COVID-19 is historical in Tanzania: Why don't USA, UK, EU and others copy from TZ how to fight against Coronavirus?

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,111
2,000
Rais Rajeolina mjanja sana. Yawezekana yeye hata kuionja hakuthubutu ila alijua wajinga wametamalaki miongoni mwetu na kweli kwa namna walivyoubugia huo ushombwe sina hamu. Kwa mbali nakumbuka kikombe cha babu na barabara ya kuelekea Loliondo ilivyochongwa haraka haraka ndani ya saa 24...masikini Wadanganyika, we never learn.
Hapa kwetu kuna mabanda yalijengwa Muhimbili na Mloganzila, lakini kuna wakati tunakwenda Nairobi

Rajoelina kauona ukweli kwa watu wake waliopoteza maisha sana na kwingine.
Hukusibiri ushuhuda kageuka nyuma na sasa kaiangukia WHO. Anataka chanjo.

Ni wakati sasa tupate chanjo. Makampuni ya dunia yametenga dozi milioni 400 kwa Afrika. Ni bure

Somalia na Al shabab wanatoa vaccine, sisi tunasubiri nini?

Mapapai hayafai wala mazoezi ya kukimbia si tiba! mvinyo wa NIMR hauna ithibati ni kama wa Madagascar

Tuukubali ukweli kwasababu umedhihiri, virus haihitaji mzaha malipo yake ni makubwa kwa watu wetu

Vaccine ililetwe wanaotaka wapate wasiotaka wasibughudhiwe
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,857
2,000
Let us point out clearly for those just tuning in!

1. About Masks

Myth:
Wearing mask is the only way to protect one from Coronavirus. Forcing everyone to wear a mask, it is a highlight of a caring national administration.
Reality: In science, there are debates as to the effectiveness of masks. See


2. About Lockdown

Myth:
Locking down healthy populations is the only way to protect them from COVID-19. A caring administration locks down its population.
Reality: Lockdowns may be more harmful. See


3. About Social Distancing

Myth:
Social Distancing is the only way to protect yourself and others from COVID infection in social situations.
Reality: Social Distancing may not be as effective as it is touted to be. See


4. About COVID-19 Vaccines
Pana hii video ya kichochezi imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii Tanzania hivi karibuni...


View attachment 1735140
SOURCE: a viral social-media video


There is a NATIONAL GUIDELINE OF CLINICAL MANAGEMENT AND INFECTION PREVENTION AND CONTROL OF NOVEL CORONAVIRUS (COVID-19). The document shows the directives from the ministry responsible for health in Tanzania. You can see for yourself how the MoH guides the fight the disease. The MoH uses science. The document has been making rounds in Tanzanian social media. I am not sure of the aunthenticity of the copy making rounds, though. Here it is attached.
 

Attachments

  • File size
    1.7 MB
    Views
    2

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,111
2,000
There is a NATIONAL GUIDELINE OF CLINICAL MANAGEMENT AND INFECTION PREVENTION AND CONTROL OF NOVEL CORONAVIRUS (COVID-19).
Kama sikosei hiyo ni nyaraka ya 2019. Kama Document hii ni authenticated itakuwa outdated. Kwa miaka 2 kumekuwa na development katika maeneo mengi.
The document shows the directives from the ministry responsible for health in Tanzania. You can see for yourself how the MoH guides the fight the disease. The MoH uses science.
Not True! ukusanyaji wa data ulipigwa marufuku na ndio ulimuondoa Prof na Naibu Waziri wakati huo
Waziri aliyepo alihimiza mazoezi na kutafuna mananasi na kukimbia na vibuyu vya maji.

Ukitazama guideline hakuna mahali imeeleza hilo.
Naibu wake aliyeondolewa alipingana na WHO kuhusu data akitoa majibu ya hovyo

Waziri akatamka hakuna mpango wa chanjo , tutaendelea kuchemsha majani ! hiyo ni Science kweli

Rais Marehemu alionya Wizara ya afya kutofuata miongozo bali kuhimiza ufukizaji wa nyungu

Waziri wa TAMISEMI siyo wa Afya akatangaza nyungu season 2

Marehemu akapiga marufuku vaccines huku akitilia shaka masks kwamba zimewekewa wadudu. Hiyo ni science?

Wizara ya Afya haikuwahi kukanusha au kusema lolote

Mabanda ya kuhemea yakajengwa MNH na Mloganzila. Guideline haina na sijui ni science gani ilifuatwa hapo

NIMR wakaja na NIMRCafe ,Covidol na Mpiji ambazo hazijathibitishwa popote pale isipokuwa Tanzania tu!
Hapa kuna Science kweli!

Ikatumwa ndege kwenda kchukua Dawa Madagascar, dawa isiyothibitishwa. Hiyo ni Science?

Kusema eti kuna muongozo wa Science ni kumkana mwendazake na kuyakana maneno yenu ninyi wapambe.

Msimkimbie mwendazake hata kabla ya 40. Hamkujua kuwa mlitumika tu?

Nina hakika nafsi zinawasuta na sasa mnataka kurudi katika science baada ya umbuko !

Tunahitaji vaccines hayo makabrasha warudishe MoH, hayana maana kwasababu hayakuwa na maana miaka 2 eti leo baada ya safari ya mtu ndiyo yanatumbukizwa mitandaoni!
The document has been making rounds in Tanzanian social media. I am not sure of the aunthenticity of the copy making rounds, though. Here it is attached.
Hayana maana ni outdated na hayakutumika kusaidia watu sijui kwanini yatumike sasa

Jaribu kutafuta 'authenticity' lakini ni likely hii ni Doc ya serikali
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,857
2,000
Kama sikosei hiyo ni nyaraka ya 2019. Kama Document hii ni authenticated itakuwa outdated. Kwa miaka 2 kumekuwa na development katika maeneo mengi.

...
Umeisoma dokumenti?

"Ukitaka kumficha kitu Mswahili, weka kwenye maandishi."
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,111
2,000
Umeisoma dokumenti?

"Ukitaka kumficha kitu Mswahili, weka kwenye maandishi."
Oh sorry ni ya March kama ni authenticated
Haikuandikwa kiufundi ninakuhakikishia

Siyo tu nimesoma mimi nina detail za kila mstari na ninaweza kukuonyesha outdated info ndani yake

Lakini kwa vyovyote iwavyo je, inabadilisha uzembe uliofanyika chini ya uangalizi wa watu hao hao?

Je, unabadilisha ukweli kuwa mabanda ya hovyo yalijengwa MNH? na waliosimamia ni hao hao

Why now!

Watu wamekufa sana, why now!

Halafu wapambe wanaitembeza mitandaoni wakati watu wasio na hatia wamelipa gharama za maisha yao kwa utashi wa watu wachache na kukosa maadili kwa wapambe wao

Tunataka chanjo hatutaki hadithi nyingine . Ni chanjo tu

''Mbuzi kala mkeka wapambe mtakalia nini?''
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,111
2,000
Si ndio maboresho yatokanayo na sayansi mpya na uzoefu? Miongozo ya awali ilikuwa ya 2020. Mingine ipo pia.

E.g.;

Discharge Criteria

Sekta ya Misitu

Usafiri wa Anga

n.k.
Mlenge hakuna sayansi mpya, kuna dharura inayohitaji kubadilika na kwenda na muda kama wafanyavyo wengine duniani. Mwaka 2019 Covid ilikuwa death sentence, kwa maana ukiipata madaktari hawakujua nini cha kufanya, kwasasa Covid inakuwa 'managed' vizuri tu

Hicho unachokiita maboresho ni hatua zilizopaswa kuchukuliwa siku nyingi. Kwa jicho la public health hatua za kukabiliana na maradhi yanayoambukiza huchukuliwa kwa ujumla wake ''holistic'

Ukianza na mistu, sekta ya anga na discharge unapaswa kwenda mbali zaidi kwa kuangalia interactions, transportation zingine kama meli, mabasi n.k. bila kusahau mikusanyiko kama Kariakoo

Kuna mambo yanayoonekana kama hatua nzuri. Kwanza, Rais Samia ameufuta salamu za kidini
Kumbuka ni salama hizo ndizo ziliendelezwa na kuaminisha watu kwa kutumia aslama alaykum na Bwana Yesu asifiwe basi maradhi yanaondoka. Watu wakaambiwa wasihangaike na sayansi ! upuuzi uliogharimu roho za watu

Hatua ya pili ya Rais Samia ni kukubali kuwa kuna COVID-19. Rais hakuita changamoto au kutumia maneno mengine kuficha ukweli. Hii ni hatua nzuri kwani ni mwanzo wa kuliona tatizo

Hatua ya tatu ni kuunda timu ya watalaam. Hii nayo imechelewa lakini watalaam hao wanakazi moja kubwa , kuangalia namna gani tunakabiliana na maradhi tukiwa sehemu ya dunia lakini pia tukiangalia masilahi yetu

Rais Samia kasema sisi si kisiwa ni sehemu ya dunia. Huu ni ukweli usiohitaji elimu au certificate yoyote

Hatuwezi kujitenga na dunia tukidhani tuna mbinu za hovyo za maombi na mabanda ya kufukiza tu kwasababu mtu mmoja alitaka iwe hivyo hata kama ni kwa gharama za maisha ya watu.

Hatua ya nne ya Rais ni kutofanya 'promo' za mitishamba isiyotafitiwa wala kufanyiwa ithbati .

Kwahiyo Rais Samia amefanya mambo mawili muhimu katika wakati huu
1. Ku-rest position ya Tanzania katika ulimwengu iliyoharibiwa vibaya kwa miaka 5 iliyopita
2. Kukabliana na ukweli wa COVID-19 kama ulivyo bila kubabaisha, kudanganya au kupotosha

Kumbe basi tunachokiona sasa hivi kwa hii miongozo inayotolewa na kuletwa hapa jamvini na tunaposikia Rais akisema ni dhahiri wengi hawakupendezwa na jinsi utawala uliopita ulivyoshughulikia tatizo la Covid

Swali la kujiuliza ni kwanini tuliacha watu wetu wapoteze maisha kwa kuogopa kusema ukweli?
Madaktari na watalaam wanaoamka sasa walikuwa wapi?

Ili kumsaidia Mh Rais wapambe wakae pembeni. Maprofesa uchwara na waongo wakae pembeni.
Taasisi zilizopoteza heshima kama ile ya utafiti wa magonjwa zikae pembeni
Wapambe katika mitandao wachukue likizo bila malipo

Muda wa kudanganywa na changamoto , majani ya kuchemsha na mapambio umeondoka na haupo tena
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,857
2,000
Mkuu Nguruvi3 ,

Mikusanyiko Kariakoo... Kwa hiyo unataka lockdown? Utalisha ambao rizk zao ziko kwenye kutoka kila siku, na hazipatikani kwenye Zoom meetings?

Yaani Nguruvi3 solution ya nchi zenye uchumi wa juu unaileta kwenye nchi inayoibukia?
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,857
2,000
Hiyo miongozo ni mifano tu kudebunk disinformation campaign yenu mnayoinsinuate kwamba nyungu, maombi, na tibalishe ndio zilikuwa njia pekee za nchi kupambana na korona.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,111
2,000
Mkuu Nguruvi3 ,

Mikusanyiko Kariakoo... Kwa hiyo unataka lockdown? Utalisha ambao rizk zao ziko kwenye kutoka kila siku, na hazipatikani kwenye Zoom meetings?

Yaani solution ya nchi zenye uchumi wa juu unaileta kwenye nchi inayoibukia?
Nadhani ni jambo jema kutopotosha alichoandika mchangiaji. Soma aya hii

''Hatua ya tatu ni kuunda timu ya watalaam. Hii nayo imechelewa lakini watalaam hao wanakazi moja kubwa , kuangalia namna gani tunakabiliana na maradhi tukiwa sehemu ya dunia lakini pia, tukiangalia masilahi yetu''

Hakuna mahali tumesema 'lockdown' zaidi ya kusisitiza maneno tukiangalia masilahi yetu.
Hii ina maana nyingi, kwamba, tunaweza kutoa elimu kwa husika katika kutumia mask na social distancing

Pili, tuwaondoe wahusika ujinga waliojazwa kwamba covid inaletwa na wazungu kwa kutuonea gere.

Kufuta upuuzi uliojengwa vichwani mwao kuwa mapambio, maombi na swala na sala ndio tiba ya tatizo.

Katika kuangalia matatizo ya afya kwa miongozo ya public health , primary health care inahusisha education. Kwamba unaweza kukabiliana na tatizo kwa njia zote lakini muhimu ni watu kulielewa tatizo

Hatua za kuzuia ugonjwa usiingie nchi zimepitwa na wakati kwani aina zote zipo Tanzania.
Kinachotakiwa ni kukabiliana na ugonjwa ukiwa ndani ya nchi.

Huwezi kukabiliana na maradhi bila kuwa na data. Data zinasaidia kuelewa ukubwa wa tatizo, wapi tatizo lililpo na linahusisha nini na kina nani ni waathirika. Bila data huwezi kujua hot spots

Hapa ninahoji, hao waliotoa miongozo hiyo walitumia vigezo gani? Huwezi kutoa muongozo bila data.

Matokeo yake tunaona muongozo wa wasafiri wa anga, kasehemu tu ka wasafiri wa nchi kavu na majini.

Usafiri wa anga si tatizo kama la la dala dala. Tujiulize kwanini usafiri wa anga kwanza?

Misitu, hivi kweli tunahitaji muongozo wa misitu badala ya muongozo ya masoko ya Kariakoo na Tandale n.k?

Muongozo wa ku discharge wagonjwa ni 'internal memo' ya watu wa afya haihusu jamii kwa sehemu kubwa.
Lakini basi unatoaje muongozo wa ku discharge wakati hakuna vipimo vya Corona?

Nimalizie kwa bandiko lako la 'ku debunk' hoja kuwa hakuna juhudi. Hii miongozo inatoka baada ya kuondoka.

Marehemu alihubiri kanisani kwa mara ya mwisho akiwajibu maaskofu. Katika mahuri yake alisifia wasiovaa barakoa. Mikutano yote aiyofanya hakuwahi (nisahihishwe) kuvaa barakoa

Aliaminisha watu hakuna Corona ndio maana kulikuwa na changamoto.

Akaaminisha watu vipimo ni fake lakini serikali anayoongoza ikitumia vipimo hivyo fake kwa Dola 100 !!

Aliaminisha watu maombi , sala mapambio na kuchemsha majani ya ng'ombe au kondoa yanaponyesha changamoto.

Chanjo ilikataliwa kwamba eti inaletwa kutu ua.

Katika mazingira hayo, unaweza kusema aliwahi kusikiliza hii miongozo au kujua kama ipo?

Mbuzi kale mkeka wapambe mtakalia nini?
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,857
2,000
...
Hii ina maana nyingi, kwamba, tunaweza kutoa elimu kwa husika katika kutumia mask na social distancing

....
Kwa hiyo unataka watu wa Kariakoo walazimishwe kuvaa barakoa na wapigwe marufuku kukusanyika. How is the mask and lockdown diktat thingy working for you over there? And you want that in the Kariakoo-Shimoni situation? Siyo kila homa ni maleria.


...
Mbuzi kale mkeka wapambe mtakalia nini?
Nshakufahamu!
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,111
2,000
Kwa hiyo unataka watu wa Kariakoo walazimishwe kuvaa barakoa na wapigwe marufuku kukusanyika. How is the mask and lockdown diktat thingy working for you over there? And you want that in the Kariakoo-Shimoni situation? Siyo kila homa ni maleria.
Mkuu ni hivi, ukiwa na tatizo hutafuti majibu ya mkato au rahisi. Hutafuti majibu yasiyotoa majibu.

Hao watu wa Kariakoo shimoni usiwadharau ni wanadamu na wana ufahamu.

Tatizo linalotukabili Waafrika ni ''approach' ya matatizo kama unavyofanya au kufikiri.
Hili limetuharimu wakati wa COVID tukihamisha tatizo kwa Wazungu bila sababu

Wenye busara wanasema kwamba '' ukiwa na kinywa (kwa wenye heshima) au domo kwa wanaobwawabwaja kuna mambo makuu mawili ya kuyaangali. Moja, uongee kwa busara , pili, ufunge mdomo usioongee kabisa

Wananchi wana ufahamu mzuri sana. Kilichotakiwa ni hiki
1. Kuwaeleza tatizo na ukbwa wake na jinsi ugonjwa unavyoonea
2. Kuwaeleza namna ya kujikinga kwa kutumia social distancing au Mask
3. Kusikiliza changamoto zao na wao wanafikiri nini kifanyike
Hapa utafungua mdomo kwa busara

Kisichotakiwa ni kufungua mdomo
1. Kuwaambia hakuna ugonjwa wa Corona , hizo ni propaganda za Wazungu kuna changamoto
2. Kuwaaminisha kuna mapambano na vita kubwa sana ya uchumi, Corona ni moja ya silaha za adui
3. Kuwaamininisha majani ya michongoma, ya ng'ombe na ngogwe ni tiba ya changamoto
4. Kutumia media na mitandao kuwapotosha kwa habari za kubumba , uongo na uzushi
4. Kuwaambia matatizo (1,2,3) hapo juu yataisha kwa maombi, sala , mapambio na uzalendo n.k.

Ni rahisi sana kubomoa hiyo miongozo ya usafiri wa anga, misitu na discharge kutoka Hospital

Hivi discharge linakuwaje public problem bada ya kuwa professional approach.

Wanaotengeneza miongozo wana takwimu za kuwaongoza?

kama hawana wanatumia nini kufanya analysis ya tatizo?

Haya hayatokei kwasababu hawajui,la hasha! ni kwasababu siasa iliingia utalaam.

Duniani kote kuna mananasi tukaona kiongozi wa afya akila mananasi na kukimbia hovyo barabarani kama tiba ya Covid. Hivi mtu kama huyu anatuvusha vipi katika nyakati tulizo nazo?

Wapambe mumekalia nini?
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,857
2,000
...
Hili limetuharimu wakati wa COVID...

...

Congratulations Nguruvi3 for being the first to yet again refer the COVID-times in past-tense. You have brought us right to the time-period when this thread was posted. And, you are right. By the look of the hustle-and-bustle of Tanzanian daily living, people live their lives as if COVID is yet-again referred to in the past-tense, as you JUST did. And guess what? The fanatical obituaries posted in the social media, accompanied with insinuation of death by COVID, have dwindled spectacularly, hugging the horizontal axis of the graph. Thank you so much for pointing this out.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,111
2,000
Congratulations Nguruvi3 for being the first to yet again refer the COVID-times in past-tense. You have brought us right to the time-period when this thread was posted. And, you are right. By the look of the hustle-and-bustle of Tanzanian daily living, people live their lives as if COVID is yet-again referred to in the past-tense, as you JUST did. And guess what? The fanatical obituaries posted in the social media, accompanied with insinuation of death by COVID, have dwindled spectacularly, hugging the horizontal axis of the graph. Thank you so much for pointing this out.
Sijui ni past ipi unayozungumzia kwa Tanzania. Mahali tulipoambiwa 'hata watu wakifa hawatakufa wote'' hakuna '' times in past tense '

Kwa nchi za wenzetu kupoteza watu ni issue kwa Tanzania ' tuliambiwa tufukie vichwa mchangani adui hatatuona'

Kuhusu ''fanatical obituaries '' kwa wasioelewa ugumu na ukubwa wake ulichosema ni sawa.

Kwasisi wa mitaani tunaotafuta Coaster na zingine zikiwa zimeandama misururu , kwa wale inayobidi wachague bega ni msiba upi wa kuhudhuria kwanza na upi ufuate, na wale wanaofikiri wataomba vipi ruhusa ya kwenda msibani tena '' fanatical obituaries' ni matusi sana.

Tunaweza kutofautiana kwa mambo mengi lakini si kwa maisha ya Mwanadamu

Kuna picha inazunguka mitaani ikionyesha watu 4 katika nafasi kuu ya nchi wote wakiwa ni marehemu.
Hivi hiyo picha unaweza kuiita fanatical obituaries

Kweli kuna mtu anaweza kutoa picha au tangazo la msiba wa mpendwa wake 'for fun' ili tuweze kuita fanatical obituaries. Please, kama kuna kitu Corona imetufundisha ni ubinadamu

Tumeona watu wakionyesha ubinadamu wa hali ya juu, na pia kukosa ubinadamu kwa kiwango cha kutisha

Kukataa chanjo ambayo wapo waliokuwa tayari kuinunua kwa bei yoyote kwa maisha yao au Wapendwa wao ni moral decay ya hali ya juu sana.

Kudanganya watu kuhusu Corona ni mora decay na wale waliohusika kudanganya kwa kudhamiria au kwa matumbo nao pia ni wadhulumu kama wengine wote.

Tunahitaji chanjo sasa, hatuhitaji kamati za Maprofesa kama yule aliyengeneza Togwa na Mtindi

Hatuhitaji kamati itakayosimamiwa na wala mananasi na kutembea hovyo kama tiba ya Covid

Rais Samia kasema Tanzania si kisiwa bali sehemu ya dunia.

Maneno haya yanafariji kwamba sasa tumetoka katika lindi la udwanzi wa kukataa sayansi ili watu wakalime wakiwa wanauguza na misiba!!! Real ?

Tukishindwa Lockdown, mask or social distancing tuna Vaccination.

Wapambe! anueni tufungue mtaa, mbuzi kala mkeka! mtakalia nini?
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,857
2,000
Why do Nguruvi3 brand anyone who died in the past three or so months, as death caused by coronavirus? Did all other causes of death cease to kill people? Didn't you see people online tagging every death as COVID-death, even when the families provided the real reasons for the death?

Kuhusu chanjo, ije tu. Tutachanja kila mmoja kwa hiari yake. Mradi tu msihamishe magoli kutaka kulazimisha ambao hawatachanjwa wachanjwe. Wala pasiwe na vizuizi au ubaguzi kwa waliochanjwa au wasiochanjwa.

Kwa anayeelewa, atusaidie ukweli kuhusu yafuatayo:

1. Mpaka sasa zipo chanjo kadhaa zilizo sokoni. Tuchukue ipi? Ya China, Urusi, Uingereza, Marekani, au ya Uganda (inayotajwa kuwa mbioni kutengenezwa)?

2. Pamekuwa na maneno mitandaoni kwamba chanjo zilizoko hazizuii aliyechanjwa kuambukizwa virusi vya korona. Je ni kweli?

3. Pamekuwa na maneno mitandaoni kwamba chanjo zilizoko hazizuii aliyechanjwa kuambukiza wengine virusi vya korona. Je ni kweli?

4. Pamekuwa na maneno mitandaoni kwamba chanjo zilizoko hazizuii aliyechanjwa kuumwa COVID-19, ila uwezekano mkubwa hataumwa sana. Je ni kweli?
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,111
2,000
Why do Nguruvi3 brand anyone who died in the past three or so months, as death caused by coronavirus? Did all other causes of death cease to kill people? Didn't you see people online tagging every death as COVID-death, even when the families provided the real reasons for the death?
Hili si tatizo la watu au Familia, ni tatizo lililotengenezwa na Serikali. Kitendo cha kuzuia uksanyaji wa takwimu ndio mzizi wa tatizo. Homa (fever) si ugonjwa ni dalili (symptoms) za ugonjwa na inaweza kuwa magonjwa zaidi ya 100. Ukikataza uchukuaji wa data wakati kuna tatizo kubwa katika jamii kuna maana moja, unaficha jambo

Unapokataa kutaja maradhi husika na kuita changamoto, unaficha jambo. Kwa vile hakuna ugonjwa wa changamoto duniani hilo ni jibu rahisi la kusema fulani kafariki kwa COVID.

Pili, COVID inaweza kuua kwa njia mbili. Moja kama ugonjwa wenyewe. Pili, kuwa sababu ya kifo kwa wale wenye maradhi ya kudumu 'underline disease'. Kwa mfano mgonjwa wa moyo tayari anatatizo katika mifumo inayohusisha damu na upumuaji. Kuingia kwa Corona kwa mgonjwa huo kuna chagiza vifo

Kwahiyo ni fair kusema tatizo lililopo linachukua nafasi katika mazingira yaliyopo. Kutokana na kuficha ficha ukweli kwanini alaumiwe atakayesema kila kifo ni Corona? Hata kama si kweli, hoja ni kuwa wapi takwimu za kupinga hoja hiyo?


Kuhusu chanjo, ije tu. Tutachanja kila mmoja kwa hiari yake. Mradi tu msihamishe magoli kutaka kulazimisha ambao hawatachanjwa wachanjwe. Wala pasiwe na vizuizi au ubaguzi kwa waliochanjwa au wasiochanjwa.

Kwa anayeelewa, atusaidie ukweli kuhusu yafuatayo:

1. Mpaka sasa zipo chanjo kadhaa zilizo sokoni. Tuchukue ipi? Ya China, Urusi, Uingereza, Marekani, au ya Uganda (inayotajwa kuwa mbioni kutengenezwa)?

2. Pamekuwa na maneno mitandaoni kwamba chanjo zilizoko hazizuii aliyechanjwa kuambukizwa virusi vya korona. Je ni kweli?

3. Pamekuwa na maneno mitandaoni kwamba chanjo zilizoko hazizuii aliyechanjwa kuambukiza wengine virusi vya korona. Je ni kweli?

4. Pamekuwa na maneno mitandaoni kwamba chanjo zilizoko hazizuii aliyechanjwa kuumwa COVID-19, ila uwezekano mkubwa hataumwa sana. Je ni kweli?
Yes, nakubaliana nawe 100%, chanjo iletwe atakaye apewe asiyetaka hiari yake.

Kitendo cha kuzuia chanjo kwa imani binafsi ni kuwanyima watu haki za kuamua maisha yao.

Kila mmoja apewe nafasi kama zile za wachemsha majani, maombi, sala n.k.

Habari za mitandaoni zipo tu na zitatoka katika vyanzo tofauti. Muhimu ni kuchuja information

Nitajibu kwa ujumla: Ni lazima uelewe sayansi ya vaccine. Inafanyaje kazi na inatengenezwa vipi n.k.

Vaccine zinatengenezwa kutoka vyanzo tofauti, iwe wadudu waliopunguzwa nguvu, wadudu waliouawa, au sehemu za wadudu zinazoleta ''immune response''

Immune response ni namna mwili unavyojenga antibodies baada ya ku introduce vaccine katika mwili.

Uwepo wa antibodies ndio utajenga kinga dhidi ya maradhi husika kwasababu antibodies ni specific

Mili yenye udhaifu inaweza kutotoa immune response na hivyo kutojenga antibodies.

Watu wenye maradhi yanayodhoofisha immunity iwe HIV, TB, Cancer au watu wanaotumia dawa zinazopunguza immunity wanaweza kutotoa antibodies na hivyo kutokuwa na immune response.

Chanjo inaweza kuwa na matokeo tofauti kutokana na factors tofauti.

Kuhusu chanjo ipi inafaa; hili linahitaji tathmini tu. Kuna chanjo zimekuwa proved na zingine zipo njiani

Ni suala la kitaalaamu la kuchukua takwimu na kuzifanyia tathmini na watu wenye credibility
Maprofesa wetu wamepoeza credibility , tuseme ukweli hata kama unauma

Maprofesa wanaweka taaluma zao makabatini wakihubiri vitu hadi unajiuliza inatokeaje hivi! Profesa!

Na wala wasihusishwe viongozi wala mananasi na kukimbia hovyo mitaani maana hawana credulity yoyote
Hawa wanaoonyesha mananasi na maembe ni tiba ni waganga njaa na opportunists tu

Tunaweza kulipa wataalam kutoka nje!
Yes kutoka nje maana hawa wakwetu wanaojenga mabanda ya kufikiza na kuandikia wagonjwa madogori hawana credibility. Huu ni ukweli mchungu , Covid imetuonyesha ubovu wa wataalam wetu.

Just think about this, hivi unatoaje muongozo wa Covid na Misitu , usafiri wa anga na discharge ukaacha maeneo kama masoko, dala dala, mabasi ya abiria , meli n.k.?

Mbuzi alaumiwe
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,857
2,000
.....
Nitajibu kwa ujumla: Ni lazima uelewe sayansi ya vaccine. Inafanyaje kazi na inatengenezwa vipi n.k. ...

Now, that you mention science of vaccine: there are some claims that the vaccines are not actually vaccines, but they are gene-therapy, not conforming to CDC's own definition of a vaccine; what is the truth?
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,111
2,000
Now, that you mention science of vaccine: there are some claims that the vaccines are not actually vaccines, but they are gene-therapy, not conforming to CDC's own definition of a vaccine; what is the truth?
Hapa ndipo kuna tatizo la mitandao, misinformation

Kuhusu hili, kwanza niseme 'Factually incorrect''

Gene therapy unaongelea modification of gene kwa mechanism tofauti ili kukabiliana na maradhi ya gene

Gene therapy una modify gene kwa ajili ya kutibu au kuponya (treat or cure)
Hapa unaongelea gene

Vaccine unaongelea introduction of 'antigens ' ili ku stimulate the antibodies productions against specific agent
Hapa unaongelea antigens and antibodies

Corona Virus unaongelea viral infection (kuambikiza) kunakosababisha madhara kwa njia tofauti.

Vaccine ya Corona imelenga ku introduce antigen ili kuwezesha mwili kutoa antibodies against corona virus

Hili ni somo pana sana, ninachotaka uelewe ni kuwa '' gene therapy siyo sawa na vaccination''
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,857
2,000
Vaccine ya Corona imelenga ku introduce antigen ili kuwezesha mwili kutoa antibodies against corona virus
Asante. Hizo vaccines za corona, wanasema ni zinatumia virusi vya adenovirus; jambo ambalo linatajwa kuongeza hatari ya maambukizi ya VVU. "Roll-out of an effective SARS-CoV-2 vaccine globally could be given to populations at risk of HIV infection, which could potentially increase their risk of HIV-1 acquisition." -- chapisho kwenye jarida la Lancet. Hilo unaliongeleaje?

Kuhusu gene-therapy, hizi chanjo zimetajwatajwa kuwa zinatumia teknolojia ya mRNA. Hili nalo limekaaje?

CDC na FDA za Marekani zimesitisha matumizi ya chanjo ya korona ya Johnson & Johnson. Wanasema, pameripotiwa "...cases of a rare and severe type of blood clot in individuals after receiving the J&J vaccine. In these cases, a type of blood clot called cerebral venous sinus thrombosis (CVST) was seen in combination with low levels of blood platelets (thrombocytopenia)". Kwako Mwalimu Kashasha Nguruvi3 , tuelezee hii ikoje.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,111
2,000
Asante. Hizo vaccines za corona, wanasema ni zinatumia virusi vya adenovirus; jambo ambalo linatajwa kuongeza hatari ya maambukizi ya VVU. "Roll-out of an effective SARS-CoV-2 vaccine globally could be given to populations at risk of HIV infection, which could potentially increase their risk of HIV-1 acquisition." -- chapisho kwenye jarida la Lancet. Hilo unaliongeleaje?
Kwasababu ya misinformation itabidi nirudi kuangalia kama kweli ni kutoka Lancent.

Nilitarajia kusoma mjadala katika British Medical Journal, New England Medical Journal au JAMA! Sijaona

Pili, nikutaarifu kuwa kuna kusoma kwa kusoma na kusoma kwa kuelewa. Hukusoma kwa kuelewa

Mwanzo mwa andiko hilo(kama ni kweli) limeanza hivi '' We are writing to express our concern''

Hapa maana yake kuna watu wameandika kueleza shaka yao hivyo ni maoni yao wala si facts.

Andiko hilo halihusiani na Vaccines zilizopo na ushahidi ni huu

Recombinant- Kwa vaccines zilizopo hakuna recombinants na hapa wameeleza ni katika study phase 1

Walichokiona ni increased risk ya wanaume kupata HIV tena wakieleza risk hiyo kama ile ya kutotahiriwa(uncircumcised).

Nikuache kwanza urudi kusoma andiko ukiwa na key words hizi
Recombinant, Phase 1, Increased risk, HIV acquisitions.
Kuhusu gene-therapy, hizi chanjo zimetajwatajwa kuwa zinatumia teknolojia ya mRNA. Hili nalo limekaaje?
mRNA protein like kama ilivyo DNA.

Kuna uwezekana ikatumika katika gene therapy kwasababu mechanism za gene therapy ni nyingi ikiwemo kutengeneza copy za gene ili kutibu maradhi au mapungufu.

mRNA ni possible kwasababu hii ni messanger RNA inaweza kutoa copy kwa njia nyingi.
Somo ni pana tuachie hapo kabla hujachanganyikiwa
CDC na FDA za Marekani zimesitisha matumizi ya chanjo ya korona ya Johnson & Johnson. Wanasema, pameripotiwa "...cases of a rare and severe type of blood clot in individuals after receiving the J&J vaccine. In these cases, a type of blood clot called cerebral venous sinus thrombosis (CVST) was seen in combination with low levels of blood platelets (thrombocytopenia)".
Yes kuna taarifa za AstraZeneca kusababisha blood clot ingawa hakuna uthibitisho rasmi. Hali hii imeripotiwa nchi za Ulaya na Jana kuna taarifa za tatizo hilo kutokea nje ya Ulaya.

Nafuatilia ingawa ''Bundle' za Tanzania zinanyima mawasiliano kutoka hapa Kicheba Muheza na DC , London n.k. Nikipata taarifa nitakueleza

Yes FDA wamerudi mezani baada ya watu 15 kuonyesha serious side effects.

Kwa majuha hii ni mada na washamba waliitumia sana kudanganya watu .

Ni hivi vaccines zinatengeneza katika njia mbali mbali, lakini muhimu ni 'vehicle' ya vaccines.

Hizi ni protein ndogo sana lazima ziwe katika volume fulani kuweza kuwa injected na kuleta

Kila kampuni ina ingredients zake ndiyo maana kuna tofauti ya kuhifadhi. Hizo ingredients zinaweza kuwa na matatizo kwa baadhi ya watu.

Kumbuka, hakuna dawa ambayo ni 100% bila kuwa na makando kando.
Muhimu ni benefit risk ratio ndio utasikia watalaam pale Paris wakisema '' the benefit outweighs the risks'

Kwa nchi za wenzetu maisha ya mtu 1 yana thamani.

Hata kama watu milioni 300 wametumia vaccines ikitokea tatizo ambalo ni 0.0001% bado linafanyiwa kazi kwasababu kwa mtu aliyeathirika ni 100% na lengo ni kuponya

Hawa ni tofauti na washamba wanaosema 'hata wakifa hawatakufa wote'' wasiothamini maisha ya watu

Kwahiyo Johnson and Johnson au AstraZeneca kuwa na side effects ni jambo lililotarajiwa.
Watu wanadhurika na maji ya kawaida yenye PH 7 seuse dawa?

Muhimu hapa ni je, watu wangapi wametumia na nini chance ya watu kauthirika?

Leo kuna mahali wamesema the chances ni 1 in a milllion , kabla sijamaliza mawasilian '' Bundle' ikakata ! nchi masikini hizi

Kwako Mwalimu Kashasha Nguruvi3 , tuelezee hii ikoje.
Yes utafanya 'sarcasm' etc, lakini maandishi yangu yana prove kuwa sahihi. Nilisema chanjo wapambe wakazogoa leo wamesimama katika viambaza, mbuzi kala mkeka watakalia nini?

Taifa letu limeumizwa sana kwa maamuzi yasiyozingatia sayansi. Leo wanasayansi wanaibuka kutoka katika madema ya kufikiza moshi na kusema eti kuna miongozo ya watu wa misitu, wasafiri wa anga na hata dischargeReal? kwamba haya ni makundi yenye risk? Real!!!

Kundi lisilojua hata priorities ndio kashasha. Ni aibu kubwa sana.

Ni kundi lile lile lililokubali mabanda ya kufukiza huku Maprofesa wakitukuza Togwa na mitindi bila ushahidi

Tunasema hivi, hatuhitaji kamati , tunahitaji Chanjo leo.

Kama unadhani ujanja ni ghali basi jaribu Ushamba!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom