kaligopelelo
JF-Expert Member
- Jun 20, 2013
- 2,764
- 3,940
Habarini wapendwa, poleni kwa majukumu.
Niingie moja kwa moja kwenye maudhui, kama inavyofahamika hivi sasa dunia inapita kwenye kipindi kigumu sana ambacho kwa hakika dunia inajitengenezea historia kubwa kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa covid-19 ambao umenguliwa china mwishoni mwa mwaka 2019.
Ugonjwa huu umefanikiwa kuzua kwa taharuki kwa watu wengi ulimwenguni kutokana na Kasi yake ya maambukizi na kuenea katika nchi mbalimbali licha ya tahadhari zinazochukuliwa ili kuweza kuukabili ugonjwa huo.
Mpaka sasa ugonjwa umesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani kote huku wengi wao wakiwa ni wazee.
Mipaka ya nchi nyingi duniani imefungwa,miji mingi imewekwa karantini na watu wake hawaruhusiwi kutoka ndani kiholela kama ambavyo miji ilikuwa kabla ya ugonjwa kuingia.
Pamoja na miji kuwekwa lockdowns lakini pia dunia imeshuhudia viongozi wakuu katika nchi mbalimbali wakizuia mikusanyiko ya watu katika kile kinachodaiwa kuwa ni jitihada za kukabiliana na COVID-19. Ukianza china kufunga shule zao na kuzuia mikusanyiko Sasa sehemu kubwa ya dunia inafanya hivyo kama sio dunia yote.
Aidha katika kuzuia mikusanyiko kumbi za starehe zimefungwa,madangulo mbalimbali hayafanyi kazi tena Sasa hivi. Bar nazo zimefungwa katika maeneo mengi na maeneo mengine kama ilivyo uingereza mpaka migahawa kwenye miji mikubwa imefungwa pia.
Pamoja na hayo yote hakuna malalamiko hata Kama baadhi ya watu walizoea kujirusha kwenye kumbi za starehe ifikapo mwishoni mwa wiki. Lakini wasanii na watumbuizaji mbalimbali wamepangua ratiba zao kupisha COVID-19. Ligi mbalimbali zimesimama duniani kote, lakini hii haiwafanyi hata wale wapenzi wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu waweze kukaidi amri ya kutokukusanyika lakini yote hayo ni hofu ama kuchukua tahadhari.
Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi kutoka kwenye kichwa cha habari hapo juu,nimeona kuwa mambo mengi ambayo yalikuwa yanaonekana kama ni magumu kuachwa au kuyazuia kwa kipindi hiki yamewezekana kuachwa au watu kujizuia nayo. Miongoni mwa mambo hayo ya anasa nimeyataja hapo juu na mengine sijayataja,ni dhahiri yalikuwa yanakemewa na viongozi mbalimbali wa dini na kuwataka watu waweze kuachana nayo.
Kwa kumalizia hii ilikuwa ni tafakari yangu binafsi hivyo ningewaomba wakosoaji wakosoe kinidhamu na wachangiaji wengine waongeze hoja za msingi ambazo mimi nimeshindwa kuzidiriki.
Ahsanteni Sana.