na mahakimu wenye hukumu na maamuzi (Ruling) watatumi kipindi hichi katika kuzikamilisha” alieleza Mrajii huyo.

Hadi sasa Zanzibar imeripoti visa vya wagonjwa wawii ambao wamebukizwa virusi ambapo wanaendelea vizuri na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua hatua kadhaa za kujikinga na miripuko wa virusi hivy

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachofanyika Zanzibar (ama kuamuliwa na SMZ) lazima tu kitakuwa na effect kwa nchi

Serikali ya Muungano iidhibiti SMZ, kwa kuwataka wawashirikishe katika intension zao ili zipimwe na ikiwezekana zitekelezwe kwa pamoja (visiwani na bara) - endapo ni nzuri
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom