COVID-19 Imetukuta Watanzania kipindi kibaya sana. Pray for the nation

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Ndugu Watanzania na taifa kwa ujumla, mimi leo nakuja mbele yenu kuwaambia jambo moja zito sana na kiukweli naomba mnielewe. Nawaomba tuliombee taifa letu na viongozi wetu wasasa na wazee pia.

Hakuna asiyejua tunapita kipindi gani kama taifa na hakuna asiyejua kwa wakati huu mezani kwa Rais kuna maamuzi magumu kuchukuliwa kabla ya kuwepo kwa taifa hili mbaya kuliko yote maamuzi hayo ynamuitaji yeye na Mungu wake kuyachukua kwa niaba yetu sote Watanzania. Ni maamuzi magumu ni maamuzi yatakayoumiza wengi lakini yanatakiwa yachukuliwe japo sio lazima.

Tunapita kipindi kigumu sana kiukweli; serikali yetu kwa hakika na hali tuliyonayo ni dhahiri shahiri hawakuwa wanategemea yatatokea haya yametokea na kuharibu kila jambo jema lililokusudiwa na serikali ya awamu ya tano.

Kila mtu anasema la kwake na huenda lipo kundi linamlaumu mkuu wa nchi lingine linamsifia kila mtu, almradi kujikomba au kukosoa. Yote ni maoni japo kundi linamsifia Rais kwa asilimia kubwa lina kundi la wanafiki ndani na hawa mimi nawaona ni wabaya sana maana wamekuwa sehemu ya kumpotosha Rais.

Ndugu zangu, gari ikiwa kwenye safari ndefu na mwendo mkali huwezi isimamisha kwa ghafla na kuizima maana lolote laweza tokea. Hivi ndivyo uchumi wetu ulivyokuwa before Covd-19 hivyo kusimamisha kila kitu kwa mara moja serikali itashindwa na tutakuwa kwenye hali mbaya sana.

Kwa bahati mbaya sana, samahani lakini kama kuna mtu atakwazika. Kwa mimi ninavyoona, kwa maoni yangu, sector binafsi kipindi hiki hatukujenga mahusiano mazuri ambapo katika nyakati kama hizi serikali ingetumia sector binafsi kujinasua ktk hali mbaya inayotaka kutokea kupitia taasisi kama TRA.

Hii sector badala ya kuwa rafiki wa serikali, nadhani wengi wana kila aina ya vilio na sasa Covid19 imeingia basi kila mmoja analia kwa namna yake; serikali ana kilio while sector binafsi ina kilio.

Wengi covid-19 imekuta hawana mitaji mizuri au wamepunguza uzalishaji basi ni tabu tupu. Ikumbukwe sector binafsi na serikali ni ndugu wawili wanaopaswa kupendana; yaani serikali ikiimarisha sector binafsi inaajiri Watanzania ambao serikali isingeweza waajiri. Wakati huo huo, serikali iinapanua wigo wa makusanyo while pp ya watu ikipanda na hivyo kuwa na mzunguko mzuri wa uchumi.

Sasa baada ya hayo yote, ni vyema tukajiandaa kisaikolojia hasa nyakati hizi ambapo ikiwa serikali itatangaza total lockdown, kuna kila dalili watu wengi watapoteza ajira, pia hali yetu huenda ikawa mbaya kuliko Kenya maana wakati Kenya atakuwa visa vinashuka sisi ndio tutakuwa tuna panda jambo litakuwa baya sana.

Ndio maana napinga siasa kuchukua nafasi katika kipindi hiki na tuwape wataalam nafasi wafanye kazi yao. Nje ya hapo tutalilia chooni.

Mungu ibariki Afrika, Tanzania na viongozi wake. Amen!
 
Hili janga la Corona, binafsi naona lipo kimkakati zaidi na mambo ya siri katika utawala wa dunia hii, ukiangalia utaona kwamba ilikuwa ni lazima kila nchi hili janga liingie kwa vyovyote vile.

Kulikuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kudhibiti hili janga lisiingie Afrika kabisa, lakini naona viongozi waliangalia tu likiwa linakuja.

Kama hofu ilikuwa ni kupoteza pesa na mapato kutoka nje, basi tulikuwa na nafasi kubwa ya kukaa chini na kuweka mipango na mikakati ya uzalishaji wa ndani ili kuongeza pato la ndani. Lakini ninachoona Corona ilikusudiwa kuingia kila nchi duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TumainiEl,

Umesema sawa ila umeweka Utanzania na kujifanya nice guy bila sababu na hakuna anayemlaumu mtu, sema hao usiotaka walaumiwe ndio kazi yao na huu ndio muda wao kuonyesha weledi wao. Hatuna sababu yeyote ya kujiandaa kusurubiwa sie tumeshakubali na kwa hakika silka na hulka ya viongozi wetu tunawajua sie wananchi tunaenda kupasuka tena sababu mara zote wenzetu wamekuwa wakilinda viongozi, serikali na wateule wao kwanza then ndio wananchi.

Sie wananchi tunanyanyua mikono juu kumshuru muumba kwa kuwaonyesha sio kweli kwamba wao ndio wako juu. Corona imefungua masikio ya watu kumjua mungu zaidi wakati huu, Siasa iliaminisha watu kuwa wanasiasa ndio wenye majibu ya kila kitu, wachache walioongea kipindi hiki dunia imeona uwezo wao.

Siunaona utanzania ulivyokugharimu yaani umemalizia kumuomba Mungu Ibariki, Afrika, Tanzania na viongozi wake kwa hiyo sie watu tusiokuwa viongozi hatumo katika maombi yenu hivi ndio vitu vinavyomkasirisha M/Mungu, Mungu Tubariki waafrika.
 
Dah umeongea kwa uchungu sana, kiukweli tunapitia wakati mgumu na ni Mungu pekee ndiye anaweza kutunusuru.

Watu wengi wanafanya masikhara kwenye hili lakini kiukweli kabisa hatari yake ni kubwa kwenye wakati wenyewe wa kupambana nalo na baada ya janga lenyewe Kwisha tutapambana na janga kubwa la kiuchumi ambalo litakuwa na madhara makubwa sana kama akili na nguvu za zaidi hazitatumika.

Hapo kwenye sekta binafsi nipakujutui sana maana ingekuwa strong ingeweza kuwa na msaada wakati huu kwa kuikopesha serikali ili ipambane au kuja kuinua uchumi utakaokufa baadaye.

Mungu ni mwema atatupitisha salama.
 
TumainiEl,
TRA imepeleka mambo kibabe sana. Sector binafsi ilishaumizwa siku nyingi zilizopita. Kwa sasa biashara zinasuasua. Utalii umekwama kabisa.

Kama kweli tunajipenda, leseni za madini kwa makampuni ambayo wanataka kuwekeza, zitolewe sasa. Maana it takes forever for some of those licenses to be issued.

Biashara za Kariakoo, zipewe msukumo mpya maana wenzetu wengi wamejifungia ndani. Sisi tuwe lango Lao la kufikisha mahitaji ya lazima.

Na tupende tusipende, gharama zetu za uendeshaji inabidi zishushwe. Haya mambo ya mtu anaenda kwenye mkutano na ndege halafu magari kadhaa yanafuatia barabarani, ni ufujaji wa mali za walipa kodi. Unless ni kiongozi mkubwa wa nchi, wengine waache kufanya hivyo.
 
Prayers don’t work. Anzeni social distancing na kuvaa mask acheni ushenzi. Mnaenda kukusanyika kwenye maombi mnaaambukizana kanisa zima.
 
"Hako kaugonjwa ni ka kawaidaa tuu wala kasitutishe, ni ugonjwa wa watu weupe kwa hiyo watanzania chapeni kazi kwerikweri,msitishike hata kidogo". Lumumba-Chair person
 
Back
Top Bottom