Covid-19 ikifikia hatua ya nchi kuingia kwenye lockdown, haya ndio mapendekezo yangu

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
9,354
2,000
Mosi.
Inabidi tukubali kuwa tayari nchi haina ujanja wowote wa kuepukana na janga hili kwani tayari wagonjwa tunao zaidi zaidi zitafutwe mbinu tu za kupunguza maambukizi.

Pili
Isifungwe miji yote bali baadhi ya miji ambayo itaonekana kinara wa maambukizi

Hii itasaidia shughuli kuendelea kwingineko ili kukabiliana na athari za kiuchumi n.k

Tatu
Na kama italazimika iwe kote nchini basi kule kusikokuwa na maambukizi mengi laweza tokewa tamko pasiwepo mikusanyiko zaidi ya watu 5 na hao wakae ktk umbali unaopendekezwa na wataalamu

Nne
Ikitokea serikali imeamua kuifunga nchi nzima basi imuangalie huyu anae ishi kwa wastani wa chini ya dola moja kumwezesha namna ya kuishi ktk kipindi chote cha lockdown

Tano
Kuchapana viboko na kulazimishana kujifumgia ndani kusiwepo mambo ya kizamani hayo, mwananchi mwenyewe akiona misiba minne nyuba za jirani atajiongeza na kukaa ndani pasipo shuruti

Hii inamaana kwamba ni ngumu raia kujifungia ndani afe kwa njaa wakati huohuo kwenye mji aanaoishi hakuna maambukizi ambayo yamesha tangazwa.

Sita
ongezeni na nyie.

Maoni yangu ya kuhitimisha

Raia tujitahidi kufuata maelekezo ya wataalamu, hakuna mwaansiasa au kiongozi yeyote iwe wa dini au kisiasa atakaye kuokoa na janga hili

Tahadhari utakayochukua ndio itaamua hatima yako juu ya ugonjwa huu.
 

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
2,478
2,000
Kwenye hili la lockdown tusiwafuate mataifa makubwa, kama Brazil wenyewe wamesurrender sisi ni akina nani mpaka tuweke lockdown?
Unforgetable
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
9,354
2,000
wale wacheza draft, karata n.k inadi kupunguza au kuacha ili kuepuka kupasiana mambukizi

mliozoea kuhesabu noti kwa kuloweka vidole midomoni au kuhesabu chochote kile mpak upakaze mate naomba muache kabisa

kushika koki mbayo imeshikw na mwenzako pasipo umakini kwa kujidanganya kuwa umenawa bado haita sidia chochote
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
5,843
2,000
Hahaha usiwape vichwa wataalam wa afya kwamba ndio wanaweza kutuokoa. Mbona wagonjwa hufia mahospitalini kila siku na hawafanyi lolote kuokoa?
Kifo kipo na hakuna mjanja so far. Unadhani huko wanako kufa hakuna wataalam wa afya? Ugonjwa hauna dawa, kupunguza misongamano ni kupunguza rate ya maambukizi sio kuzuia ugonjwa.
Mbona NZIGE walipita mbali, labda na Corona itapita huko huko, pigeni kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom