COVID-19: Jinsi ya kutumia Simu yenye Password ili kumsaidia Mgonjwa ambaye simu yake ina Password

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,488
86,003
Wakuu, Poleni kwa kuwapoteza Wapendwa wenu kwa namna moja ama. Kuna nyakati inabidi kuna mambo tukumbushane au tufundishane, si dhambi. Kwa kipindi hiki cha Corona kuna wenzetu wanaweza kuzidiwa ghafla na tukahindwa kumsaidia kwakuwa hatuawafahamu ndugu zao na kwakua simu zao zina Passwords. Nawexza kusema sio kwa Corona tu bali hata kwenye ajali au dharura nyingine yoyote. Twende pamoja na nakusihi, ukijifunza kitu hapa basi mshirikishe na mwenzio.
1588182704068.png

Picha hii ya kwanza ni jinsi Screen yangu ya simu ambayo ni smartphone inavyonekana, Naamini kuwa simu nyingi zitakua zina display namna hio kama simu hio itakua na password. Kama huna Passoword ya Mhusika hutaweza kuendelea zaidi ya hapo, sasa nini kifanyike? Fanya hivi, Click hilo neno EMERGENCY, ukili click litakueletea picha hii ifuatayo
1588182925348.png

2. Kwenye Screenshot hii baada ya kugonga neno EMERGENCY itakuja kitu kama hicho hapo, sasa hapo ukipafungua patakuletea Screen nyingine ambayo itakua na taariza za mhusika wakati wa dharura, labda hapa niseme kwamba ukinunua simu yake au hata sasa kama hujafanya hivyo, unatakiwa na ni muhimu ukaingiza hapo taarifa zako rasmoi ambazo zinaweza kutumika wakati wa dharura kama screen inayofuata inavyoonyesha.

1588183523822.png

Screen hiii zitakua na sehemu mbili, za zote nitaziweka kwenye screenshot yake kila moja, ya kwanza, inaonyesha INFO taarifa zako za kiafaya, kama una aleji, group la damu, wapi unapatikana, n.k, ni vyema kujaza taarifa zako sahihi. Hizo ni taarifa zangu sahihi kwa sasa. Screen ya mwisho nayo ina taarifa ambazo ni muhimu sana.
1588183756139.png

Screen hii ya mwisho kwenye mlolongo huu inaonyesha tuuite CONTACTS hapa ndio utapata namba za simju za dharura ambazo unaweza kuzitumia kuwapata ndugu wa Mhusika. Muhimu hapa ni kuweka taarifa au namba za simu ambazo huyo mtu au ndugu yako sio wale ambao hawapokei NEW NUMBER, unatakiwa kuweka namba ambazo zina watu wenye kuweza kufanya maamuzi juu yako, sio wale ambao wataanza kulia badala ya kutoa msaada wa faster.

Nakaribisha maboresho zaidi kwa simu nyingine au simu nyingine pia, kwa mfano kwa Watumiaji wa Samsung series kuna button ukiwa na dharura ukiibonyeza inatuma taarifa za location ulipo kwa namba ambazo umesevu pamoja na kuendelea kupiga picha na kutuma kwenye hizo namba hio ikiwataka kuja kutoa msaada wa haraka.
 
YEHODAYA hii hapa nimeshaiposti njoo usome na uwashirikishe na wengine. Usije na siasa
 
Safi sana! Kuna mtu aliweka uzi akidai tusifunge simu zetu kwa nywila ili wakati wa dharula iwe rahisi kuwapata ndugu wa karibu,nadhani kwa bandiko hili litasaidia wengi.
 
Back
Top Bottom