#COVID19 COVID-19 is historical in Tanzania: Why don't USA, UK, EU and others copy from Tanzania how to fight against the Corona Virus?

Nilichomaanisha si Matumizi Mabaya ya Sayansi, bali ni Udanganyifu unaoweza kuwa ndani ya Sayansi.
Maelezo yangu yalilenga kukuonyesha kuwa sayansi ipo open and vulnerable kwa abuse
Nikakupa mifano ambayo ikitumiwa vibaya sayansi itaonekana kama balaa

Udanganyifu kwa kutumia sayansi upo kama ule wa kuaimini uwepo wa '' (virus) wa kupandikizwa katika masks ili anayevaa avute hewa aathirike'' . Huu ndio udanganyifu wa kutumia '' maneno ya sayansi''

Sayansi inasema kuna virus wanaosababisha maradhi kwa mfumo wa hewa na njia ya ku-mitigate risks za kupata maradhi ni kuvaa masks.
Binafsi ninatambua wazi kuwa Hii Sayansi ya leo INA MIPAKA ya karibu sana, haiko perfect 100%. Bahati mbaya Utambuzi ulio nje ya mipaka yake umepewa laana na kukaririshwa watu na kuuimba kama barbaric way, ujinga, ushirikina, uchawi, nk...
Kinachouma zaidi sisi wenyewe kutumika kujilaani wenyewe kwa kujivunia ujuzi wa Sayansi za majuu ambazo hatuna hata Blue print zao.
Nikuulize kwani ni sayansi pekee ambayo hatuna blue print?
Nikuhakikishie tu, Upo Ujuzi na Maarifa nyeti sana beyond hii Sayansi ya leo. Na uwezekano mkubwa zaidi, hao wanaotuletea hii yenye mipaka wanatumia juzi hizo beyond today's science, they won't tell you.
Je ni sayansi pekee?
Kosa ni kutumia hizi Limited Scientific Laboratories, ku-asses science beyond today's science findings... Ni kutwanga Maji. Ni kujitia kitanzi.
Kwanini tunadhani Lab ni limited !
 
Tuwaruhusu waje, ila waje wakiwa na uthibitisho wa chanjo ya COVID.

Do you approve the above message?
No thank you.

Kuna nchi zilijaribu kuamini vipimo vya Tanzania ikiwemo Oman.
Kuwaruhusu waje kunafungua njia ya kuwa na certificates fake. India ni third world , mind you!

Nchi za mataifa zimepiga marufuku ndege kutoka India na Pakistan
 
Hukunielewa Mkuu, nilichomaanisha ni Uongo/Udanganyifu wa Sayansi, Si matumizi mabaya ya Sayansi.

Hii bookish science ya Leo haina majibu yote, still haiwezi kukubali juzi na maarifa mengine nje ya kanuni zake. KWANINI?

Lab ni limited kwasababu today's science is limited. Sayansi ya Leo haina majibu ya kila kitu...

Si Sayansi pekee ambayo hatuna blue print nayo, hakika. Ndio maana shaka yetu i juu ya kila kitu, na mwishowe kabisa tunaona haja ya Reforms.
Tunachojiuliza HAKIKA yenu inatoka wapi?????? Kiasi cha mtu mpaka kutamka kwamba "Tunataka Chanjo..." Hii hakika inatoka wapi? Kiasi cha kubeza aina yoyote ya cheche za reforms na kuzidunisha kabisa, Wapi wenzetu mnatoa Hakika yenu?

Nikuhakikishie tu, Yapo Maarifa mengi, makubwa na bora zaidi nje ya haya sayansi ya leo. Tufungue vifungo vyetu tupate kuelea katika bahari kubwa ya maarifa. Sayansi ya leo Imejaa HILA na GHIRIBA.
 
Hukunielewa Mkuu, nilichomaanisha ni Uongo/Udanganyifu wa Sayansi, Si matumizi mabaya ya Sayansi.
Sayansi haina uongo. Hii internet inayotuunganisha tukiwa sehemu tusizojuana ni sayansi si uongo
Sayansi ndiyo inayoongoza matibabu na tiba, udanganyifu na uongo wake upo wapi?
Ndege na magari tunayotumia ni sayansi, uongo wake upo wapi?
Binadamu katua mwezini na sasa wanatafuta '' madini'' huko Mars, uongo wa sayansi upo wapi?
Orodha inaendelea kwa page 1001

Kinachoweza kutokea ni watu wadanganyifu kutumia sayansi kwa njia za kidanganyifu au zisizokusudiwa
Nimekupa mfano
Hii bookish science ya Leo haina majibu yote, still haiwezi kukubali juzi na maarifa mengine nje ya kanuni zake. KWANINI?
Yes haina majibu yote. Haiwezi kukubali maarifa mengine yasiyo na ithibati.

Kwamba mtu aamke asubuhi na kusema majani ya mpapai yanatibu malaria basi watu wakubali kwasababu ni mbdala wa maarifa.

Hao ni wajinga na wapumbavu. Tumejaribu maarifa mbadala katika nyakati hizi, tumeonekana hayawani na kuchekwa.Maarifa mbadala lazima yawe na maelezo yanayoeleweka ! si ndoto za mtu
Lab ni limited kwasababu today's science is limited. Sayansi ya Leo haina majibu ya kila kitu...
Yes na sayansi haijawahi kukamilika ni 'work in progress''
Si Sayansi pekee ambayo hatuna blue print nayo, hakika. Ndio maana shaka yetu i juu ya kila kitu, na mwishowe kabisa tunaona haja ya Reforms.
OK kama tunakubaliana hilo tuachie hapo. Kuna mengi hatuna blue print lakini tunayakubali
Tunachojiuliza HAKIKA yenu inatoka wapi?????? Kiasi cha mtu mpaka kutamka kwamba "Tunataka Chanjo..." Hii hakika inatoka wapi? Kiasi cha kubeza aina youote ya cheche za reforms na kuzidunisha kabisa, Wapi wenzetu mnatoa Hakika yenu?
Cheche za reforms za kijinga hazitusaidii. Tulijaribu kwenda kununua dawa ya Covid Madagascar.
Huko Antananarivo wakazika hadi wakaomba msaada, ndio cheche hizo?

Tumejaribu kuchemsha majani hovyo kila nyungu na majani yake, tumepoteza watu wetu! ndio cheche hizo?

Maarifa yakwetu nayakubali pale yanapothibitika pasi na shaka.

Nisichokubali ni wendawazimu tu! kwamba leo aibuke mjinga mmoja atueleze Malaria inatibiwa na maji ya mto Ruvu nasi kwa ujinga tuzingatie na kukimbia kwenda Ruvu kuteka maji tukiimba nyimbo za shangwe na shamra shamra. Si kwamba tutakuwa wajinga tu, hata Mamba watatuona hayani na kututia vinywani mwao

Maarifa mbadala hayamaanishi ujinga mbadala

Chanjo tunazikubali kwasababu tumezitumia si leo si jana.

Chanjo kwa wenye weledi zina maelezo yanayotua katika bongo , lakini lazima awaye afungue akili kwanza na awe tayari kuitumia. Chanjo za wajanja zinafanya kazi kinyume chake unataka tuchemshe majani??
Nikuhakikishie tu, Yapo Maarifa mengi, makubwacna bora zaidi nje ya haya sayansi ya leo. Tufungue vifungo vyetu tupate kuelea katika bahari kubwa ya maarifa. Sayansi ya Imejaa HILA na GHIRIBA.
Yapo maarifa, yawekwe hadharani.

Hadi hapo tutakapo yabaini na kuyathibitisha sayansi ya leo ni mkombozi wa maisha ya mwanadamu.
 
Kuwaruhusu waje kunafungua njia ya kuwa na certificates fake. India ni third world , mind you!
Third-World status yao ni kwa ajili ya kugema rasilmali toka nchi za Magharibi, na kufaudu upendeleo wanaopewa nchi za Dunia ya Tatu toka taasisi za kifedha za kimataifa. India inatengeneza chanjo yake yenyewe ya korona. Ni space-faring nation. Ni Nuclear-armed nation. How much more first-world can a nation be?

Iinaonekana hauamini tu kwamba chanjo+(mask+testing wanavyokuwa subjected wasafiri wa kimataifa) inaweza kuwa na manufaa ya afya ya jamii.
 
Hapana! chanjo wanayotengeneza ni AstraZeneca ambayo si 'intellectual property ' yao.
Leo wameomba wapewe materials zaidi ya kutengeneza

Kinachotokea India ni capacity yao ya kutengeneza ni kubwa na ni cheap kwahiyo kuna 'sourcing' ili kuweza kupunguza gharama za chanjo zinazokwenda nchi masikini.

Kuhusu first world, hata sisi ni uchumi wa kati lakini je, tukilanganisha na zenye uchumi wa kati tupo?

Nchi ya uchumi wa kati kama 'Tanzania' inatoa vyeti vya Corona halafu vinakuwa proved ni fake.
India ina watu wengi na moja ya sifa yao ni 'forgery'
Ukiamini wana satellite na Nuke basi uamini kila kitu chao utakuwa doomed

Hivi umeona umasikini ulivyotamalaki India? Usione hao wa Dar, nenda Mumbai utashangaa! Abject poverty
 
Kutaka Ithibati ya kisayansi ya Maarifa na juzi zilizo nje ya kanuni za Sayansi ya leo, ni Self Enslavement. Ni kujifungia kwenye kaboksi kadogo ka maarifa.

Jifunze zaidi nje ya unavyoaminishwa...

Hao waliotumia chanjo India wanapukutika na Huduma bora za kiafya juu, wale wa nyungu tupo na athari ndogo(Sijajua unaishi wapi kwa sasa, ila hali unayotaka kutuaminisha ni Uongo) Bado hukubeza chanjo, na umekubali kulishwa maneno ya ati kirusi kipya. KWANINI HUONI SHAKA YOYOTE JUU YA KILA WASEMACHO?

Katika Ulimwengu wa Utambuzi, unaogopaje kuchekwa Mkuu? Tena na wapumbavu?

Unachokiita Mafanikio ya Sayansi hayahalalishi kutokuwepo kwa Uongo ndani ya Sayansi. Upo.
 
Hapana! chanjo wanayotengeneza ni AstraZeneca ambayo si 'intellectual property ' yao.
Leo wameomba wapewe materials zaidi ya kutengeneza

Kinachotokea India ni capacity yao ya kutengeneza ni kubwa na ni cheap kwahiyo kuna 'sourcing' ili kuweza kupunguza gharama za chanjo zinazokwenda nchi masikini.
Ni kweli wanatengeza AstraZeneca under licence. Lakini pia wanayo chanjo ya Covaxin ambayo ni ya kwao wenyewe. Angalia:

Kuhusu first world, hata sisi ni uchumi wa kati lakini je, tukilanganisha na zenye uchumi wa kati tupo?
Kuhusu sisi kuwa uchumi wa kati huwa ninatatizwa na uwezekano wa mawili yanayokinzana:
1. Kwanza, ni kweli tumefikia uchumi wa kati. Kongole kwa CCM chini ya uongozi shupavu wa JPM kuwezesha kufikia hapo mapema.
2. Pili, si kweli tumefikia uchumi wa kati, lakini 'mabeberu' wenye kuionea donge nchi yetu waliamua 'kutusulubu' kwa kutuvika kilemba cha ukoka kwamba tuko uchumi wa kati, ili waihujumu kasi kubwa ya maendeleo iliyokuwa ikionyeshwa na serikali yetu tukufu. Kwani, nchi zenye uchumi wa chini hupokea nafuu nyingi kwenye mikopo na mahusiano ya kibiashara kuliko zenye chumi za kati.

India ina watu wengi na moja ya sifa yao ni 'forgery'
Ukiamini wana satellite na Nuke basi uamini kila kitu chao utakuwa doomed

Hivi umeona umasikini ulivyotamalaki India? Usione hao wa Dar, nenda Mumbai utashangaa! Abject poverty
That is one broad brush to use against a nation. Tukiipeleka hoja hiyo mbele zaidi, ina maana hata nchi za Kiafrika, ambazo ni masikini zaidi, tutasema nazo zinafanya usanii tu kwenye masuala haya ya chanjo ya korona. Kwa hiyo we should not take them vaccination claims seriously.

So, still... we either still allow Indians to arrive as we allow anyone else, or, we can force them to come here already vaccinated.

Let us give them the benefit of doubt kwamba watachanja kweli. Or for the purpose of discussion, kwamba watachanja kweli.
 
Ni kweli wanatengeza AstraZeneca under licence. Lakini pia wanayo chanjo ya Covaxin ambayo ni ya kwao wenyewe. Angalia:

China walitengeneza yao , just to realize haifanyi kazi. Wamekubali kuiacha. Hii ya India sijui vipi maana wanaomba materials kutoka US na Europe
That is one broad brush to use against a nation. Tukiipeleka hoja hiyo mbele zaidi, ina maana hata nchi za Kiafrika, ambazo ni masikini zaidi, tutasema nazo zinafanya usanii tu kwenye masuala haya ya chanjo ya korona. Kwa hiyo we should not take them vaccination claims seriously.
OK, tuna choice kama ile ya Madagascar ! iliyoishia na aibu tu . Tukaonekana hayawani na kuwa cheko la dunia
So, still... we either still allow Indians to arrive as we allow anyone else, or, we can force them to come here already vaccinated.
I can't trust any Cert of vaccination from India. Indians are crooks like our' Nigerian broda'
Let us give them the benefit of doubt kwamba watachanja kweli. Or for the purpose of discussion, kwamba watachanja kweli.
OK, but here is the fact , B.1.617 is ravaging India, the health care system is near collapse
Wameruhusiwa kuzika watu in a backyard, crematorium ziko overwhelmed

Tulisikia variants ya South Africa na hapa jamvini tukasema ni tatizo. Tulipuuzwa lakini wakati unaeleza, kilichotokea tunakumbuka not long ago.

Ukitazama kinachotokea India kuna mambo ya kujifunza
1. Kwamba Hospitali lazima zijiandae na hapa kwetu tunaweza kuwa na tents kwa ajili ya wagonjwa
2. Hospitali zitafute namna ya kuwa na oxygen za kutosha , na mitungi iwe tayari. O2 haiozi
3. Kuwe na watumishi wa afya tayari ikiwa kutatokea idadi kubwa ya wagonjwa . Andaa wastaafu etc
4. Elimu ya makusudi kwa umma kuonyesha nini kinaendelea India ili watu wajue ukubwa wa tatizo

Haya tunayasema si kwasababu ya kutisha watu.
Kuna uwezekano isitoke kabisa lakini tahadhari ni bora kuliko kushtukizwa na panic katika ugonjwa.

Huko nyuma tulidanganywa kwamba hofu inaua zaidi, tukabweteka huku tukizika kwa mfululizo.

Tukaambiwa tusipovaa mask hakuna corona, yaani kama kuna eneo watu hawana mask basi hakuna corona
Huu ujinga tukaumbatia badala ya kukumbatia tahadhari, tukalipa gharama kubwa

Tukaambiwa tusiseme COVID tuite changamoto ya kupumua ili kuficha ukweli, haikutusaidia tukazika

Tujifunze kutokana na ujinga uliopita siku za nyuma. Kwamba tuchukue tahadhari na kwamba ugonjwa upo duniani na unau watu. India, US , Brazili , UK, n.k. zinatueleza

Tusijifariji kwa kutokuwepo tatizo! B.1.617 ikitua kutoka India tunaweza kuwa na tatizo hasa majira haya ya baridi

Wapambe tusikilizeni mkiwa upenuni, mbuzi kala mkeka....
 
Tukaambiwa tusipovaa mask hakuna corona, yaani kama kuna eneo watu hawana mask basi hakuna corona
Huu ujinga tukaumbatia badala ya kukumbatia tahadhari, tukalipa gharama kubwa

Tukaambiwa tusiseme COVID tuite changamoto ya kupumua ili kuficha ukweli, haikutusaidia tukazika
Kumbe ni simpo tu ufumbuzi ni kuvaa mask! Kwa nini Wahindi hawavai mask ili wasiambukizwe? Na wao kwani wameacha kuiita COVID?

Kama huamini cheti cha India, would you distrust their vaccine too?
 
Kumbe ni simpo tu ufumbuzi ni kuvaa mask! Kwa nini Wahindi hawavai mask ili wasiambukizwe? Na wao kwani wameacha kuiita COVID?

Kama huamini cheti cha India, would you distrust their vaccine too?
Ni hivi kuna mshamba alisema '' Hakuna corona kwasababu watu hawavai mask''
Yaani kwavile watu hawavai mask basi hiyo ni ishara ya kutokuwepo corona. Hayo si maneno yangu ni ya mtu

Kuhusu kuvaa mask, bado narudia kusema hatua za kujikinga ni muhimu. Social distancing, kutumia sanitizers, kuepuka unnecessary crowds, kuzuia shughuli zinazokusanya watu n.k.

Sisi ''tulijaribu'' kwa kukemea mask kanisani , tena tukiwasifu wasiovaa

Vaccine inayotengenezwa under license kutoka India Yes. Hiyo Cova.... ya India watumie wenyewe kwanza

Wapambe mlikataa ya South Africa tuka prove wrong! Sasa kuna B.1.617 I hope I'm wrong! and I pray so , otherwise ni balaa jingine.

Wapambe mtahangaika, mbuzi kala mkeka mtakalia nini?
 
Mlenge

All is good this side, tumemaliza msiba na safari yetu bado inaendelea kumkomboa Mwafrika katika koti kuu kuu ambalo wazungu wamelivaa na kuligubika bara letu.
Safari ya kumkomboa Mwafrika aelewe kuwa majani ya ng'ombe hayatibu Virus unless yatafitiwe
Safari ya kumkomboa Mwafrika kuwa Mungu alitoa akili zitumiwe. Elimu ikiwemo ya Virus ni sehemu ya matumizi

Mkuu pole na kuanua tanga, karibu tuelimishane maana safari ya kumkomboa Mwafrika ni ndefu
 
Hii variant ya India naona inapukutisha vibaya huko. Tuombe isifike huku kwetu!
Tumetoa angalizo kuhusu B.1617. Kama kawaida Wapambe wakatumbia eti '' Usitishe watu''.
Huko India watu wameruhusiwa hata kuchoma wapendwa wao katika back yard
Kule crematorium ni foleni ya kwenda kuwachoma wapendwa na kila dakika 5 kuna 'mpya' inaingia

Kwa Tanzania kuna good and bad news
Kwanza, hatutaweza kujua kama B.1.617. Tulizuiliwa kutoa takwimu au tafiti na Marehem.
Hatuwezi kufanya gene sequencing. Kwahiyo hakuna hofu na wala watu wasiohofu

Pili; Hatutajua ila tutahisi tu kutokana na taarifa mbali mbali .

Natamani yote hayo hapo juu yasiwe kweli, na kwamba, tulichosema hakitatokea na kitabaki hadithi
 
Back
Top Bottom