Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,399
- 31,352
Hapana ! hoja zangu zipo waziNguruvi3, umepatwa na nini? Mbona umekaa kimipashomipasho aisee? Mpaka narudia mara mbilimbili kusoma Username yako kuhakiki.
Hoja zako zaweza kujitegemea pasipo mipasho na bezo za ajabu ajabu, kwa sasa zinaonekana kuwa ni msukumo wa chuki ba kinyongo binafsi.
Jitafakari Upya Mkuu.
1. Kuzuia upotoshaji kuhusu Corona na Chanjo
Kwanza, Corona ni ugonjwa na ni pandemic. Ni tatizo la dunia na si vita ya aina yoyote ile
Pili, tunahitaji mbinu za sayansi kukabiliana na maradhi. Sala, Maombi na mapambio ni mali binafsi
Tatu, conspiracy theory zinazoenezwa kuwadanganya wananchi tutazipinga kwa nguvu zote
Nne, kuwaeleza wasomaji nini hasa kinaendelea katika ulimwengu katika zama hizi za ugonjwa hatari
2. Kudai haki ya chanjo
Kwamba, kama raia wa dunia tuna haki ya kupewa fursa ya chanjo. Si lazima kwa mtu, kukataa chanjo ni haki ya mtu. Haki hiyo ndiyo inayotoa haki ya watu kudai chanjo. Ni haki na si hisani ya mtu kwa utashi wake tu
Afya ni suala la mtu binafsi na haliamuliwi na mamlaka au idara yoyote au mtu mmoja tu kwa hisia zake
Mbona hatuoni serikali ikisimami watu wakubali au wakatae operesheni ?
Nafahamu kibwagizo cha mbuzi kala mkeka knaudhi hasa kwa washabiki walioaminishwa ujinga nao pasi kufikiri wakauchukua kama ukweli. Ni kero kwa waliopewa kazi ya kupotosha umma !
Ndiyo maana nasema tumechekwa sana duniani ! tunaita ugonjwa wa dunia changamoto ya kupumua kwa kuhofia mtu na si afya zetu. Tunakataa sayansi kumpendeza mtu na si kuponya nafsi zetu.
Msomi katika kiwango cha juu anaposema lishe ni dawa ya corona, hapo tukimsema itakuwa mipasho?
Msomi anapotengeneza dawa leo India wanaumia na hawezi kuipeleka ni mipasho kweli?
Hivi hukuona balozi wa Japan akikabidhi choo cha sekondari kwa mkuu wa Wilaya. Katika hali hii tunawezaje kuhoji chanjo ya virus tusiowaona ikiwa hatuwezi kufukua ardhi na kuweka mashino. Ni mipasho hiyo kweli!
Tumekubali kulishwa majani eti ni dawa kwasababu tu kuna mtu kaamua.
Tukaambiwa kuna dawa zetu ambazo huwezi kupeleka katika nchi yoyote jirani miongoni mwa mataifa 8 yanayotuzunguka. Tukaaminishwa mchachai unaponya.
Tukaambiwa garlic, pepper zinaponya, leo wahindi wanaokula vitu hivyo hali ni tete
Lakini mkuu, siku zote silaumu huwa natoa maangalizo.
Kabla ya ATC kusitisha safari sisi tulisema wiki nyingi kabla
Tukaeleza hatari ya kutotoa elimu kwa umma, wao wakaja siku nyingi baadaye
Ni hayo mkuu, uwe na amani nipo kama nilivyokuwa