#COVID19 COVID-19 is historical in Tanzania: Why don't USA, UK, EU and others copy from Tanzania how to fight against the Corona Virus?

Taifa letu limeumizwa sana kwa maamuzi yasiyozingatia sayansi.

Tuache masikhara: hivi ni kweli unaamini kwamba Watanzania tulipokuwa tukienda hospitalini wakati wa korona, madaktari walikuwa wakituprescribe nyungu, malimau, au tangawizi?
 
Tuache masikhara: hivi ni kweli unaamini kwamba Watanzania tulipokuwa tukienda hospitalini wakati wa korona, madaktari walikuwa wakituprescribe nyungu, malimau, au tangawizi?
Hivi hukubali kwamba hilo lilitokea?
Yale mabanda ya nyungu MNH na Mloganzila yalikuwa ya nani?

Zile Covidol, NIMRcafe zilitengenezwa kwa ajili ya kina nani?

Ile Togwa ya Madagascar iliagizwa kwa ajili ya akina nani?

Waziri wa Afya na Naibu wake si walionekana wakibugia Togwa na mitindi!

Waziri wa Afya si alionekana akipiga nyungu na Mumewe na picha zipo?

Rais wa JMT Marehemu John si alikuwa anasisitiza matumizi ya nyungu!

Waziri Jaffo hakuagiza nyungu, season two na kuoenkana dhahiri shahiri

Haya ulikuwa wapi hukuyaona ?

Kama unadhani ujanja ni ghali jaribu Ushamba
 
Kwasasa hakuna ubishi tena kwamba 'tuliingizwa chaka' na hisia za mtu wala si sayansi

Badala ya kulima mahindi ili kuwauzia majirani tumefukua ardhi kuzika wapendwa wetu

Swali moja, je, tunahitaji watu wale wale walioshangilia udwanzi watusaidie kupambana na gonjwa?
Wale wa nyungu season 2 na Wala mananasi tena wakiwa na jukumu la wizara husika ndio hao watakaotuvusha ?

Wale wa nyungu na mananasi na kukimbia hovyo barabarani watarudi vipi kwa umma kuueleza kuhusu vaccines?

Tunahitaji mabadiliko, tunahitaji fikra mpya. Wale walioshindwa wakae pembeni, zama za mapambio zimepita

Mbuzi kale mkeka wapambe mtakalia nini? tumeshaondoa turubai ! tufungue mtaa
 
Hivi hukubali kwamba hilo lilitokea?
Yale mabanda ya nyungu MNH na Mloganzila yalikuwa ya nani?

Zile Covidol, NIMRcafe zilitengenezwa kwa ajili ya kina nani?

Ile Togwa ya Madagascar iliagizwa kwa ajili ya akina nani?

Waziri wa Afya na Naibu wake si walionekana wakibugia Togwa na mitindi!

Waziri wa Afya si alionekana akipiga nyungu na Mumewe na picha zipo?

Rais wa JMT Marehemu John si alikuwa anasisitiza matumizi ya nyungu!

Waziri Jaffo hakuagiza nyungu, season two na kuoenkana dhahiri shahiri

Haya ulikuwa wapi hukuyaona ?

Kama unadhani ujanja ni ghali jaribu Ushamba
The above was in reply to :
Tuache masikhara: hivi ni kweli unaamini kwamba Watanzania tulipokuwa tukienda hospitalini wakati wa korona, madaktari walikuwa wakituprescribe nyungu, malimau, au tangawizi?

Now people who are actually in Tanzania can be the best judges in this whether the doctors in health facilities prescribed to them nyungu, malimau and tangawizi... then can make their own opinions as to the motives of Nguruvi3 in falsely claiming so.
 
For anyone looking for objective reality of Tanzania's approach to fight against Coronavirus/COVID-19, can read discombobulation correspondence published in The Lancent Journal HERE.
 
For anyone looking for objective reality of Tanzania's approach to fight against Coronavirus/COVID-19, can read discombobulation correspondence published in The Lancent Journal HERE.
There was no approach! it was a one man show (denial).

Kuna approach ya kuwaambia watu mask zinawekewa Virus! real? That's an approach!

Tuweni wakweli kwani wakati Rais anawaambia watu wakalime hatukusikia?
Rais akiwananga wavaa barakoa kanisani , hatukumsikia?

Watu wamepoteza maisha kwasababu tu wapo waliokataa sayansi na kuendekeza ushamba.

Wapambe mtahangaika ukweli haubadiliki, mbuzi kala mkeka mtakalia nini?
 
The above was in reply to :

Now people who are actually in Tanzania can be the best judges in this whether the doctors in health facilities prescribed to them nyungu, malimau and tangawizi... then can make their own opinions as to the motives of Nguruvi3 in falsely claiming so.
Mabanda ya kufukiza kwanini yaliwekwa MNH na Mloganzila?
Kwanini hayakuwekwa 'Fire station' ? Kwanini hayakuwekwa Magomeni na Mburahati?

Profesa wa NIMR alikuwa anahubiri nini? Covidol ilikuwa prescribed wapi? NIMR Cafe ilitumikaje?

Watu wamepoteza maisha bila sababu za maana isipokuwa kukataa sayansi.
 
COVID-19 YAINGIA HATUA NYINGINE

''Double mutant' ya India sasa ni tishio.

Katika majira ya baridi kali kuelekea joto (spring) hasa kwa nchi za kasakazini mwa Sahara ni wakati wa fukuto
Wengi walitaraji kungalikuwa na nafuu ya Corona kwa kuzingatia pia chanjo imetolewa kwa sehemu kubwa

Kwa baadhi ya nchi za Ulaya , North America hali imekuwa tofauti na matarajio.
Kumekuwa na wimbi la tatu ''third wave' lililopelekea kurudi katika lockdown.

Watalaam wanasema kulikuwa na uharaka wa kufungua shughuli kabla ya chanjo kufikia 'herd immunity'' .

Hali ni tofauti nchini India ambapo vifo ni vingi na takribani watu 300,000 ni wagonjwa wapya wa siku moja.

Mifumo ya utoaji huduma '' healthcare ' imezidiwa na sasa ni misiba tu. Oxygen imekuwa bidhaa adimu huku watu wakifia ndani ya Ambulance na kupelekwa 'crematorium kwa cremation' moja kwa moja

Wiki kadhaa zilizopita India ilikuwa na sherehe za kidini ambapo watu huingia mtoni na kujimwagia maji.

Kwa aliyetazama ilikuwa ni hatari na kielelezo kwamba mbele ya safari kuna tatizo, tena kubwa.

Kwasasa kuna aina ya Virus ya India inayojulikana kama B.1.617 ambayo ni 'double mutant'. Watalaam bado wanatafakari kuhusu jina hilo . Kwa kifupi ni kuwa Virus si mpya bali amebadilisha 'code' za mwili wake inayokuwa na tabia tofauti na ile ya mwanzo. Yaani ni kama vile kubadili '' password''

India pia ina aina ya B.1.1.7 ya UK na P.1 ya Brazil. Haijulikani ni aina ipi hasa inayoleta dhahma kwa Wahindi.
Kinachojulikana ni kwamba hali ni mbaya sana na Mataifa ya dunia yamechukua hatua za dharura kukabiliana na hali hiyo kwa kupiga marufuku ndege na wasafiri kutoka India.

Mtaalam Gupta wa Cambridge University anasema kuna uwezekano mkubwa sana B.1.617 ikapunguza uwezo wa chanjo kukabiliana na ba Virus. Hata hivyo hayo ni maoni binafsi ya wataalam na yachukuliwe hivyo.

Ni kwa muktadha huo, Tanzania inakwenda katika majira ya baridi. Huu ni wakati ambapo Virus hustawi vizuri.
Kuna kila sababu ya kuamini kuwa hali haijaimarika na huenda kukawa na wimbi lingine kali kama lililopita.

Ni vema tahadhari ikachukuliwa kuhusu wasafiri kutoka India kwasababu kimazingira hatutofautiani sana na hivyo basi Virus akiingia linaweza kuwa tatizo kubwa .

Pamoja na hayo bado umuhimu wa chanjo upo pale pale na hatua zote zichukuliwe kukabiliana na janga.

Tuyafanye mambo kwa weledi tukiitazama dunia inavyozunguka. Ule ushamba wa kufikiri tunachofikiri ni sahihi ufike mwisho. Tuokoe maisha ya watu wetu kwa njia za kitaalam! maombi na Swala zibaki nyumba za ibada na kwa watu binafsi.

Wapambe wapate funda la maji, mbuzi wa jirani keshakula!
 
Asante kwa kuzingatia tena kwamba wimbi limepita, na lilikuwa wimbi lingine.
Yes kupita haina maana imeondoka. Kumbuka tunazungumzia 'wave' na unajua ni mkunjo wa high and low, ukiwa kati kati huwezi kusema umepita. Ukiwa juu au chini huwezi kusema umepita, ni hadi wimbi liondoke

Yes, ushamba wa kuita Corona changamoto! ushamba wa kukana masks, ushamba wa kuamini kuna makusudi
Sayansi ipo wazi isipokuwa tu kukumbatia ushamba.
 
Mkuu Nguruvi3, kama wewe hauko maabara mwenyewe, basi usiwe na 100% ya ukweli kuwa wazi kisa ni Sayansi.

Sayansi inaweza geuzwa kuwa Siasa wakati wowote. Ni hitajio tu linapotokea.

Nilitamani sana kujua ni nini hasa kiko ndani ya hili janga corona. Kwanini mara zote limekuwa kama linacheza mchezo wa kupishana njia?
Chanjo kutozuia Maambukizi,
Kuongezeka kwa Aina, nk yaani kwa namna yoyote linataka tuamini kuwa HALIWEZEKANI.
 
Mkuu , ni namna gani unaitumia sayansi ndilo jambo la muhimu sana.
Sayansi inaweza kutumika katika siasa, uchumi, jamii , kigaidi, kijeshi n.k.

Ugunduzi wa atoms na electrons ulipelekea ugunduzi atomic Bomb iliyoua halaiki kule Nagasaki na Hiroshima

Sayansi imeleta ugunduzi wa mabomu. Kisayansi mabomu ni ''combustion'' na hvyo basi combustion zinazotumika katika ndege , Magari na mashine nyingine ni 'mabomu' katika ''calculated amount''

Ndivyo ilivyo kwa dawa za binadamu ambazo ni ''sumu'' lakini sayansi inatuwezesha kunywa na kupona
Kwahiyo ukinywa dawa ni sawa na kunywa sumu katika kiwango kinachokubalika

Ni sayansi inatuwezesha kupeleka chombo maili 300 kutoka duniani kuangalia sayari nyingine.
Lakini pia sayansi inatuwezesha kutekeleza uchumi, shughuli za kijeshi, kijamii na siasa ikiwemo

Hoja ni kuwa sayansi haina tatizo, kuna tatizo wakati wa kutumia sayansi na watumiaji wa sayansi.
Kama unaambiwa virus wanaambukiza halafu unaamini si virus ni vita ya uchumi ! tatizo si sayansi.

Kuhusu hoja ya chanjo, hili nalo tumelijadili sana. Kwamba kuna jamii ya virus ambayo utengenezaji wa chanjo yake una challenges. Moja ya virus hao ni HIV-AIDS kwasababu za kisayansi (ndefu kuzieleza)

Ukisikia kuna mutation basi wapo virus wanafanya mutations kwa kasi sana na kwa namna tofauti kiasi kwamba vaccines iliyogunduliwa leo inaweza isifanye kazi baada ya mwezi.

Inategemea aina virusi. Katika nchi za magharibi ''flu' inapita kila mwaka na chanjo za flu ni kila mwaka.
Si jambo geni.

Kwahiyo ni lazima kwanza uelewe vaccines zinafanyaje kazi, zina target wapi, zinakuwa za aina gani.
Je, ni live atenuated? Je, ni extracts za proteins ? n.k. n.k.

Katika hili ni kuelewa sayansi . Tatizo kubwa lipo kwa wapiga ramli na madogori kama wale wanaotengeneza Togwa bila kueleza inafanyaje kazi. Ni kuongozwa na hisia tu!

Hatuwezi kuwa peke yetu kwenye dunia hii ! tumeumiza watu wetu kwa ujuha wa changamoto za kupumua
Tumejificha nyuma ya ujinga tukiamini tumejificha.
 
Hili ni jambo la muhimu, na naunga mkono hoja ya kuendelea kuchukua tahadhari.
Kuchukua tahadhari kuna aina mbili
Moja, kwa watu binafsi kujilinda ( masks, sanitizers etc)
Serikali; kuchukua hatua za dharura. Kwasasa ni muhimu kuzuia watu kutoka India
Sijui kama hatujachelewa!
 
Nilichomaanisha si Matumizi Mabaya ya Sayansi, bali ni Udanganyifu unaoweza kuwa ndani ya Sayansi.
Binafsi ninatambua wazi kuwa Hii Sayansi ya leo INA MIPAKA ya karibu sana, haiko perfect 100%. Bahati mbaya Utambuzi ulio nje ya mipaka yake umepewa laana na kukaririshwa watu na kuuimba kama barbaric way, ujinga, ushirikina, uchawi, nk...
Kinachouma zaidi sisi wenyewe kutumika kujilaani wenyewe kwa kujivunia ujuzi wa Sayansi za majuu ambazo hatuna hata Blue print zao.

Nikuhakikishie tu, Upo Ujuzi na Maarifa nyeti sana beyond hii Sayansi ya leo. Na uwezekano mkubwa zaidi, hao wanaotuletea hii yenye mipaka wanatumia juzi hizo beyond today's science, they won't tell you.

Kosa ni kutumia hizi Limited Scientific Laboratories, ku-asses science beyond today's science findings... Ni kutwanga Maji. Ni kujitia kitanzi.
 
Kuchukua tahadhari kuna aina mbili
Moja, kwa watu binafsi kujilinda ( masks, sanitizers etc)
Serikali; kuchukua hatua za dharura. Kwasasa ni muhimu kuzuia watu kutoka India
Sijui kama hatujachelewa!
Sayansi inatilia shaka maski. Na sanitaiza. Kutokana na makandokando kwenye tararila za KOVID.

Kuhusu kuzuia wasafiri kutoka India, hilo siafiki. Acha waje tu.

Kwenye ndege hawaruhusiwi kupanda mpaka wawe wamepimwa. Na wamevaa maski. Na kisha, natural progression ya mutation ya virii ni kuelekea less virulence. Kama vimemutate, so much the better. Vitakuwalikely less virulent.

Usitutishe!

Unataka tujae hofu in our approach to COVID. Hofu ni mbaya kuliko ugonjwa, nikinukuu maneno yaliyotuset free.
 
Sayansi inatilia shaka maski. Na sanitaiza. Kutokana na makandokando kwenye tararila za KOVID.
Kwamba masks zimewekewa virus kama tulivyoaminishwa? ha ha ha ha! Mzungu aweke Virus kwenye Masks?
Kuhusu kuzuia wasafiri kutoka India, hilo siafiki. Acha waje tu.
OK, kuna aliyewahi kusema 'waliokwenda nje ndio wamereta hii aina mpya''
Sasa likitokea la kutokea tutaelezana tu. Tulibishana hapa ukajisahau, kugeuka mbuzi kala mkeka!
Kwenye ndege hawaruhusiwi kupanda mpaka wawe wamepimwa. Na wamevaa maski. Na kisha, natural progression ya mutation ya virii ni kuelekea less virulence. Kama vimemutate, so much the better. Vitakuwalikely less virulent.
Kuna nchi wanapimwa airport walipofika na kubaini 30 wana B.1.617. Ni facts siyo hisia
Tanzania sidhani kama wanapimwa wakifika maana hata kipimo tuliambiwa hakifai

Kipimo kichotengenezwa na spec za virus kikapima mafenesi halafu tulitegemea majibu sahihi
Hakuna aliyefikri false negative or positive, tukaaminishwa ni vibaya huku wakichaji 300K kwa kipimo.

Kuhusu mutation, naomba urudi kwa aliyekueleza akueleze vizuri. Mutations inaweza kutoa majibu tofauti
Tumeona Variant ya UK (B.1.17) inasambaa haraka sana lakini siyo ''lethal'' kama ile ya South Africa
B.1.617 ya India ambayo ni double mutation inasemwa inaua na kusambaa haraka sana.

Mutation inaweza kuwa less virulent lakini mara nyingi inakuwa na severe virulence kwasababu miili inakuwa haina uzoefu. Hivyo ulichosema kina walakini. Hili la mutation tuliache maana nitakuumiza kichwa bure
Usitutishe!

Unataka tujae hofu in our approach to COVID. Hofu ni mbaya kuliko ugonjwa, nikinukuu maneno yaliyotuset free.
Hapana, wala sina nia hiyo. Ni habari tu zipo duniani na watu wanaziona sioni sababu ya kutoandika.
Ukitazama news za dunia , leo US, Indonesia, Pakistan wanaelekea kusaidia India.

Hatuna approach ya COVID. au unaamanisha kujenga mabanda ya kufukiza zaidi? MNH na Mloganzila!!
Kunywa Mpiji , covidol na NIMRcafe? Hatuna approach so far .

Labda kama awamu hii ina mipango, awamu iliyopita ilituaminisha madogori, maombi , Sala, mapambio na Swala. Ilifika mahali hatupati Coaster za kwenda mikoani!
 
maombi , Sala, mapambio na Swala
Hili ni eneo lingine ulilo na tatizo nalo. Kwani kuna shida gani kusema tumuombe Mungu huku tukiendelea kusikiliza wataalam? Au nawe chifu ni secular-humanist?
 
Back
Top Bottom