COVID-19 ilivyobadili maisha yako

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,001
112,648
Kirusi kipya cha Corona ndo habari ya dunia sasa hivi.

Dunia nzima sasa inakabiliana na tishio la maambukizi yake.

Kutokana na tishio hilo, watu imetubidi tubadili namna tuishivyo.

Yale mambo yaliyokuwa ya kawaida sasa si ya kawaida tena. Na yale ambayo ni mapya, kwa sasa ndo tunajifunza kuyazoea.

Mimi imenibidi nifanye mabadiliko kiasi. Baadhi ya mabadiliko ni ya kulazimishwa. Baadhi ni ya hiari.

1. Nimeacha kula kwenye migahawa ya Wachina. Sababu ni vile huu ugonjwa unasemekana umeanzia huko China kwenye soko la wanyama wa kila aina.

Kwenye hili hata hivyo naona nimechelewa sana. Kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikisikia stori kwamba Wachina huwa wanawalisha watu nyama za paka, mbwa, n.k.

Muda wote huu nimekuwa nikizipuuzia hizo stori. Ilikuwa nikienda kwenye ‘Chinese buffet’ nashindilia ile mi-satay chicken, sijui General Tso’s chicken, Mongolian beef na mazagazaga mengine. Nikitoka hapo kitumbo ndiiii, nimeshiba.

Kusema ukweli ni wao tu ndo wajua kama kweli walikuwa wanatulisha kile ambacho walikuwa wanadai ndicho.

Kuna nyakati hiyo mi-satay chicken inakuwa ina ladha ya ajabu ajabu ambayo hata haifanani na ladha ya kuku lakini mtu unajipa tu moyo na kujiambia ‘itakuwa ni vile viungo wanavyoweka ndivyo vyenye kubadili ladha’. Yawezekana nishakula hadi Popo bila hata kujua.

Ila kuanzia sasa hapana. Sitaki tena mi vyakula ya Kichina.

2. Kwa vile mikusanyiko ya watu inaendelea kupigwa marufuku, gym za kufanyia mazoezi nazo zimeanza kufungwa. Leo nimepata barua pepe yenye kunifahamisha kuwa gym niendayo kufanya mazoezi, kuanzia leo itafungwa hadi mnamo mwisho wa mwezi huu.

Wengine kwetu kwenda gym ni sawa na kwenda msikitini kila Ijumaa au kanisani kila Jumapili.

Sina jinsi. Ni kukubaliana tu na matokeo na kutafuta njia nyingine ya kupiga tizi.

7AA23DC4-0F94-43CD-833B-0D1C8592B9F7.jpeg


3. Shule nazo zimefungwa. Maofisi nayo pia. Watoto wanasoma kwa kutumia mtandao. Wazazi [wenye kuweza] wanafanyia kazi toka nyumbani.

4. Wiki ijayo nilikuwa na safari. Kwa sasa nadhani itabidi niiahirishe tu

5. Tulio wapenzi wa michezo kwa sasa hatujui hata tufanye nini maana michezo mingi imesimamishwa sasa hivi.

6. Kushinda ndani siku nzima tena kwa muda usiojilikana ni mateso. Huu sasa ndo muda wa kuangalia kilichomo kwenye DVR. DVR yangu imejaa kwa asilimia 99. Sitokosa vya kuangalia.

7. Nikichoka kuangalia TV, natafuta cha kugongea ili mradi siku iende. Old Town Liquor store baby.

90A3B902-CC55-4091-AB2F-E0D1089E4E04.jpeg


Siwezi kushinda nakunywa maji na juisi tu kwa siku nzima.

Ni muhimu kusahau kidogo madhila ya ulimwengu.

Je, wewe mdau maisha yako yamebadilikaje katika hiki kipindi cha Corona?
 
Gym imefungwa, nafanyia kazi from home, ratiba za bar weekend zimekuwa suspended, restaurants nyingi wanatoa service ya drive-thru tu.

Na hakuna dalili za mambo ku-reverse very soon. Balaa na nusu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa huku Afrika mambo bado hayajapamba moto...ila ngoma imeanza mdogomdogo tusubiri kwanza.Ila stock ya vikali ni muhimu!
 
Nilikuwa na safari ya Montreal kupitia bara la Uropa....next week..imeota mbawa.. till further notice..
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom