Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,408
- 31,392
AHSANTE SANA TLS
Chama cha kitaaluma cha mawakili na wanasheria nchini kimepita na kinapita katika nyakati mgumu
Ugumu unatokana na kuingiliwa na hata kutungiwa sheria zinazolenga kukidhoofisha
Ukifuatia kwa umakini TLS ina misimamo thabiti na kusimamia kwa dhati taaluma ya sheria, wanasheria na masilahi mapana ya umma (public interest)
Wiki chache zilizopita baraza la chama hicho lilisimama na kueleza tatizo la Corona na jinsi lilivyoathiri wanachama wake lakini pia kwa ukubwa wake katika nchi yetu na linavyoathiri jamii.
Msimamo huo hakuwa rahisi lakini ulikuwa wa lazima kwa masilahi ya chama na umma.
Ipo video nyingine kutoka kwa kiongozi wa TLS Bw.
Nshala likieleza mambo kadhaa kwa ufasaha wake bila kupendelea au kuuma maneno , bila kujikomba au kuudhi.
Katika salam zake kwa Rais Mama Samia Suluhu , TLS imeanza kwa kueleza matarajio yake kwa kiongozi huyo
TLS imeongelea umuhimu wa utawala wa sheria na kikaangazi agenda ya katiba mpya kwa nchi.
Baraza likazungumzia umuhimu wa kukumbatia sayansi katika nyakati hizi za Corona
TLS haikucha kuzungumzia vymbo vya sheria , mahakama na hata mawakili kusimamia misingi ya sheria
Orodha ya waliyonena inaendelea kwa mtazamo wa masuala ya jamii , nchi na dunia kwa ujumla wake
Kikubwa zaidi ni TLS kuutendea uma haki kwa kueleza utaratibu unaopaswa kufuatwa sasa hivi.
Wanasheria hao wamebaini uwepo wa upotoshaji wa makundi ya jamii hasa kuhusiana na katiba na kuwachanganya wananchi.
TLS ikaeleza kwa kina nini kifanyike katika wakati huu wa kihistoria kwani nchi haijawahi kupitia haya.
Ilichokifanya TLS ni kutimiza wajibu wake kwa umma na kuhakikisha unatetea masilahi mapana ya umma.
Pengine TLS kama walivyo wananchi wengine wenye uelewa walijiuliza kuhusu kikao cha baraza la mawaziri. TLS imefafanua kiapo hakivushwi bali kuhamishwa kwa kiapo kipya
Ukipata fursa ya kutazama au kusoma taarifa ya TLS kuna kitu utabaini.
Baraza hilo ni moja ya mabaraza muhimu na yanayojitambua nchini.
Pengine ule msemo wa 'mwembe wenye matunda hupopolewa mawe' unadhihirika hapa.
Kuna cha kujifunza kwa vyama vya kitaaluma nchini.
Vingi vimebaki kuwa wapiga debe bila kujua hata miriindimo ya debe hilo.
Katika nyakati ngumu za dunia kama hizi za Corona tulitegemea vyama husika kushika hatamu, kinyume chake baadhi vimegeuka kuwa matawi ya chama.
Kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa ni kosa.
Vyama vya kitaaluma kama kile cha Madaktari( MAT), Wauguzi, Wahindisi n.k vina nafasi ya kujirekebisha na kurejea katika misingi na malengo ya uwepo wake.
Vyama hivyo vinapaswa kuiangalia TLS kama mfano na kioo.
Inasikitisha pale TLS inapokabiliana kwa ujasiri na mambo yaliyopaswa kusemwa na vyama vingine.
TLS inaweza kuwa si timilifu lakini kuna kitu cha kusema, ni chama kinachojielewa
Ahsante kwa kuitendea taaluma yenu haki na kuisadia jamii.
Tusemezane