COVID-19 inavyoacha funzo la Dunia bila anasa inawezekana

kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Habarini wapendwa, poleni kwa majukumu.

Niingie moja kwa moja kwenye maudhui, kama inavyofahamika hivi sasa dunia inapita kwenye kipindi kigumu sana ambacho kwa hakika dunia inajitengenezea historia kubwa kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa covid-19 ambao umenguliwa china mwishoni mwa mwaka 2019.

Ugonjwa huu umefanikiwa kuzua kwa taharuki kwa watu wengi ulimwenguni kutokana na Kasi yake ya maambukizi na kuenea katika nchi mbalimbali licha ya tahadhari zinazochukuliwa ili kuweza kuukabili ugonjwa huo.

Mpaka sasa ugonjwa umesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani kote huku wengi wao wakiwa ni wazee.

Mipaka ya nchi nyingi duniani imefungwa,miji mingi imewekwa karantini na watu wake hawaruhusiwi kutoka ndani kiholela kama ambavyo miji ilikuwa kabla ya ugonjwa kuingia.

Pamoja na miji kuwekwa lockdowns lakini pia dunia imeshuhudia viongozi wakuu katika nchi mbalimbali wakizuia mikusanyiko ya watu katika kile kinachodaiwa kuwa ni jitihada za kukabiliana na COVID-19. Ukianza china kufunga shule zao na kuzuia mikusanyiko Sasa sehemu kubwa ya dunia inafanya hivyo kama sio dunia yote.

Aidha katika kuzuia mikusanyiko kumbi za starehe zimefungwa,madangulo mbalimbali hayafanyi kazi tena Sasa hivi. Bar nazo zimefungwa katika maeneo mengi na maeneo mengine kama ilivyo uingereza mpaka migahawa kwenye miji mikubwa imefungwa pia.

Pamoja na hayo yote hakuna malalamiko hata Kama baadhi ya watu walizoea kujirusha kwenye kumbi za starehe ifikapo mwishoni mwa wiki. Lakini wasanii na watumbuizaji mbalimbali wamepangua ratiba zao kupisha COVID-19. Ligi mbalimbali zimesimama duniani kote, lakini hii haiwafanyi hata wale wapenzi wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu waweze kukaidi amri ya kutokukusanyika lakini yote hayo ni hofu ama kuchukua tahadhari.

Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi kutoka kwenye kichwa cha habari hapo juu,nimeona kuwa mambo mengi ambayo yalikuwa yanaonekana kama ni magumu kuachwa au kuyazuia kwa kipindi hiki yamewezekana kuachwa au watu kujizuia nayo. Miongoni mwa mambo hayo ya anasa nimeyataja hapo juu na mengine sijayataja,ni dhahiri yalikuwa yanakemewa na viongozi mbalimbali wa dini na kuwataka watu waweze kuachana nayo.

Kwa kumalizia hii ilikuwa ni tafakari yangu binafsi hivyo ningewaomba wakosoaji wakosoe kinidhamu na wachangiaji wengine waongeze hoja za msingi ambazo mimi nimeshindwa kuzidiriki.

Ahsanteni Sana.
20200319064817_-1406712192_480_293_webp.jpg
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Hujazingatia kuwa kwa kufungwa hizo kumbi sijui bar n.k kuna athiri uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi (dunia) kiujumla.

Hujafikiri nje ya box mkuu. Fikiri waliokuwa wanaendesha maisha yao kwa kufanya kazi hizo sehemu je wataingiza vipi kipato?
Kifupi kama hawafi kwa kukosa pesa kwa njia hiyo, maana yake wanaweza kupata pesa kwa njia iliyokuwa bora zaidi ya ile. Tatizo ni mazoea tu kwenye shughuli binfsi.
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Ikumbukwe kabla ya ugonjwa wa Corona haujafika Tanzania, Bavicha na chadema kwa ujumla walikuwa wakikesha mitandaoni wakiombea Corona ije ili wamkomoe na kumcheka rais Magufuli!.

Mwana jamii forum anayeitwa technically alileta Uzi humu akiombea na kushangaa kwa nini Corona haifiki haraka Tanzania!, Naam kama ilivyoandikwa aombacho mtu ndiyo hupewa, kama alivyoomba technically Corona imekuja Tanzania na hatua ya kwanza imeshambulia familia ya boss wake Freeman Mbowe!, nadhani sasa technically atakuwa anarukaruka kwa furaha sana huko aliko

Tuwaonye tu vijana wa chadema kuwa Mungu hana mchezo, mahaba yenu kwa Mbowe yasiwatoe ufahamu na kuanza kuiombea mabaya nchi mkidhani mnamkomoa rais Magufuli.
Sasa hivi mnamkejeli Makonda kwa kusema ni tasa mnasahau kuwa HalimaMdee ana miaka 45 na hana mtoto wala kutundikwa mimba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba huu uzi usiharibiwe na wanasiasa.binafsi niko mbali na siasa badala yake tujikite kwenye maudhui halisi.
 
DIVIDEND

JF-Expert Member
Jan 15, 2017
1,822
2,000
Kwahiyo wewe umeona bar na kumbi za starehe tu.
Hoja yako ingelikuwa na mantiki kama shughuli nyingine zingeendelea kama kawaida alafu bar na kumbi za starehe tu ndio zikawa zimefungwa.
Ni sawa na kusema corona inaacha funzo kuwa dunia bila mikusanyiko na shughuli za kiuchumi inawezekana
 
bogie

Member
Oct 30, 2015
8
45
Kama unazani Covid 19 imekuja kutoa funzo kwa hao tu wewe unaozani walikuwa wanafanya starehe na hanaxa umekoxea kidogo, Covid 19 imekuja kuharibu uchumi na maixha ya watu kiujumla na xio kutoa funzo kama unavozani kwaxababu kama ingekuwa inawahadhibu wanaofanya izo hanaxa na starehe tu kweli ningekubaliana na wewe kuwa imekuja kutoa funzo kwa wale wote wanaopenda hanaxa lakini ni tofauti kabixa! Fikiria na upande wa pili xio unafikiria upande mmoja tu! Covid 19 haijali kama unafanya, ulikuwa unafanya au utafanya hanaxa, ukikaa xaiti yenyewe inaxema na wewe tu mze! Ni hatari jamani xio jambo la kufurahia na kudai eti limetoa funzo wakati nchi zinapoteza nguvu kazi nyingi za watu katika mataifa yao!

Soma vizuri bandiko langu,haujanielewa.
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Kwahiyo wewe umeona bar na kumbi za starehe tu.
Hoja yako ingelikuwa na mantiki kama shughuli nyingine zingeendelea kama kawaida alafu bar na kumbi za starehe tu ndio zikawa zimefungwa.
Ni sawa na kusema corona inaacha funzo kuwa dunia bila mikusanyiko na shughuli za kiuchumi inawezekana
Hoja yangu imejikita kwenye mambo ya anasa na ndio chukizo ndio maana yanakemewa.
 
MAGO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
1,943
2,000
Habarini wapendwa, poleni kwa majukumu.

Niingie moja kwa moja kwenye maudhui, kama inavyofahamika hivi sasa dunia inapita kwenye kipindi kigumu sana ambacho kwa hakika dunia inajitengenezea historia kubwa kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa covid-19 ambao umenguliwa china mwishoni mwa mwaka 2019.

Ugonjwa huu umefanikiwa kuzua kwa taharuki kwa watu wengi ulimwenguni kutokana na Kasi yake ya maambukizi na kuenea katika nchi mbalimbali licha ya tahadhari zinazochukuliwa ili kuweza kuukabili ugonjwa huo.

Mpaka sasa ugonjwa umesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani kote huku wengi wao wakiwa ni wazee.

Mipaka ya nchi nyingi duniani imefungwa,miji mingi imewekwa karantini na watu wake hawaruhusiwi kutoka ndani kiholela kama ambavyo miji ilikuwa kabla ya ugonjwa kuingia.

Pamoja na miji kuwekwa lockdowns lakini pia dunia imeshuhudia viongozi wakuu katika nchi mbalimbali wakizuia mikusanyiko ya watu katika kile kinachodaiwa kuwa ni jitihada za kukabiliana na COVID-19. Ukianza china kufunga shule zao na kuzuia mikusanyiko Sasa sehemu kubwa ya dunia inafanya hivyo kama sio dunia yote.

Aidha katika kuzuia mikusanyiko kumbi za starehe zimefungwa,madangulo mbalimbali hayafanyi kazi tena Sasa hivi. Bar nazo zimefungwa katika maeneo mengi na maeneo mengine kama ilivyo uingereza mpaka migahawa kwenye miji mikubwa imefungwa pia.

Pamoja na hayo yote hakuna malalamiko hata Kama baadhi ya watu walizoea kujirusha kwenye kumbi za starehe ifikapo mwishoni mwa wiki. Lakini wasanii na watumbuizaji mbalimbali wamepangua ratiba zao kupisha COVID-19. Ligi mbalimbali zimesimama duniani kote, lakini hii haiwafanyi hata wale wapenzi wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu waweze kukaidi amri ya kutokukusanyika lakini yote hayo ni hofu ama kuchukua tahadhari.

Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi kutoka kwenye kichwa cha habari hapo juu,nimeona kuwa mambo mengi ambayo yalikuwa yanaonekana kama ni magumu kuachwa au kuyazuia kwa kipindi hiki yamewezekana kuachwa au watu kujizuia nayo. Miongoni mwa mambo hayo ya anasa nimeyataja hapo juu na mengine sijayataja,ni dhahiri yalikuwa yanakemewa na viongozi mbalimbali wa dini na kuwataka watu waweze kuachana nayo.

Kwa kumalizia hii ilikuwa ni tafakari yangu binafsi hivyo ningewaomba wakosoaji wakosoe kinidhamu na wachangiaji wengine waongeze hoja za msingi ambazo mimi nimeshindwa kuzidiriki.

Ahsanteni Sana.
View attachment 1399029
Lakini kumbuka hata makanisani/misikitini hatuendi tena!!!

Kwa vyovyote vile hili linaonekana kuwa jambo LA muda mfupi ila athari zake zitakuwa za muda mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Lakini kumbuka hata makanisani/misikitini hatuendi tena!!!

Kwa vyovyote vile hili linaonekana kuwa jambo LA muda mfupi ila athari zake zitakuwa za muda mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijaliona katazo la watu kutokwenda makanisani na misikitini kokote kule. Lakini hata Kama likiwepo watu wafanya iabada wanaendelea kuabudu na kuomba popote pale walipo.
 
Chrismoris

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
13,208
2,000
Habarini wapendwa, poleni kwa majukumu.

Niingie moja kwa moja kwenye maudhui, kama inavyofahamika hivi sasa dunia inapita kwenye kipindi kigumu sana ambacho kwa hakika dunia inajitengenezea historia kubwa kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa covid-19 ambao umenguliwa china mwishoni mwa mwaka 2019.

Ugonjwa huu umefanikiwa kuzua kwa taharuki kwa watu wengi ulimwenguni kutokana na Kasi yake ya maambukizi na kuenea katika nchi mbalimbali licha ya tahadhari zinazochukuliwa ili kuweza kuukabili ugonjwa huo.

Mpaka sasa ugonjwa umesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani kote huku wengi wao wakiwa ni wazee.

Mipaka ya nchi nyingi duniani imefungwa,miji mingi imewekwa karantini na watu wake hawaruhusiwi kutoka ndani kiholela kama ambavyo miji ilikuwa kabla ya ugonjwa kuingia.

Pamoja na miji kuwekwa lockdowns lakini pia dunia imeshuhudia viongozi wakuu katika nchi mbalimbali wakizuia mikusanyiko ya watu katika kile kinachodaiwa kuwa ni jitihada za kukabiliana na COVID-19. Ukianza china kufunga shule zao na kuzuia mikusanyiko Sasa sehemu kubwa ya dunia inafanya hivyo kama sio dunia yote.

Aidha katika kuzuia mikusanyiko kumbi za starehe zimefungwa,madangulo mbalimbali hayafanyi kazi tena Sasa hivi. Bar nazo zimefungwa katika maeneo mengi na maeneo mengine kama ilivyo uingereza mpaka migahawa kwenye miji mikubwa imefungwa pia.

Pamoja na hayo yote hakuna malalamiko hata Kama baadhi ya watu walizoea kujirusha kwenye kumbi za starehe ifikapo mwishoni mwa wiki. Lakini wasanii na watumbuizaji mbalimbali wamepangua ratiba zao kupisha COVID-19. Ligi mbalimbali zimesimama duniani kote, lakini hii haiwafanyi hata wale wapenzi wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu waweze kukaidi amri ya kutokukusanyika lakini yote hayo ni hofu ama kuchukua tahadhari.

Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi kutoka kwenye kichwa cha habari hapo juu,nimeona kuwa mambo mengi ambayo yalikuwa yanaonekana kama ni magumu kuachwa au kuyazuia kwa kipindi hiki yamewezekana kuachwa au watu kujizuia nayo. Miongoni mwa mambo hayo ya anasa nimeyataja hapo juu na mengine sijayataja,ni dhahiri yalikuwa yanakemewa na viongozi mbalimbali wa dini na kuwataka watu waweze kuachana nayo.

Kwa kumalizia hii ilikuwa ni tafakari yangu binafsi hivyo ningewaomba wakosoaji wakosoe kinidhamu na wachangiaji wengine waongeze hoja za msingi ambazo mimi nimeshindwa kuzidiriki.

Ahsanteni Sana.
View attachment 1399029
Kupitia unachokiita anasa kuna watu wanaendesha maisha yao
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Kupitia unachokiita anasa kuna watu wanaendesha maisha yao
Inaweza kuwa hoja ya msingi ya watu kuacha kukataza uovu wao?
Serikali inakataza biashara ya madawa ya kulevya,kwa hoja yako huoni kuwa serikali haiwatakii mema wafanyabiashara wa madawa ya kulevya?
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Nafikiri uelewa wako ndio mdogo zaidi, kwasababu sijaona mtu hata mmoja amesupport hoja yako.
Kubali tu kuwa umetoa boko, amna hoja hapa
Kumbe unafuata mkumbo? Sijatoa hoja kulazimisha watu wawaze Kama mimi.
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Kutokuwepo movements zozote wewe umeona ni mafanikio?biashara zimeshuka,uchumi wa dunia umetikisika vifo vingi wewe unaona mafanikio gani hapa mwenzetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ungesoma vizuri ungeona sehemu ambapo nimeandika kuwa ugonjwa huu umezua taharuki kwa watu wengi na kusababisha vifo. Wapi nimeandika au kuashiria furaha kutoka kwenye thread yangu?
 
Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
9,584
2,000
Umenena kweli.
Habarini wapendwa, poleni kwa majukumu.

Niingie moja kwa moja kwenye maudhui, kama inavyofahamika hivi sasa dunia inapita kwenye kipindi kigumu sana ambacho kwa hakika dunia inajitengenezea historia kubwa kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa covid-19 ambao umenguliwa china mwishoni mwa mwaka 2019.

Ugonjwa huu umefanikiwa kuzua kwa taharuki kwa watu wengi ulimwenguni kutokana na Kasi yake ya maambukizi na kuenea katika nchi mbalimbali licha ya tahadhari zinazochukuliwa ili kuweza kuukabili ugonjwa huo.

Mpaka sasa ugonjwa umesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani kote huku wengi wao wakiwa ni wazee.

Mipaka ya nchi nyingi duniani imefungwa,miji mingi imewekwa karantini na watu wake hawaruhusiwi kutoka ndani kiholela kama ambavyo miji ilikuwa kabla ya ugonjwa kuingia.

Pamoja na miji kuwekwa lockdowns lakini pia dunia imeshuhudia viongozi wakuu katika nchi mbalimbali wakizuia mikusanyiko ya watu katika kile kinachodaiwa kuwa ni jitihada za kukabiliana na COVID-19. Ukianza china kufunga shule zao na kuzuia mikusanyiko Sasa sehemu kubwa ya dunia inafanya hivyo kama sio dunia yote.

Aidha katika kuzuia mikusanyiko kumbi za starehe zimefungwa,madangulo mbalimbali hayafanyi kazi tena Sasa hivi. Bar nazo zimefungwa katika maeneo mengi na maeneo mengine kama ilivyo uingereza mpaka migahawa kwenye miji mikubwa imefungwa pia.

Pamoja na hayo yote hakuna malalamiko hata Kama baadhi ya watu walizoea kujirusha kwenye kumbi za starehe ifikapo mwishoni mwa wiki. Lakini wasanii na watumbuizaji mbalimbali wamepangua ratiba zao kupisha COVID-19. Ligi mbalimbali zimesimama duniani kote, lakini hii haiwafanyi hata wale wapenzi wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu waweze kukaidi amri ya kutokukusanyika lakini yote hayo ni hofu ama kuchukua tahadhari.

Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi kutoka kwenye kichwa cha habari hapo juu,nimeona kuwa mambo mengi ambayo yalikuwa yanaonekana kama ni magumu kuachwa au kuyazuia kwa kipindi hiki yamewezekana kuachwa au watu kujizuia nayo. Miongoni mwa mambo hayo ya anasa nimeyataja hapo juu na mengine sijayataja,ni dhahiri yalikuwa yanakemewa na viongozi mbalimbali wa dini na kuwataka watu waweze kuachana nayo.

Kwa kumalizia hii ilikuwa ni tafakari yangu binafsi hivyo ningewaomba wakosoaji wakosoe kinidhamu na wachangiaji wengine waongeze hoja za msingi ambazo mimi nimeshindwa kuzidiriki.

Ahsanteni Sana.
View attachment 1399029
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom