#COVID19 COVID-19 is historical in Tanzania: Why don't USA, UK, EU and others copy from Tanzania how to fight against the Corona Virus?

Mlenge hiyo taarifa ya Afya ni ya COVID au maradhi yote?

Ukiisoma ni mchanayato tu lakini ukweli unabaki pale pale inahusu COVID.
Tunashukuru na kuwapongeza wametusoma na kufanyia kazi baadhi ya maeneo tuliyozungumzia.

Pamoja na hayo kinachoendelea bado ni kile kile isipokuwa kwa mwendo tofauti kidogo.

1. Ukurasa 1 , unasema serikali inaweza kuudhibiti ugonjwa.
Well, mwaka jana tulisikia tambo hizo, ulipoibuka tena tunajua kilichotokea huko mtaani na kwingineko.

India, wiki iliyopita walishangalia kudhibiti Covid wakaachiwa wajimwage mto Ganjes kwa raha zao

Leo new cases ni 400K (Maambukizi mapya ni laki 4), wanakochomea hakufai, ruksa k katika back yard (uani)

Ukurasa 2.
Kueleza watu ukweli si kuwatia hofu ni kuwaandaa na tahadhari.

India hawakuwaambia watu tatizo wakawaacha waogelee mtoni . Leo wanazika wenyewe kila mtu na ndugu ye.

Ukweli si hofu bali ni ukweli.

Ulaya wanachanja watu na kuchukua kila tahadhari kumaliza COVID. Israel wamefungua nchi na kwingine wanafanya hivyo. Hawaridhiki na ujinga wa kuishi na maradhi, wanapiga vita maradhi.

Vaa barakoa panapolazimika.
Hii ni kauli ya mtaani kweli kweli. Hivi nani anajua wanalazimika wapi ?
Huwezi kutoa kauli ukaiacha open namna hiyo , kutakuwa na tafsiri tofauti na mwisho huta achieve chochote.

Fanya mazoezi
Hili nalo ni la Tanzania tu. Huko kwingine kuna mazoezi kweli kweli na watu wamekufa

Lishe:
Hili ni la kubumba bumba kujaza ukurusa. Kuna nchi ukitaka ' protein, vitamin or minerals' unaipata kama ilivyo.

Huhitaji kubugia maembe kama yule Mama ! Bado watu wamekufa sana, nani kasema ni dawa ya Covid?

Hili laTiba za asili sitaliongelea.
Wapo waliojaribu ! mabanda yakajengwa wengine wakatumia wengine wakapelekwa Hospitali
Hili ni la akili ya kila mtu. Kama majani yanatibu hureee! na iwe hivyo.

Unaweza kuona hali ilivyo!
Ndiyo maana tunasema chanjo ije atakaye apate asiyetaka aendelee kula matunda, kujifukiza, maombi sala n.k.

Hiyo taarifa ukiisoma ilipaswa kuwa kurasa 1, imejazwa mavitu na uganga wa kienyeji, at this day and age!!!

Kokoro limesomba kila kitu ziwani ! Wapambe mtaelewa lini?
 
SOMO KUTOKA INDIA

Taarifa ya Wizara ya Afya Tanzania katika mabandiko hapo nyuma imesisitiza 'serikali inaweza kudhiti COVID-9' .

India nchi iliyoathirika sana na wimbi linaloendelea la Corona inakabiliwa na tatizo mawili makubwa
Tatizo la muda mfupi na la dharura ni upatikanaji wa 'Oxygen'
Tatizo la pili ni vaccination kwa mamilioni ya watu ili kudhibiti ugonjwa kama ilivyofanyika nchi za Magharibi

Mfumo wa Healthcare wa India upo juu ukilinganisha na wa kwetu ndiyo maana tunapeleka Wagonjwa wetu.

Mfumo wa usambazaji wa hewa ya Oxygen katika nchi zilizoendelea ni '' Central' kwa maana,kuna mtungi mmoja mkubwa kama ile ya vituo vya mafuta, halafu wodi za wagonjwa zimeunganishwa ''system' na mfumo huo.
Hivyo mgonjwa anapata Oxygen akiwa katika kitanda na ipo switch ndogo ya kuunganisha hewa

Kuna wakati California ilikabiliwa na tatizo la Oxygen kwasababu ya ongezeko la Wagonjwa.
Hata hivyo tatizo hilo lilitatuliwa mara moja kutokana na mifumo imara ya usambazaji

Kwa Tanzania, mfumo wetu ni ule wa kutumia mitungi ya Oxygen.
kwamba mgonjwa mmoja na mtungi mmoja. Kwa Wagonjwa 200 basi utahitaji mitungi 200 ( 200 O2 cylinders)

Ndicho kinatokea India kwasasa na nchi zilizoendelea zinapeleka misaada ya mitungi kwa ndege na Oxygen katika matanki kwa njia nyingine ikiwemo reli na meli

Kuna Hospitali moja ya ''Badra' nchini india iliyokuwa na Wagonjwa 230 katika ICU. Oxygen ilikwisha na ilichukua dakika 80 kupata tena kwa maana ya supply kufika. Katika kipindi hicho watu 12 walipoteza maisha.
Fikiria hivi kwa Saa 1 na Dakika 20 watu 12, je ingekuwa saa 6 au 8 au 10 nini kingetokea!!

Mwaka jana wakati wimbi linavuma Tanzania kulikuwa na ''taarifa'' za ndugu kuhaha kutafuta mitungi ya Oxygen.

Ilifika mahali '' ikasema rushwa' ilitumika . Katika mazingira ya ugonjwa rushwa ni jambo la hatari hasa ikiwa 'against' asiye na uwezo. Hayo yalisemwa na tuyaache kama yalivyo, lakini, tulishuhudia mengi

Ni kwa mantiki hii tunajiuliza ikiwa serikali imejiandaa kwa njia zote.

Kuna tofauti ya kudhibiti ugonjwa inayosema na Serikali na kukabiliana na ugonjwa ''emergency' unapotokea.

Kudhibiti ugonjwa ni long term plan, kukabiliana na ugonjwa ni 'emergency'

Badala ya kuendeleza zogo la kijinga la lishe, mitishamba na madogori ya asili na kienyeji, wizara ya Afya itafakari ikiwa Hospitali zina uwezo wa kutoa Oxygen na ikiwa nchi inaweza kuzalisha Oxygen katika high demand

Tunayasema haya si kwa kutisha watu, wala haina maana wimbi la India laja! la hasha

Kuna kitu kinaiitwa 'preparedness' kwamba unajiandaa kwa dharura hata kama haipo katika njia yako

Wapambe waliosimama kiambazani watasema 'tusitishe watu'', wanasahau mbuzi hakuwatisha ! kala mkeka
 
Kuna kitu kinaiitwa 'preparedness' kwamba unajiandaa kwa dharura hata kama haipo katika njia yako
Katika wizara iliyojiandaa vizuri TZ, walau kimfumo, kwenye "preparedness" ya dharura, ni ile yenye dhamana ya afya. Tayari wizara ina miongozo mbalimbali ya namna bora ya kujiandaa na majanga. There is always room for improvement in anything, so they may as well look for ways to improve, e.g., conducting a specific Vulnerability, Risk Assessment and Mapping (VRAM) for COVID... and update the previous VRAMs and HSI (Hospital Safety Index) reports.

Tukokotoe kidogo.

Mwaka 2019 India ilikuwa na watu bilioni 1.366 (watu 1,366,000,000) kwa mujibu wa mtandao.

Kasi ya vifo mwaka 2019 ni 7.265 kwa watu elfu (World Bank).

Yaani, mwaka 2019 watu 7.265 x 1,366,000 = 9,923,990 watu waliofariki kwa mwaka mzima. Au 827,000 kwa mwezi, au 27,500 kwa siku.

Kwa hiyo kila siku, kwa wastani, nchini India, hufa watu takriban 27,500.

Toka corona imeingia India, imeua watu 218,945 (worldometers.info). Tuchukulie walipunguza mahesabu. Walikuwa 500,000 kwa mwaka mzima.

Hao laki tano ni 500,000/9,923,990 = 5% ya vifo vyote. Pana vitu vingine vinavyosababisha 95% ya vifo huko India. Generous estimation. Real rate could be much lower.

Every human loss is tragic. Tell me the scientific reason to deal with a cause of 5% of deaths in India, and ignore causes that kill the remaining 95%? Kwa mfano si chini ya 15% ya vifo nchini India inasababishwa na magonjwa yahusianayo na moyo. These diseases kill many more than coronavirus - Times of India

Kila kifo tungetamani kisiwepo. Na tuchukue hatua zote zinazowezekana kukizuia. Lakini kwenye afya ya jamii -- yanaangaliwa mambo mtambuka -- katika kufanya maamuzi ya kuweka vipaumbele.

IndiaDeathRates.jpg
Source: Times of India
 
Mlenge unachotaka kusema hapa ni kuwa vifo na hali inayotokea India ni ya kawaida kwa uwiano wa population!

Umenikumbusha hoja moja ya kipuuzi niliyowahi kuisikia ikisema ' hata wakifa hawatakufa wote'' hapa Tanzania

Ni hivi kuna vifo vya kawaida vinavyoitwa natural death. Hivi hata kama vinatokea kwa kiwango kikubwa vinaeleweka. Halafu kuna vifo vinatokea katika idadi inayoleta maswali kulikoni?

Kwa watu wa Epidemiology na Biostastic huangalia pattern. Ikiwa vifo vinatokea kwa homa tu isiyojulikani basi husemwa ni outbreak ya homa. Ikifika hapo watu wa Pathology watatafuta sababu ya chanzo cha homa.
Chanzo cha homa kikishakuwa established, na kama ni eneo fulani hiyo itatiwa epidemic. Ikisambaa duniani ni Pandemic.

Vifo vya India vina established cause ambayo ni COVID-19 , b.1.617. Vifo vinatokea kwa wingi ikiwa ni outbreak ndani ya outbreak ya Covid. Ndiyo maana wingi wa vifo umelazimu haya

1. Nchi 40 duniani zikiwemo za viwanda zimeingilia kati kusaidia India kwasababu vifo ni vingi sana isivyo kawaida

2. India, yenye watu Bilioni na ushee unayosema , imelazimu kuruhusu watu kufanya back yrad kama crematorium

3. Leo wizara ya misitu imeruhusu kukata miti ili kuchomea watu, kwamba, kuni za kuchomea maiti ni bidhaa adimu India achilia mbali Oxygen.

4. Nchi za dunia zimezuia watu kutoka India kuingia nchi mwao kuchelea variant isiyoeleweka makali yake

Katika hayo 4, ni bwana msafiri na wapambe wake tu wanaoweza kudhani vifo ni kawaida kwa idadi ya watu.

Kuhusu wizara ya afya. Miongozo iliyopo ilikuwepo na haikuwahi kufanyiwa kazi, leo kuna kipi kigeni?
Miongozo ni ile ile ya kutumia mavumba, manyanga, madogori, chemsha chemsa , lishe na maembe
Ni watu wale wale waliosababisha janga la kokoro na kuzoa kila kitu bado wameshika uzi sasa tutegemee maajabu gani. Wale wale waliohubiri mafenesi na kukimbia hovyo ni dawa ya COVID ndio wanaoongoza halafu tutegeme kuna OXygen cylinders za kutosha. Maembe yatapigiwa debe lini!!

Wapambe pambane ni hali yenu, mu wakiwa ! alaumiwe mbuzi
 
But but but steam inhalation works very well in India. Besides, India has got fantastic herbs such as turmeric, garlic, cinnamon etc etc etc.

How is that working?
 
Kinachosemwa ni kwamba huwa wanaangalia "excess deaths". Hilo halikusikika likisemwa.

Halafu wanaosema, ni wenyewe Wahindi... These diseases kill many more than coronavirus - Times of India
Hiyo kauli kuna yule! naye alikuwa anaisema lakini haina mantiki.
Ni kutokuwa na sympathyau concerns na maisha ya mwanadamu.

Watu wa aina hii wana moral decay, na ni wakatili sana. Hawajui thamani ya maisha ya mwanadamu

Tunaangalia vifo kwa wingi wake na muda. Inapofikia crematorium haziwezi ku handle kuna tatizo
Inapofikia kuni hazitoshi ina maana ile natural pattern imepita kiwango
Inapofikia watu wanachomea maiti katika backyard kuna tatizo
Inapofikia serikali inalegeza masharti ku accommodate situations kuna tatizo
Inapofikia mataifa 40 yanaingilia kati si hali ya kawaida

Ni hivi kuna tatizo India, hao wahindi wanasema na wanamlaumu sana Narendra Mohdi kwa kudharau ushauri wa wataalam kama alivyofanya Bosnaro wa Brazili , Trump na washamba wengine huko duniani

Mtahangaika sana, miili yenu imejaa chanjo! ukweli mnajujua mnachotaka ni kuubabisha umma.

Mbuzi alaumiwe, kala mkeka wapambe wamesimama viambazani
 
''When asked by SciDev.Net whether his remarks could lead to COVID-19 vaccine hesitancy among the public, Mgaya said: “The urgency to push the vaccines to the mass consumption phase does not make them non-experimental.”

Ipo siri kubwa kwenye hili sakata la Covid-19.
 
Mgaya ni huyu Profesa wa NIMR?

Kuna ujinga unaenezwa duniani. Hawa wote wanaodhani vaccine ina matatizo milini mwao wamebeba Polio, DPT n.k. Sasa sijui wanakataa nini. Leo wengine wamepeleka watoto kupata chanjo.

Wajanja duniani wametoa vaccines kwa watu wao, Africa na conspiracy theory na ambao hata vyoo vya shule wanasubiri balozi wa Japan ajenge eti wanahoji vaccine

Tuliona wasomi wakubwa tu wakibugia maji ya mchachai kule Madagascar !

Halafu kuna wakaidi , well, virus haina ukaidi na haijui nyadhifa, wasifu au hadhi.

Wapambe ! tunahitaji vaccines ninyi msiohitaji hamlazimishwi. Kwanini mnahangaika kushawishi umma

Tunataka chanjo kama hamtaki msipige ila msitumie mitandao kupotosha umma

Mbuzi kala mkeka na kuwatia ukiwa, mtahangaika sana!
 
Mbuzi kala mkeka na kuwatia ukiwa, mahangaika sana!
You are correct, but no one knows the effects /madhara ya hizo chanjo baada ya mwaka moja au miwili. Research iliyofanywa Canada imeonyesha animals kufa ghafla nk. Lakini hiyo siyo sababu ya kupinga hizi chanjo. Chanjo inatakiwa kuwa safe period.

Chanjo za zamani zilifanyiwa upembuzi na madhara hayakutokea, vile vile waliotengeneza hizo chanjo hawakuogopa kushitakiwa, hatuwezi tukaamini hizi chanjo mpya ambazo zinafanywa kimashindano na kuondoa kinga ya kushitakiwa kama zitakuwa na hitilafu. Kwa nini hawataki kushitakiwa? Kwa nini wanaopewa chanjo wachukue risk na sio watengenezaji wa chanjo?

BTW Tanzania tangu mwaka jana huu ugonjwa mbona haupambi moto kama tunavyoaminishwa?
 
Hiyo kauli kuna yule! naye alikuwa anaisema lakini haina mantiki.
Ni kutokuwa na sympathyau concerns na maisha ya mwanadamu.

Watu wa aina hii wana moral decay, na ni wakatili sana. Hawajui thamani ya maisha ya mwanadamu

Tunaangalia vifo kwa wingi wake na muda. Inapofikia crematorium haziwezi ku handle kuna tatizo
Inapofikia kuni hazitoshi ina maana ile natural pattern imepita kiwango
Inapofikia watu wanachomea maiti katika backyard kuna tatizo
Inapofikia serikali inalegeza masharti ku accommodate situations kuna tatizo
Inapofikia mataifa 40 yanaingilia kati si hali ya kawaida

Ni hivi kuna tatizo India, hao wahindi wanasema na wanamlaumu sana Narendra Mohdi kwa kudharau ushauri wa wataalam kama alivyofanya Bosnaro wa Brazili , Trump na washamba wengine huko duniani

Mtahangaika sana, miili yenu imejaa chanjo! ukweli mnajujua mnachotaka ni kuubabisha umma.

Mbuzi alaumiwe, kala mkeka wapambe wamesimama viambazani

Mkuu Nguruvi3 unatukosea sana wasomaji wako. Unao uwezo mkubwa wa kujenga hoja. Umetupatia shule ya mambo ya epi posti mbili tatu hapo juu.

Imekuwa countered na concept nyingine ya "Excess Deaths". Unaweza na tena ni vema kabisa usipokubaliana nayo kwa mtazamo wako. Lakini si vema kufanya personal attacks, kwa vile inatutoa kwenye kujadili ishu.

Linki hiyo ya Google Search, angalia taasisi na watu wengine wakiijadili concept hiyo na kuitumia kuelezea afya ya jamii, ikiwemo COVID-19.

Kuhusu chanjo ya corona, my personal estimation ni kwamba mwisho wa hadithi, itakuja tu kuruhusiwa.

Na tena nakisia kuhamishwa magoli. Inaweza isiwe kwa anayetaka tu. Iwe kwa lazima.

India wamechanja. Na tena wanatengeneza chanjo. If I get you right, unamaanisha wanaokufa sasa hivi huko India ni wale tu ambao bado kufikiwa na chanjo. Right?

Right?
 
You are correct, but no one knows the effects /madhara ya hizo chanjo baada ya mwaka moja au miwili. Research iliyofanywa Canada imeonyesha animals kufa ghafla nk. Lakini hiyo siyo sababu ya kupinga hizi chanjo. Chanjo inatakiwa kuwa safe period.

Chanjo za zamani zilifanyiwa upembuzi na madhara hayakutokea, vile vile waliotengeneza hizo chanjo hawakuogopa kushitakiwa, hatuwezi tukaamini hizi chanjo mpya ambazo zinafanywa kimashindano na kuondoa kinga ya kushitakiwa kama zitakuwa na hitilafu. Kwa nini hawataki kushitakiwa? Kwa nini wanaopewa chanjo wachukue risk na sio watengenezaji wa chanjo?

BTW Tanzania tangu mwaka jana huu ugonjwa mbona haupambi moto kama tunavyoaminishwa?
Wacha1 ,

In the end, nionavyo, chanjo zitaletwa Tanzania na zitaruhusiwa. It is a matter of when.
 
But but but steam inhalation works very well in India. Besides, India has got fantastic herbs such as turmeric, garlic, cinnamon etc etc etc.

How is that working?
It works the same way vaccine works, perhaps.

Are the people dying now in India ALL of them die because they are not fully vaccinated? Well, inawezekana hawajapiga nyungu pia.

Data zikiwepo za kulinganisha relative risks kwa makundi ya waliochanja vs wasiochanja; waliopiga nyungu vs wasiopiga, ndipo itakapojulikana vema.

Pana video imesambaa sana TZ kuhusu India na mlipuko huu wa sasa. Siwezi kuishea hapa ili kuheshimu TOS. Video ina madai kwamba baadhi ya hospitali zinachenji kota vifo vingine na kuviita vya korona, for nefarious reasons. Data hizo hapo juu zitafaa katika kudebunk video kama ile.
 
You are correct, but no one knows the effects /madhara ya hizo chanjo baada ya mwaka moja au miwili. Research iliyofanywa Canada imeonyesha animals kufa ghafla nk. Lakini hiyo siyo sababu ya kupinga hizi chanjo. Chanjo inatakiwa kuwa safe period.
Sijui hiyo ni stage gani ya Clinical Trial. Sijui.

Ninachokijua ni kuwa kuna vifo vya ghafla kutokana na Variants zilizoingia.
Haijulikani kama ni za Kent, Brazil au South Africa. Hili nalo linafanyiwa uchunguzi

Kwa taarifa tu stage za clinical trial zinahusisha wanyama katika hatua za awali si za mifugo.
Hizi conspiracy theory na kuokota vitu kuna matatizo yake.
Chanjo za zamani zilifanyiwa upembuzi na madhara hayakutokea, vile vile waliotengeneza hizo chanjo hawakuogopa kushitakiwa, hatuwezi tukaamini hizi chanjo mpya ambazo zinafanywa kimashindano na kuondoa kinga ya kushitakiwa kama zitakuwa na hitilafu. Kwa nini hawataki kushitakiwa? Kwa nini wanaopewa chanjo wachukue risk na sio watengenezaji wa chanjo?
Si kweli. Katika uzi huu tumeeleza Dr E. Jenner alivyoanza ugunduzi wa chanjo kwa kutumia wadudu wenyewe na kumpa mtu mzima. Ilibainika kuwa katika immune compromized situation watu wanakufa hasa wenye debilitating or pre existing conditions. Baada ya hapo ikafanyika live attenuated kwamba, wadudu wanapungumzwa makali ili wasilete tabu kwa watu wenye matatizo yanayohusiana na immunity.

Ikaonekana bado live attenuated wanaweza kuwa na nguvu kwa mgonjwa sana hasa wanaohusiana na immunity.
Ndipo ikaja extractions ya toxins na hii ya mMRA

Ugunduzi wa chanjo ya COVID-19 Ulianza siku nyingi kwa idea ya mRA lakini ulipata nguvu wakati wa SARS na ilipotokea Corona ilikuwa ni ku switch tu gene coding na kufanya gene sequencing ili kujua coding. Nivumilie kidogo!

Sasa chanjo za zamani zilikuwa na madhara hasa ukiangalia kitu kinachoitwa Post Market Surveillance.
Post Market surveillance inachukua hata miaka 20 na ndiyo maana inaweza kujulikana dawa ina madhara baada ya miaka mingi. Hii ni kutokana na collections ya data na kuzifanyia analysis kutoka katika market.

Sehemu kubwa ya chanjo ni vehicles kwa maana kiini cha vaccine kinabebwa na vitu vingi .
Huko nyuma walitumia hata vimiminika vya ''madini'ambayo baadaye yaligundulika kuwa na madhara.
Hii ndiyo chanzo cha anti-vaxxers

Chanjo ya sasa haitolewi kwa watoto na wajazito wanachukua risk kwa kusaini consent form.

Sababu kubwa ni kwamba hakuna anayejua ina impact gani kwa embryo, fetus, neonatal , babies au children.
Ni mpaka clinical trial itakapofanyika na tunaweza tusijue matokeo hadi miaka 20 baada ya post market surveillance

Kuna Bibi wa miaka 100 amepona Corona. Wataalam walipofuatilia wakagundua alizaliwa mwaka 1920 miaka 2 baada ya spanish flu pandemic. Hapa wataalam wanafanyika kazi uhusiano wa spanish flu na COVID-19 yaani miaka 100 baadaye. Hivyo si sahihi kutoa verdict kwa njia ya short cut kwamba Vaccine zilizopo zimeharakishwa

Kuharakishwa ni kwasababu ya emergency iliyopo lakini kazi ilianza 10 years ago. Hakuna mashindano ila kuna kugawana utaalam. Mfano, kuna makampuni hasimu yanafaya kazi pamoja kwa kutafuta common solution
BTW Tanzania tangu mwaka jana huu ugonjwa mbona haupambi moto kama tunavyoaminishwa?
A! hili hata sina jibu. Naomba tuliache tu maana tukilinyumbua tutaishia kwingine! please

Hoja kubwa ni kuwa vaccines iletwe na watu wapewe option ya kutumia au kutotumia.

Kwanini mgonjwa akiingia theatre ana sign consent form kwamba anakubali matokeo yoyote ya kupona au kifo? Vipi leo tunaona huruma kwa watu wanaotaka chanjo kwa ridhaa yao. Hapana hii ni kuwanyima haki

Kuna watu wapo tayari kuifuata popote duniani, lakini hakuna fursa.

Vaccine iletwe wakati huo huo maombi, sala, swala, mapambio ,. mitishamba, majani ya madagascar, Kicheba, Kidogobasi, Manyovu, Majita na Naliendele yaendelee kwa atakaye.

Kokoro limezoa dagaa, tasi, chuchunge, Sangara, papa na nyanguni! Wapambe miwani mumeacha wapi?
 
Swala la huu ugonjwa bado ni gumu, hakuna hata mmoja mwenye majibu sahihi ni ubabaishaji tu. Muda ndio utaongea, kwa wale ambao wanataka kufuata chanjo nje rukhsa. Serikali ya Tanzania bado haijaridhia chanjo hadi hivi sasa.

Hapa hakuna kitu kigumu hata kimoja, kuna watu wagumu kuelewa na hasa kujifunza kwa kutumia internet na conspiracy theory. Chanjo kama ya flu ipo miaka mingi na inaelezeka, sitashangaa hata covid ikiwa hivyo

Kuna taarifa zisizo rasmi kwamba wale variants wa India B.1.617 wame mutate , na new strain ni lethal 15X
Strain hiyo ina evade vaccine kwa mujibu wa habari. Tunasisitiza habari hizo zibaki kuwa zilivyo, ikitihibitika kisayansi tutawajulisha. Sisi hapa si Washamba na hatutakumbatia ushamba,tunaiamini Sayansi

Kuwaambia Watanzania wafuate chanjo nje ya nchi ni kuwanyima haki yao kama Raia.
Chanjo haitolewi kwa mtu binafsi, inaweza kutolewa na mashirika binafsi katika mazingira fulani.
Chanjo ni jukumu la serikali na serikali za dunia zinafanya hivyo

Kukataa chanjo ya Corona hakuna maana ikiwa tunapokea zile EPI
Chanjo iletwe kama dawa nyingine, anayetaka apige asiyetaka asilazimishwe. Period

Chanjo hailipiwi na serikali , zaidi ya hayo nchi za Ulaya zilitoa mabilioni ? ?27 hadi leo hazijulikani zilitumikaje

Si jukumu la serikali kuhamasisha maombi , Swala, Sala na Mapambio. Hiyo ni jukumu la mtu binafsi kuchagua

Serikali inapohubiri dini badala ya kuleta chanjo ni kituko sana.
Lini imani ikawa muongozo wa umma?Huu ujinga umetugharimu na tusiuendekeze tena!

Chanjo iletwe, kila mmoja achague. Kama hakuna chanjo basi tusisikie majani au mitishamba, kila mtu ajifie tu

Tusiwanyime Raia haki zao, wapo wanaojali na wapo tayari kununua chanjo kwa gharama yoyote.

Wapambe, mumesimama viambazani, miwani mliacha wapi? Tunajua mbuzi kala mkeka, lakini miwani je!
 
Nunueni basi na jab ya flu? Kama nchi ni lazima kujiridhisha na sio kufuata upepo tu jinsi unavyovuma.
 
Nunueni basi na jab ya flu? Kama nchi ni lazima kujiridhisha na sio kufuata upepo tu jinsi unavyovuma.
Kila siku nauliza swali, kujiridhisha na nini? Unaletewa chanjo za EPI kila siku. Leo kipi kigeni?
Maprofesa wetu si hawa wanaokunywa mchaichai! Si hawa wa ugunduzi wa Covidol ha ha ha OMG
India wana shida, kwanini hampeleki Mpiji, Covidol na NIMRcafe?

Hivi watalaam wetu si hawa wanaojenga mabanda ya kufukiza.
Tena tukaambiwa Garlic na pepper inakinga dhidi ya Covid, well! India wanakula sana!!!

Mataifa yote duniani yanapiga chanjo isipokuwa Tanzania kwasababu ya ushamba tu !

Tunajengewa vyoo vya shule na ubalozi wa Japan halafu tunahoji chanjo

Chanjo iletwe asiyetaka shauri yake, wapo waliokaidi uwepo wa Corona, well!

Wapambe enzi za kulishwa ujinga na kukumbatia ushamba zimepita!
 
Nguruvi3, umepatwa na nini? Mbona umekaa kimipashomipasho aisee? Mpaka narudia mara mbilimbili kusoma Username yako kuhakiki.
Hoja zako zaweza kujitegemea pasipo mipasho na bezo za ajabu ajabu, kwa sasa zinaonekana kuwa ni msukumo wa chuki ba kinyongo binafsi.

Jitafakari Upya Mkuu.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom